Hivi ni mimi ninayekula chakula kwa Speed au nyie Wenzangu mnawezaje kutumia nusu saa kwenye kula tu?

Wakati nakua ndugu zangu home walikuwa wananitania kuwa nina friji mdomoni, chai ya moto sijui nini napiga fasta bila makeke😅😅. Sipendi kabisa kupoteza muda kwenye kula, breakfast yangu huwa nakula huku naendesha gari to ofisini, naona kukaa na kula ndio niondoke ni kupoteza muda. Au nimefika ofisini alafu mara kidogo sijui ndio niende kula breakfast ni kuharibu consistence ya mambo yangu.

Kuna siku Trafic kanisimamisha asubuhi, nafungua kioo anaona niko kwenye mchakato wa kuichakaza huku naendesha, alivyoona akaniambia mzee naona una haraka hata chai unanywea kwenye gari? Nikamwambia ndio afande I’m really late aisee……..akaniambia kimbia kajenge taifa kaka…….nikasepa huku natafuta mihogo yangu😂😂😂
 
🤣🤣🤣🤣 Unatisha sana, hamna kupoteza muda Et kwenye kula tu
 
Kuna maslay Queen hao,ukiwaalika wanaagiza misosi ya gharama,halafu hawaimalizi yote, wanakula kidogo wanaacha.

Sasa wakiwa wanatumia vijiko,kukitoa kijiko kwenye sahani mpaka mdomoni na kukirudisha tena kwenye sahani anatumia dk 3.
Na anabakisha
 
Kumbe tupo wengi!! Kuna muda nilianza kujilazimisha kula taratibu nikashindwa.

Nina mpenz wangu saivi ndo kanizoea mara ya kwanza alikua hanielewi hii tabia. mimi nikienda ugenini napata shida sana maana kula taratibu au kula huku mnapiga story siwezi. Kwahyo mimi kula ugenini nakwepa sana

Mimi natafuna chakula mara 3 au 2 tu na kumeza, niliendaga sehemu kutibiwa kienyeji nilikua naumwa nilipata shida sana kwenye chakula pale, jamaa wanakula taratibu balaa, yaani Tonge moja ugali au wali linabembelezwa dakika.

Mimi hata kama sina haraka yaani labda nakula alafu nikimalize nilale lkn nakula fasta fasta yaani nilishashindwa kula taratibu
 
Mimi naweza kula Nimesimama yaan ilimradi tu nikimbizane na kitu fulani.
Mimi ni multitask yaan naweza nikala huku nafanya shughuli zingine 3/4 ingawa kiafya haishauriwi na sipendi kula kitu kimoja yaan napenda kula vitu vingi kwa wakati mmoja ambayo pia kiafya haishauri yaan sio vizuri kuchanganya carbohydrates na proteins at the same time namaanisha sio unakula wali na ndizi au ugali na ndizi ugali/wali utawahi kumeng'enywa Ila ndizi itachelewa na itabaki juu kwa hio urahisi kuvimbilwa kwa muda fulani,

All in all ili niwe nimeshiba basi ni lazima Nile chakula at least plates 2 au sinia moja zima hapo ndio najihisi kushiba apart from that najihisi njaa mda wote, hua napenda kushiba haswa jambo ambalo pia kiafya halishauriwi, kiufupi sipendi njaa yaan nachukia kukaa kaa na njaa au kula kula ovyo ovyo nipo tayari nile mlo mmoja nishibe full sio natoka kidogo nimeona mhindi ninunue sijui nmeona mshkaki nmetamani aah hio hua siipendi nikila nakula haswa, ingawa kiafya unashauriwa ule kiasi tu usishibe kupitiliza maana chakula kingine kinakua hakifanyiwi kazi pia mwili huchukua mda sana kumeng'enywa chakula km haufanyi kazi ngumu hivyo itajuchukua mda kupata Choo

Nitakuja kuendelea sijamaliza..
 
🤣🤣🤣🤣Et tonge linabembelezwaa
 
Wewe kama mm nakula kwa kasi ya 4g kuna muda hadi huwa nashtuka kimeisha bila hata kujua.
Ilakiafya ni mbaya na inachangia kuwa bonge kama usipotafuna chakula vizuri.
 
Mkuuu haya masuala ya Afya saa ingine hata kuyatekeleza ni kazi ,

Sasa unikute nawapa ushauri watu wa Ulaji 🤣🤣
 
Je unakula kias gani labda kama ni wali je nusu unamaliza Mkuu ? Maana Kuna wengine hawependi kula Sana na wapo speed anakula Vijiko vitatu.
 
Kumbe umeoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…