Hivi ni kweli hizi kodi ziko nchi hii au watu wanasema uongo kumchonganisha Samia na wafanya biashara? Huu ni zaidi ya msiba!

Hivi ni kweli hizi kodi ziko nchi hii au watu wanasema uongo kumchonganisha Samia na wafanya biashara? Huu ni zaidi ya msiba!

Unatakiwa ukiamua kufuga kuku, umuache atage mayai wazaliane ndio pengine uangalie uchinje kuku gani na uuze kuku gani ila baada ya kupata mavuno yake kwa wingi kadiri ilivyo wezekana

Sasa hawa TRA wanachofanya, wameanza kufuga kuku alfu kuku kabla hajaanza kutaga wameshaanza kumkwanyua mara mguu, mara kikwapa, sasa huyo kuku atataga vipi!!?

Wanajua namba ila hawajui mahesabu
 
Tanzania wafanyabiashara 95% ni wezi wanaoshirikiana na TRA kuiba na hawalipo kodi stahiki.
Anayebisha angalie makusanyo ya Taifa kwa kila mwezi wafanyakazi wa umma na private ambao ni asilimia ndogo sana katika Nchi wanalipa Kodi mara 2 kuliko Wafanyabishara wote Nchi nzima.
Uwepo wa kodi zisizo na umuhimu unasababisha rushwa ambayo inapelekea kodi kutokulipwa.Lakini kama zingekwepo kodi chache bas zingelipwa zote kwa usahihi na kupelekea mapato upande wa wafanyabiashara yakue
 
Mh Rais ni kweli umeamua kuuwa uchumi na biashara kabisa? Hivi kweli umeruhusu kadi za namna hii?
Hii nimeikopi kwa mwana jf wakukurupuka1
Nanukuuu
“Leo Kuna mgomo kwa wafanya biashara soko kuu kkoo kutokana na kila wiki uzinduzi wa kodi mpya

Baadhi ya kodi unazotakiwa kulipa

1: TRA.
2: FIRE.
3: JIJI.
4: USAFI.
5: Kodi ya store.
6: Makato 10% kweny commission (watu wa mihamala)
7: Kodi yakupeleka lori kkoo kubeba au kushusha mizigo”
Mwisho wa kunukuu

Hivi kweli mtu awe na store ya kuhfadhi mzigo wake halafu anatakiwa kulipa kodi? Na akitoa huo mzigo kwenda dukani akiupakia atatakiwa kulipa kodi na akifika dukani kwake atatakiwa kulipa kodi ya kushusha mzigo halafu akianza kuuza atatakiwa kulipa kodi tena hivi hii ni kweli au TRA wanasingiziwa?

Hivi kodi zipo kwa mtu mmoja au wafanyabiashara wanachangia kwa pamoja? Hivi kweli kuna mfanya biashara ataweza kudumu bila kutoa rushwa? Kuna mfanyabiashara atadumu bila kufanya magendo? Mbona kodi ni nyingi sana kwa mtu mmoja? Hii ni zaidi ya double taxation!

Hivi hizi kodi kweli zipo zote au TRA na serikali wanasingiziwa?

Kwanini Rais usimamii maneno yako?’hizi kodi zote hasa hiyo ya store na kushusha mzigo sio uporaji na unyang’anyi kabisa? Msaada wako uko wapi? Kwanini unayaacha haya au sio kweli?
Basata
TRA
Bonde la Maji
uchafu
fire
Acheni kabisa.
 
Kuna shida mfumo wa kodi...kwa kuwa serikali inataka pesa. Kila ubunifu wa kodi unatungwa. Mpaka zinajirudia ki aina.
Tukipunguza matumizi ya serikali angalau makusanyo yatakidhi kwa asilimia fulani.
Kuliko kila siku kubuni kodi kukidhi matumizi mukubwa ya serikali ya mashariki ya mbali..
Tuna matumizi yasiyo na sababu
 
Hivi kodi zipo kwa mtu mmoja au wafanyabiashara wanachangia kwa pamoja? Hivi kweli kuna mfanya biashara ataweza kudumu bila kutoa rushwa? Kuna mfanyabiashara atadumu bila kufanya magendo? Mbona kodi ni nyingi sana kwa mtu mmoja? Hii ni zaidi ya double taxation!
Kuna uzi humu ulimtaja mwanaye Rais kuwa ni mkepa kodi na anawasumbua TRA hapohapo Kariakoo, sijui hilo sakata liliishia wapi
 
Zipo zaidi ya hizo na hapo sio swala la mama ,zimekuwepo miaka na mikaka ila Sasa wamepata upenyo wa kusemea Kwa sababu Mama amewapa uhuru..

Nadhani unajua kwamba Sukima gang wanasema Hilo la wafanyabiashara Mwendazake angelimaliza Kwa sekunde na mnajua msako na Biti ambalo lingewakuta hao wanaojiita viongozi wa mgomo..
Ukisikiliza wafanyabiasharaa wanasema bora huko nyuma kwa maafisa TRa walikuwa wanaogopa kudai rushwa .kwa sasa wanalazimisha na wanakufuata hadi myumbani kama alivyosema yule mama kibonge .usikaze fuvu lako bwashee
 
Wewe ni mpuuzi tu, wakati wa Magufuli wafanyabiashara walialikwa mpaka ikuru kutoa dukuduku zao mpaka kamishina wa tra alipoteza kazi baada ya mfanyabiashara mmoja kutoka kkoo kulalamikia maofisa wa tra kumsumbua pamoja na kuwa na risiti zote za malipo baada ya kakataa kutoa rushwa,tra wakati huo Magufuli aliamuru huyo mfanyabiashara kulipwa fidia ya mali yake,mkuu wa tra alipoteza kazi siku hiyo, Magufuli akucheka na kima kama mrembo wenu mnayempamba.
 
Wanasema mbele ya PM kwamba kwa sasa mazingira ya kufanya biashara hapo Kariakoo ni tete kuliko wakati mwingine.

Licha ya Rais kusema hataki kodi za dhulma,hivi sasa ndiyo zimepamba moto TRA wanawafuata hadi nyumbani ku-negotiate rushwa.
Ww ndo umeelewa kwa sasa ,yaani ni kama vile wanalazimisha rushwa
 
Wewe ni mpuuzi tu, wakati wa Magufuli wafanyabiashara walialikwa mpaka ikuru kutoa dukuduku zao mpaka kamishina wa tra alipoteza kazi baada ya mfanyabiashara mmoja kutoka kkoo kulalamikia maofisa wa tra kumsumbua pamoja na kuwa na risiti zote za malipo baada ya kakataa kutoa rushwa,tra wakati huo Magufuli aliamuru huyo mfanyabiashara kulipwa fidia ya mali yake,mkuu wa tra alipoteza kazi siku hiyo, Magufuli akucheka na kima kama mrembo wenu mnayempamba.
Leta crip acha upumbavu wako.

Waliokuwa wamekimbia Kariakoo walikuwa kina nani? Miduka Mingi ilibakia wazi na bei ya fremu kuporomola harafu unaongea upuuzi hapa..

Sasa hivi wafanyabiashara wanachekewa ndio maana wanafanya mzaha,wanapata hela z Bure ndio maana wanavunja magorofa ya zamani na kujenga upya,Kwa nini hawakufanya kipindi Cha Mwendazake?
 
Ukisikiliza wafanyabiasharaa wanasema bora huko nyuma kwa maafisa TRa walikuwa wanaogopa kudai rushwa .kwa sasa wanalazimisha na wanakufuata hadi myumbani kama alivyosema yule mama kibonge .usikaze fuvu lako bwashee
Unalazimishwaje kutoa Rushwa na wewe ukatoa? Hapo utakuwa una makosa ndio maana unatoa Rushwa,huna makosa unatoa Rushwa ya kazi gani?
 
"Siku moja mtanikumbuka, najua mtanikumbuka kwa mazuri si kwa mabaya, kwa sababu nime 'SACRIFICE' MAISHA YANGU kwa ajili ya Watanzania maskini" ~

Hayati. John Magufuli

Hizo kodi zimeanza kwa raisi Samia eti?
 
Back
Top Bottom