Na kawaida nchi kama USA na UK wanatoa Siri baada ya miaka mingi kupitia.Nyerere hakuwa kibaraka.
Bahati mbaya vijana wa sasa hawakuwahi kuishi miaka ya Nyerere.
Watanzania wakati huo tunasahau kuwa tulilipa kwa damu zetu katika kusimamia principles za Mwalimu, Principles ambazo zilikuwa safi sana na za uhakika na za ki utu.
Majirani zetu, hasa Kenya walitucheka sana kwa misimamo thabiti ya Mwalimu.
1965, Mwalimu alithubutu kuvunja uhusiano na Ujerumani Magharibi akiitetea Zanzibar ambayo ilikuwa ina ushirikiano na Ujerumani Mashariki nchi ya Kikomunisti.
Ujerumani Magharibi ilitoa ultimatum, Tanzania lazima ishirikiane na Magharibi tu, usipofanya hivyo Ujerumani Magharibi wanajiondoa.
Mwalimu akawaambia nendeni zenu, hamtuchagulii marafiki, Ujerumani Magharibi wakaondoka na kufunga ubalozi.
Tukumbuke kuwa Ujerumani Magharibi ilisitisha misaada yote hasa ya ujenzi wa nyumba za Hational Housing(NHC) nchi nzima.
Mwalimu vile vile alivunja uhusiano na Uingereza 1968, katika kuonyesha msimamo thabiti wa kumuondoa Ian Smith Southern Rhodesia(Zimbabwe) . Smith aliitwa haini kwa vile alijitangazia uhuru bila kuwashirikisha waafrikaUDI Unilalteral Declaration of Independence).
Na hapo ndiyo kina Mugabe wakaibuliwa, wapigania uhuru waliokuwa na makao Tanzania.
We paid the price.
Tarehe 25 October 1971, kwa harakati kubwa za Tanzania, hasa Balozi wetu Salim Ahmed Salim huko UN, China iliweza kuingia Umoja wa Mataifa, jambo lililokuwa likipingwa sana na Marekani.
Hiyo ndiyo misimamo ya kianaume ambayo Tanzania , chini ya Mwalumu Nyerere tulikuwa nayo.
Sasa hivi viongozi wa Afrika wananunulika kama njugu au vikaragosi.
SAD!