Hivi mpaka sasa kuna mtu hamwelewi Rais kweli?

Hivi mpaka sasa kuna mtu hamwelewi Rais kweli?

Chikenpox

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2022
Posts
784
Reaction score
1,246
Mimi naona huyu Mama kaletwa na Mungu kuwa Rais for a purpose.

Hebu angalia yafuatayo;

1. Ameondoa retention fee ya loans board kwa wanafunzi ambao tulikuwa tunasuffer kwelikweli. Kila mwaka mkopo ulikuwa unakua whether unafanya kazi au hifanyi. JPM hakufilia kabisa hilo japo inasemekana alikuwa Rais wa wanyonge, sijui wanyonge wepi!

2. Ameongeza pesa ya kujikimu kwa wanafunzi ambapo itakuwa elfu kumi kwa siku kitu ambacho JPM hakitaka kabisa, halafu alikuwa anajiita eti ni Rais wa wanyonge sijui wanyonge wepi hao!

3. Amefuta kabisa udhalilishaji wa kila namna kwa raia wake, mfano kuwepo kwa wasiojulikana kutesa na kuua. JPM hakufikilia kabisa kukomesha hili maana ndio ilikuwa nyenzo yake kuu ya kuwabana watu hususani mahasimu wake binafsi siyo wa nchi. Halafu eti alikuwa Rais wa wanyonge, sijui wanyonge wepi hao!

3. Limebaki suala moja tu nalo ni suala la muda na mtambuka tu ambalo ni ongezeko la bei ya vyakula ambapo I'm sure hata Mama linamuuma lakini kuna external factors nyingi sana ila litaisha tu.

4. Mwisho hongera Mama na Mungu akujalie uzidi kudumu katika hekima. Sasa hivi ajira bwerere. JPM alimaliza ajira zote eti miradi na ndege ambazo zipo zote ICU.
 
Hapo kwenye kuletwa na mungu ndo umenitoa tongotongo, kumbe miungu ndo huwa inahusika kuwaleta hawa wakubwa, acha mimi niendelee na huyu Mungu wangu mwenye enzi.
 
Rais Samia ni mpango wa Mungu. Hakika baada ya yule Shetani wa Chato ambaye alikuwa anatugawa kiitikadi na kikabila, akiua na kutudanganya, tumepata kiongozi mwenye upendo, mcha Mungu na anayeipenda nchi yetu kwa dhati. Tanzania Iko salama sana mikononi mwake.

Uongozi siyo maguvu, chuki na matusi Bali ni hekima, busara na upendo.

Wanaomchukia SSH ni waabudu mungu mtu wa Chato tuliyemfukia mwaka juzi mwezi Machi.
 
SSH ni mpango wa Mungu. Hakika baada ya yule Shetani wa Chato ambaye alikuwa anatugawa kiitikadi na kikabila, akiua na kutudanganya...
Mkuu hata ukimtoa huyo Magufuli bado matatizo makubwa ya hii nchi iliyo chini ya serikali ya ccm ni yaleyale tu kwa miaka yote hii, mpaka sasa washapita marais watano ni ajabu kuanza kupima rais bora kwa kuangalia mapungufu ya Magufuli, na wala Samia hakuwekwa hapo ili kulinganishwa na Magufuli na hasa ikiwa tunaona Magufuli alikuwa alikuwa rais wa hovyo basi kwa Rais Samia kulinganishwa na Magufuli ndio inafanya tunamuona ni Rais bora kutokana na anayelinganishwa naye. Kwamba Magufuli alizuia mikutano ya kisiasa ila Samia akaombwa akaruhusu basi inamfanya kuwa Rais bora na kila atakachofanya tunaona kafanya kwa kuwa ni rais bora, ila kama tukimlinganisha na marais wengine tofauti na Magufuli au marais wa nchi zengine pengine tungemuona ni rais wa kawaida tu.
 
Mimi naona huyu Mama kaletwa na Mungu kuwa Rais for a purpose.

Hebu angalia yafuatayo...
Nchi nzima imekuwa ni ya wanafunzi?

Maana ulichoongelea ni wanafunzi sjui kupewa mkopo sjui wale washibe,

Kinachokufurahisha ni kupewa mkopo na pesa ya kujikimu ukasahau mambo ya mhimu kama kivuko kukarabatiwa kwa pesa Karibu ya kununua kivuko kipya!

Umesahau kabisa uliowaacha nyumbani kwamba wanashindwa kula Milo miwili wanakula mlo mmoja nao washida!

Umesahau kabisa kuhusu umeme unavyotia hasara wafanya biashara!

Umesahau kabisa kwamba maji yanakatika jijini Dar hata wiki mbili hakuna maji
 
Yupo vizuri naona wameamua kukarabati kivuko cha kigamboni Kwa bilioni Saba wakati kilinunuliwa bilion 8.

Hongera Kwa kufurahia ongezeko la buku jero. Wakati vitu vimepanda bei maradufu.

Utaendelea kusifiasifia wanasiasa na utakufa maskini fala sana wewe
 
Back
Top Bottom