🤣🤣🤣 Kuna kicafe fulan, nilikua Kila siku napita kunywa Maziwa fresh yamoto , basi Mimi kitu Cha kunywa hata kiwe chamoto, nakunywa chap ,utadhan Nina ka freezer mdomoni.
Wahudumu wa pale walikua wananishangaaga sana.
Nikaona isiwe nongwa ,nikacha kwenda hapo.
Toka nianze ishi na Baby Mama wangu, aahhh Kila siku jion, lazima nikute chupa ya uji wa lishe, naipigaaaaaa kama nakunywa maji 🤣
Nashindwa kujua tabia ya kula haraka haraka niliitoa wapi
Nimekulia kijijin na familia yangu,kama unavyojua kijijin huwa kuna vyakula vingi pia tulikuwa wafugaji
Nakumbuka tukiwa kijijin nilkuwa nakunywa chai ya maziwa vikombe kuanzia vinne mpaka sita tena haraka haraka na ikiwa ya moto,yaan wakati wengine wanahangaika kupoza mimi nakuwa nabugia tu
Kila siku ilikuwa inanitoka ngozi ya juu mdomoni tena linatoka likipande likubwa tu lakin sikomi kila siku ni hvyo hvyo tena kwa spidi ya ajabu
Chai(chakula cha asubuhi ndo chakula ambacho huwa nakipendelea zaidi)
Nakumbuka tulivyoamia mjini nilipata shida sana maana mama alianza kupika chakula kidogo,yaan nilkuwa napata shida mlo wa chai kutumia kikombe kimoja tu,mwanzo nilkuwa najikuta sjamaliza vitafunwa lakin chai tayar inakuwa imeshaisha kwenye kikombe,ila siku hz nimeweza kubalance nakunywa kikombe kimoja cha chai kwa mlo wa asubuh
Niliwah kwenda kuishi arusha kutokana na hz haraka zangu za kunywa chai nilikuwa naungua sana mdomo kuanzia lips,ulimi na ngozi ya juu ndani ya mdomo,yaan mpaka kula chakula cha mchana nilkuwa napata shida sana,yaan kutokana na lile baridi nikawa sihis ule umoto wa chai
Nakumbuka kipindi naanza kuishi na mwanamke kila siku nilkuwa nampiga ko za hatari,nilkuwa najikuta najisahau nakula haraka kuja kushituka unakuta kimebak kiugali kidogo,siku zingine nilkuwa namwambia uwe unanishtua maana utakuwa unashinda njaa kila siku
Au zile za kutoka out eti tushee sahani moja mademu huwa nawapiga ko za hatari hadi naona aibu,kidogo siku hz huwa nakumbuka naanza kupunguza speed
Baada ya kuwa mtu mzima speed ya kula haraka ilibaki pale pale ingawaje siri chakula kingi sana,sasa shida huwa inakuja nikiwa na mgeni na jinsi tulivyofundishwa inatakiwa wewe mwenyeji uwe wa mwsho kushiba,sasa huwa napiga haraka haraka najikuta nimeshiba haraka na wakat huo mgeni bado anaendelea sasa inakuwa noma inabid nipunguze speed au niache kula tu
Ugenini hadi wenyeji huwa wanahis mgeni hajakipenda chakula au kama ni ile style ya kila mtu sahani yake wanaomba waniongeze nawambia hapana nimeshiba kabisa