Hivi kwanini Mabasi kutoka Dar kwenda Mpanda, Katavi yanazuiwa kuendelea na safari yakifika Sikonge, Tabora?

Hivi kwanini Mabasi kutoka Dar kwenda Mpanda, Katavi yanazuiwa kuendelea na safari yakifika Sikonge, Tabora?

Dereva wenu ndie Mzembe. Angefika hapo kabla ya saa 3 usiku mngetoboa sasa Hapo Sikonge madereva wanapenda kulala kwa maksudi maaana wameoa Warabu koko wapo kibao so dereva anachelewa maksudi kufika ili akahudumie nyumba ndogo yake.

Siku nyingine Ongea na afande kiume uone ka hamjaruhusiwa.
Unahamasisha rushwa?
 
Wadau tumetoka Dar na Bus la HAPPY NATION saa 12 asubuhi na tumefika hapa Sikonge, Tabora Bus limezuiwa kuendelea na safari eti mpaka saa 12 asubuhi, eti kwa sababu njiani kuna mapori makubwa.

Kwa maoni yangu hii si sawa kabisa, yaani pamoja na jitihada kubwa za serikali kukamilisha barabara hii na sasa ni lami kutoka Dar mpaka Mpanda, bado tunawapotezea muda watanzania kukaa hapa masaa 8 kisa hatuwezi kuimarisha usalama?

Hivi tutajikwamua vipi na umasikini ikiwa tunapoteza muda kiasi hiki? Halafu sehemu yenyewe hakuna hata stend yenye facilities za kuhudumia hata abiria wa Bus mbili. Kingine cha kushangaza kwenye maamuzi yetu ni kwamba hivi unawezaje kuacha bus ilale Tabora mjini kwenye huduma nyingi halafu uje kuzuia ma Bus Sikonge?

Kwa staili hii ya kupotezeana muda kiasi hiki uchumi wa kati tutausikia tuu kwa wenzetu. Nimesikitika sana kwa kweli.
Weeeh yani huko kulivo na misitu bora mlale hapo hapo Sikonge msije enda kutolewa marinda bus zima.
 
Sio kwa mapori ya hiyo njia ambayo inatokeza Mbeya pia. Hawa polisi wenu wakimbiza vijana wa bodaboda hawana uwezo huo watabakwa live.
Hiyo ya kwenda Mbeya ukitoka Sikonge ni pori mpaka Kitunda, ukitoka Kitunda ni pori tena mpaka Rungwa, ukitoka Rungwa mpaka ufike Kampikatoto unakutana na pori tu tena lenye wanyama wa kutosha utakatiza usiku pori hilo??
 
Acha kuongea engese kwenye hoja serious aisee...
Unasema hivyo kwa sababu hujawahi kusafiri kwenye hizo njia.

Ungekuwa ulishawahi kutekwa hata siku moja barabara hizo usingesema hiki.

Hebu jiulize uko katikati ya hifadhi ya ugala halafu unaambiwa uchague kufa au kuliwa kisa una 50k tu mifukoni mwako kipi utachagua?
 
Buses Za Kwenda Kigoma, Mpanda, Kagera Hakuna Namna Lazima Mlegeze Mwili Hapo Mpaka Asubuhi Ndiyo Safari Iendelee
Ukitoka Dar Es Salaam ~Mpanda Mtalala Sikonge/Kaliua
Ukitoka Dar Es Salaam ~Kigoma Mtalala Hapo Hapo

Wasafiri Dar Es Salaam ~Kagera Nao Kahama/Ushirobo Kulala

Zamani 2007 Wanaokwenda Kigoma Walikuwa Wanapita Kahama Hapo Watu Tele Wanalala Kwenye Bus, Kubwa Zaidi Usalama Ni Mdogo Na Mapori Makubwa Sana
Ninja Akiwa Waziri Wa Mambo Ya Ndani Alisema Majambazi Yasitupangie Muda Wa Kusafiri

Watu Wasafiri Muda Wote Wanakotaka Ila Nakwambia Siyo Kagera, Kigoma, Mpanda
Mtalala Tu Njiani Mnapotoka Dar Es Salaam, Huko Noma Sana Unatembea Kilometres Tele Ni Mapori Tupu

Ukitekwa Hupati Msaada Mpaka Wachukue Vitu Vya Thamani
Serikali Vitendo Hakuna!!!
Sahihi ukitoka Sikonge mpaka Mlele ni hifadhi ya misitu then Mlele to Mpanda pia ni hifadhi ya misitu pande zote mbili ya barabara hakuna Vijiji hapo kati lakin Serikali Kwa nini isiweke kambi kadhaa za jkt au jeshi, TFS,magereza au polisi shida nini na pale masaa matatu tu upo Mpanda

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Nakubaliana na wewe huu utaratibu ni wa kukurupuka tuu na kusalimu amri kwa vibaka...Miaka ya 1980 Ma Bus njia za Dar to Mbeya, Dar to Arusha na kwingineko yalikuwa yanasafiri mpaka usiku, yaani saa 10 jioni unaenda Kisutu au pale Mnazi mmoja na alfajiri uko mkoani. Kumbuka kipindi hicho barabara zilikuwa mbaya sana na hakuna simu za mkononi kama sasa. Je tunaenda mbele au tunarudi nyuma kimaisha na kimaendeleo?
Nyongeza hapo....
Kulikuwa na mabasi ya saa 10 jioni (mengi ni ordinary abiria 65)

Saa mbili usiku(luxury)

Utaratibu huu ulikoma baada ya ajali ya busi la Yalabi Salama, Dar kwenda Dodoma. Kwa amri ya Waziri Mkuu wa kipindi hicho.

Hii ni nchi ya matamko na sio uhalisia!
 
Pori lile sio poa, tumewahi zuiwa hapo enzi hamna lami, tunaitafuta Inyonga tupo na Land Cruiser LX ,tumetoka Sikonge kwenye majukumu X, tuliona Mjuba anatoka porini na chuma mgongoni kuingia kama anachungulia aone nani anakuja nahisi walikuwa wanalia mingo ndiga za abiria, tupo mwendo wa mateka, suka akatu alert tuwe tayari huku akiwa anapunguza mwendo, vioo vilishushwa na sisi upande wetu Wakurungwa wakazikoki kuzielekeza nje tayari kwa lolote kivyovyote. Yule mjuba akatokomea tena porini kama mshale na kukawa kimya na sisi tukaenda kusimama mbele maana kulikuwa na TaTa ya abiria tuliiacha nyuma kuisubiri. Ikapita tukaisindikiza tukaiacha tukasepa zetu bila kumstua dereva wala kuleta taharuki.
 
[emoji848][emoji848]
 
Tuvumilie kwa sababu gani wakati mtu angefika Mpanda saa 6 usiku na kesho anaenda kazini au kwenye biashara zake?
Kama huko ni porini sana, basi ungewekwa utaratibu wa mabasi kuondoka saa 6 usiku ili yafike Mpanda walau 12 jioni.
 
Wadau tumetoka Dar na Bus la HAPPY NATION saa 12 asubuhi na tumefika hapa Sikonge, Tabora Bus limezuiwa kuendelea na safari eti mpaka saa 12 asubuhi, eti kwa sababu njiani kuna mapori makubwa.

Kwa maoni yangu hii si sawa kabisa, yaani pamoja na jitihada kubwa za serikali kukamilisha barabara hii na sasa ni lami kutoka Dar mpaka Mpanda, bado tunawapotezea muda watanzania kukaa hapa masaa 8 kisa hatuwezi kuimarisha usalama?

Hivi tutajikwamua vipi na umasikini ikiwa tunapoteza muda kiasi hiki? Halafu sehemu yenyewe hakuna hata stend yenye facilities za kuhudumia hata abiria wa Bus mbili. Kingine cha kushangaza kwenye maamuzi yetu ni kwamba hivi unawezaje kuacha bus ilale Tabora mjini kwenye huduma nyingi halafu uje kuzuia ma Bus Sikonge?

Kwa staili hii ya kupotezeana muda kiasi hiki uchumi wa kati tutausikia tuu kwa wenzetu. Nimesikitika sana kwa kweli.
kwanza kufasiri na basi huo ni umasikini bora kuchelewa kufuka ukafika salama kuliko kuwai mkafika mapolilini mkakutana na warundu wakawageza nyete wanawake kwa zamu mbona jamabi awafai
 
Dereva wenu ndie Mzembe. Angefika hapo kabla ya saa 3 usiku mngetoboa sasa Hapo Sikonge madereva wanapenda kulala kwa maksudi maaana wameoa Warabu koko wapo kibao so dereva anachelewa maksudi kufika ili akahudumie nyumba ndogo yake.

Siku nyingine Ongea na afande kiume uone ka hamjaruhusiwa.
Pumba
 
Siku hizi hata uwahi kabla ya saa tatu lazma ulale... Zamani ndio ilikua ukifika kabla ya saa tatu unaendelea
Hawa wanao lalamika wakitekwa au kupata hajari wakwanza kuilaume serikali heti mtu anasafiri na kitu kinacho jibuluza chini kama nyoke heti nae anataka kuwai mabasi mengi ya huko mpanda yana wabeba washamba wanaomlaumu dereva aipo endesha kwa kasi
 
Miaka 60 baada ya uhuru bado hatuwezi kudhibiti wahalifu kweli? Tutaobdokanaje kwenye umasikini kama tunapoteza masaa 8 hapa Kijijini Sikonge? Wenzetu wanafanya kazi 24 hours sisi tunachezea muda namna hii kweli? Kwa nini tusingelala Tabora mjini kwenye huduma nyingi?
kitendo cha kusafiri na basi tu ni umasikini tangu lini masikini akawa na haraka
 
Kuna kaukweli hapa maana hawa madereva wala hawajali, pia imeingia Majinja nayo imezuiwa. Swali langu ni kwa Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini hili jambo nyie hamlioni kwa jinsi abiria tunavyoteseka? Kwa nini bus zisilale Tabora mjini stend kuu ambako kuna lodges, vyakula na huduma mbalimbali badala ya kuruhusu tulale hapa Kijijini??
hoja yako inamashiko
 
Kwa hiyo miaka 60 bado hatuwezi kusafiri usiku kweli? Yaani vibaka wanatupangia maisha kweli? Ina maana hatuwezi hata kutumia JW TZ watusaidie kudhibiti hawa vibaka??
ukitaka kuwai panda ndege
 
Back
Top Bottom