Hivi kweli kuna biashara ya kuingiza faida kuanzia milioni 100 na kuendelea kwa siku/wiki/mwezi?

Sasa kama umetaja Hadi mtu kua anaweza sasa uongo wake upo wap. Kwan hyo silent nn cjui anapesa peke ake dunia mzma au
 
Hata mimi ilinishtua aisee,ukipiga hesabu ya haraka milioni 100 kwa siku,kwa mwezi ni faida ya bilioni 3,kwa mwaka ni bilioni 36 sasa mtu kama huyu si inabidi awe na kiwanda chake kwa nini aendelee kupanga fremu kariakoo na kufanya uchuuzi.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
huku arusha kuna wauzaji na suppliers wakubwa wa spare za magari, kupiga 100m kwa siku au siku kadhaa kwao kawaida mno....
Hao kweli wanapia kuna wale wahindi wa pale ungalimited nimewasahau jina wale kuna uwezekano kweli wanapiga maana wana stoo kubwa kila aina za spare hadi matairi ukitaka unapata.
Na hawategemei kuuza kwa mtu mmoja mmoja pia wanasambaza kwenye makampuni mbalimbali kwa jumla hapo ni rahisi kupata milioni 100.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Silent anaweza ingiza kupitia loose cargo ila hapati faida hiyo kwa siku.
Kwa wiki yawezekana kabisa.

Kina MO, Azam wanaingiza hiyo faida kwa siku
 
Kiukweli kwenye spare siwezi kukataa, mkuu nguo tena anakuambia KWA masaa tu M100 ina ukakasi sana
Kwenye spare ni rahisi maana injini moja tu inauzwa milioni 4 au 5,ila kwenye nguo suruali moja au shati zinauzwa elfu 20 sasa hadi uungeunge upate faida ya milioni 100 sio mchezo

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo humu hakuna aliyewahi fanya biashara kkoo
 
Umeenda mbali sana, kuna watu wanadanganywa.
 
Wewe unaamini story za jiwe?
 
Yeah, kuna jamaa yangu miaka ya 2010 alikua anauza hadi milioni 500 kwa siku tena wilayani,, ila haikua faida, bali mapato ghafi
Wilayani huko kama ni supplier mkubwa unazua vizuri hata bilioni ila unakuta faida ni ndogo ndogo sana 200-500
 
Mederin Bongo bado sana
Hapa wengi mules
 
Umeiweka kisomi mno hadi inakera
 
Kwa Abood inawezekana ila sio kwa siku, ni kampuni kubwa, hata makampuni kama Vodacom, ila sio maduka ya Kariakoo uingize wastani wa FAIDA ya milioni 100 kwa siku
Abood na mabasi yake haingizi hata ghafi ya milioni 100 kwa siku
 
Wameongelea KKOO
Faida

Hawajaongelea mauzo ghafi
 
Ndio zipo , Kariakoo watu wanaburuza hyo faida Kwa masaa, inatokana na bidhaa unaozouza , na mtaji ulio nao na coverage ya wateja , kama una coverage mpak nje ya nchi Mzee lazima ugonge tuu
Acha uongo wewe
 
Umeongea la maana sana, ni sawa na wafanyavyo Wachina Mataa wa Congo na Narungombe, wanakuuzia viatu kontena zima
 
Watu wengine hata reasoning kidogo tu hawana watu wamewekeza kwenye uchimbaji madini lakini hiyo mil100 anaingiza ndani ya mwez na sometimes inafeli na niuwekezaji mkubwa. Sasa kariakoo kunauwekezaji gani hapo wa kuingiza mil100
Kwenye madini unaweza ipata au ukaikosa yote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…