Hivi ni akili , uoga au upumbavu kuhusu UTT ?

Kule inatakiwa uweke pesa ndefu ambayo huoni pa kuipeleka..

Kupelekea vi milioni 2 vyako ulivyosave kwa mwaka is meaningless.
Kuweka maneno sawa, utt inatakiwa uweke pesa ya kustaafu, urithi au pesa za deal chafu serikalini.
Manake kiuhalisia kama mtu anaweza kutafuta hiyo pesa ndefu hawezi kuiweka utt,
 
Kabla ya mleta mada hujaandika hicho ungewaza haya, muda, nguvu, akili, usumbufu na hatari za kupoteza mtaji anazokumbana nazo muuza chips kabla ya kuvuna hiyo faida uliyoiandika.

Halafu ukitoka hapo, mlinganishe muuza chips anayewekeza laki saba kwa mwaka mzima ili kuvuna milioni 5 dhidi ya kijana anayeweza kubet laki moja na ndani ya masaa matatu anajikuta amevuna milioni 10. Ukiweza kuchanganua hicho kitendawili basi utakuwa umepata jibu.
 
Mtaani mtu anajenga banda la chips na mtaji kwa jumla ya laki 7 kwa mwaka ana make zaidi ya 5M .

Mwingine anaweka 20M UTT kwa mwaka ana make 2M

Hiki ni nini ? Mimi nadhani huko wanafaidika wanaoweka pesa nyingi
Tofauti ni malengo. UTT ni watu walio na fedha ambazo wanataka kuzihifadhi ili ziwe salama na huku zikileta faida kidogo. Pengine, ni watu walio na ishu nyingine ambao hawana muda wa kuzungusha fedha kwenye biashara nyingine. Hawa wa vibanda wa chips ni wale ambao wana muda wa kutosha kulinga lango.
 
hayo unasema mtazamo wako wewe. chips kuungua na moto plus muda wako na mahangaiko mengine? kuna watu wana mil 800-bil 1.5 na hana pa kuitumia. sasa na huyu afungue chips banda? si bora aweke utt huko. hiv unajua mo anachofanya au hawa madon wengine? yeye bwana anachofanya anaamka asubuh anachkua simu anaingia soko la hisa.duniaan huko anauza na kununua hisa anaamgalia exchange rate ya leo ngap? anauza dola zake hivo tu mpaka saa 5 asubuhi mwenzako kasha make over 100mil anakunywa chai anarudi kulala zake
 
Ukishindwa kutuwekea faida za UTT hututendei haki sisi darasa la pili D, mwaga elimu mpaka mwenye hoja ya kibanda cha chips akimbie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…