Hivi kibongo bongo mtu asiye na degree even if ni mcute au handsome kiasi gani, huko kwenye ndoa huwa yuko romantic kweli, is he/she tasting good?
Binafsi Naona kama they are not romantic na hawajui lolote linaloendelea hapa duniani?
Chukulia mfano Diamond hana hata form six failure,ampate demu mwenye bcom degree ya hapo udsm, Diamond atakua na any point ya kuongea na huyo mpenzi wake kweli apart from uhuni huni wake tu?
Kwanza mimi si shabiki wa Diamond, na naweza kusema mapungufu mengi ya Diamind. Kuanzia kukisa elimu rasmi mpaka mambo mengi ya kike Wafaransa wanachokiita savoir faire.
Lakini, kwa kuangalia ujumla wa kazi ya Diamond, amefanya kazi jubwa sana, Waingereza wanasema "he is punching above his weight".
Kwa watu walio result oriented, Diamond ni zaidi ya degree, Diamond ni somo la kusomea degree au hata kufanyia thesis ya Ph.D.
Yani, kwa wenzetu wanaoenda na wakati, maisha na kazi za Diamond yanaweza kufanyiwa thesis na utafiti, mtu akapata Ph.D ya biashara ya muziki wa Tanzabia kwa kumsoma Diamond na kuandika chapisho la kitaaluma.
Sasa ukimsengenya mtu kama huyo kwamba hana degree, wewe nsiye utakuwa limbukeni wa kuthamini elimu ya makaratasi kuliko elimu ya vitendo.
Diamond katoa somo la elimu ya vitendo ambayo watu wachache sana wameweza kulitoa, degree or no degree.
Hebu soma watu wanavyomuandika hustle zake, despite all his shortcomings.
Ask any African music lover to name the biggest superstar on the continent, and chances are you’ll get some name out of Nigeria.
Watanzania wana kasumba sana ya kuthamini elimu ya makaratasi.
Kuna Mzee mmoja alikuwa Katibu Mkuu katika wizara nyeti Tanzania.
Alisema yeye hawezi kuongea na mtu asiye na degree. Hawana cha kuongea.
Baadaye yule mzee alipata kesi kubwa akafungwa siku nyingi sana.
Wale rafiki zake wenye degree wote waliogopa kwenda kumuona gerezani, wakiogopa kuhusishwa na kesi ile.
Katika watu waliokwenda kumuona gerezani, wachacge sana walikuwa na degree, wengi wao walikuwa ni wale ambao hawakuwa na degree.
Yule mzee alivyotoka gerezani alijua kuishi kwa kuheshinu watu wote bila kujali degree.
Hizi tabia za kuthamini sana degree ni ulimbujeni wa nchi masikini ambako degree inaonekana usomi, wakati degree ni kitu cha kawaida sana, kuna wasomi wengine ni autodidakcs tu