Pori lile sio poa, tumewahi zuiwa hapo enzi hamna lami, tunaitafuta Inyonga tupo na Land Cruiser LX ,tumetoka Sikonge kwenye majukumu X, tuliona Mjuba anatoka porini na chuma mgongoni kuingia kama anachungulia aone nani anakuja nahisi walikuwa wanalia mingo ndiga za abiria, tupo mwendo wa mateka, suka akatu alert tuwe tayari huku akiwa anapunguza mwendo, vioo vilishushwa na sisi upande wetu Wakurungwa wakazikoki kuzielekeza nje tayari kwa lolote kivyovyote. Yule mjuba akatokomea tena porini kama mshale na kukawa kimya na sisi tukaenda kusimama mbele maana kulikuwa na TaTa ya abiria tuliiacha nyuma kuisubiri. Ikapita tukaisindikiza tukaiacha tukasepa zetu bila kumstua dereva wala kuleta taharuki.