Jamii zetu hizi za kibongo wanawake wakisema hawataki wanaume wafupi kama stuli au vibamia kwa uwazi kabisa itakuwa shida.
Kiujumla jamii ya Kitanzania, watu wengi kama mtoa mada at least, hawaheshimu uhuru wa mtu binafsi kujiamulia anachotaka.
Ni watu wanaopenda sana kujichomeka katika mambo ya watu wengine bila kualikwa.
Wanapenda sana mambo ya kupangiana pangiana maisha, na gia kubwa inayotumika katika ajenda hii ya kupangiana maisha ni kujali. Lakini kiukweli si kujali, ni kutaka control.
Wanapenda sana kutoa ushauri ambao hawajaombwa, kwa watu wasiowajua, kwenye mambo wasiyoyafahamu vizuri.
Mara nyingi hii inakuja kwa sababu ya kutaka kuwa control watu wengine, kutaka wao waishi kama unavyotaka wewe, bila hata kuwajua.
Ni ishara ya mtu kushindwa kujiongoza katika maisha yake, anakuwa yuko busy kuchunguza maisha ya watu wengine na kuwapangia mambo.
Ni ishara ya kutoijua dunia. Chances are, mtu anayesema mambo haya mara nyingi anakuwa hajakaa katika jamii zilizo tofauti na za Tanzania. Hajapata nafasi ya kuishi, kwa mfano, Marekani au Ulaya, kuona mambo tofauti na ujima tuliozoea Tanzania. Ingawa pia kuna Watanzania wengi wanaoishi huko nje lakini bado wana mawazo ya kijinga ya kulangiana maisha kwa sababu ile miaka yao formative, ya awali, waliyoishi Tanzania imewaharibu mpaka kukaa nje hakuja wasaidia.
Halafu pia kuna Watanzania wengine smart sana hata bila kukaa nje wanakuwa washayaelewa haya mambo, ingawa hawa nafikiri si wengi.
Na mara nyingine watu wanajikuta wako so deep katika utamaduni huo wa kutaka kuwa control wenzao, wanakuwa hata wao wenyewe hawajui kuwa wanachofanya ni kutaka kuwa control wengine.
Yani inakuwa kama wanataka kuwa control wengine by reflex action, by systemic defaults, kama wanapiga chafya tu, bila kuamua.
Wengine wako frustrated na maisha tu, na katika kutafuta mnyonge wao wa kumtolea frustrations zao, ku lash out, mnyonge wao ni mwanamke.
Yani katika mawazo yao, mwanamme hata ukiwa lofa vipi, lakini angalau unakuwa umeshinda bahati nasibu ya kuzaliwa mwanamme, hujazaliwa mwanamke, kiumbe dhalili kabisa, kwa hiyo, hata kama huna pesa, huna mali, huna akili, unaweza kutamba na huo uanaume wako tu.
So, wengine hawajui haya mambo na hawajui hata kama hawajui. Wanafanya mysoginy kimazingira tu kwa sababu washamba, hawaijui dunia. Na pengine wanajiona wanafanya kwa nia nzuri kuwasaidia wanawake.
Lakini kiukweli wengine ni kama samaki waliozaliwa katika maji, wameyazoea maji mpaka hawayaoni tena. Na hawa wanakuwa wamezoea mysoginy mpaka hawaijui tena wanaona ni kawaida tu.
Kwa sababu mifumo, tamaduni, elimu, mazoea, vyote vimesha normalize sana hizi habari za kupangiana maisha.
Kuanzia ujima, ujamaa, ukoloni, na mpaka huu uhuru feki, Mtanzania wa kawaida anachojua ni kupangiwa maisha tu.
Hakuna uhuru wa fikra na kupeana nafasi watu waishi wanavyotaka wao, si unavyotaka wewe kwa kukariri unachokijua wewe.
Na wazazi, na viongozi wa dini, na walimu, na watawala. Kote tunanyukwa na kupangiwa tu, hakuna dialogue kusijia watu wanataka nini wao wenyewe. Unapangiwa tu.
Hata chuo kikuu, sehemu ambayo panatakiwa kuchemsha akili na kubishana, kwa kiasi kikubwa imekuwa ni sehemu ya profesa ku lecture na wanafunzi kusikiliza tu. Mwanafunzi akipinga vigorously anachukuliwa kama mtovu wa nidhamu, anamkosea heshima profesa.
Tumeshazoeshwa utamaduni wa kupangiana maisha mtu mwanamme haoni haya kuanzisha uzi wa kuwapangia wanawake waolewe vipi.
Unawapangia wanawake habari za kuolewa kwani wewe kungwi?