Dah! Pole kwa yaliyokukuta na yanayoendelea sasa. Hapo ndo uone maajabu ya msemo huo "Nani kama Mama"
1. Mama anathubutu kukataa mwanaye aliyemzaa kwa uchungu mwingi eti asilipiwe ada i.e. asiende kupata elimu. Inatisha. Katika hali ya kawaida hakuna mama atakayefanya hivyo. Lakini Mama huyo ameweza na amefanya. i.e. "Nani kama Mama" Utabaki mdomo wazi unashangaa.
2. Mama huyo huyo hapo na. 1, bila aibu wala hofu anapiga vizinga vya hela. Hiyo ni hela ambayo kimsingi imetokana na kile alichokuwa anakatazia. Katika hali ya kawida, mtu atakuwa na kigugumizi namna ya kujipendekeza au kula matunda yatokanayo na alichokikataa awali i.e. aliyofanya zamani - ni sawa na kuvuna shamba ambalo hakulima, kuotesha na kupalilia. Hiyo ni aina fulani ya Dhuluma. "Nani kama mama" Mama huyo ameweza.
Mwisho: Msemo huo hutumika kuhamasisha jamii yenye waMama wengi ili wakubali na waweze kushiriki katika maendeleo. Vinginevyo watakushangaza kwani wanao uthubutu wa ajabu sana.