Hivi ni sawa kuzaa watoto kwa matarajio ya watakuja kukusaidia baadaye?

Kaka asante kwa maoni yako mazuri

Ila maana yangu ni kwamba kama mzazi unajiona huna uwezo wa kutosha hakuna haja au ulazima wa kuzaa watoto wengi ambao unaona kabisa kuwahudumia ni kazi

Na mbaya zaidi unawazaa wengi ukiwa na matumaini watakusaidia baadae

Unakuta unazaa kwa matumaini ya kusaidiwa huku watoto wenyewe huwatengenezei mazingira mazuri

Wanapambana wanapata chochote kitu unaanza tena kulalamika kua husaidiwi na pengine unasaidiwa ila unataka zaidi

Hiyo sio sawa kabisa
 
Mm nafikiri kwa mwanaume kuwa na watoto wengi tena ikiwezekana kwa wanawake tofauti tofauti ina faida kubwa kuliko kuwa na watoto wachache kwa mwanamke mmoja. Kikubwa cha kuzingatia ni kuhakikisha unazaa na wanawake wanaojielewa ambao ukiwapa support mfano biashara wanaweza kujisimamia na kukuza biashara, au wanawake wenye kazi nzuri inayoweza kumpatia mtoto malezi mazuri.....
Ukipata Mama bora wa watoto wako ukampa support kwenye kazi au biashara basi unakua na future nzuri ya baadae.
 
Ooh sawa sawa kaka Asantee kwa maoni karibu tena
 
Achs uvivu saidia wazee
 
Kama unaweza kuhonga na kusaidia watubaki kwanini usisaidie mzazi/ wazazi wako? Saidia kama hisani kwa hiyari toka moyoni kiasi ambacho hata wewe mtoa msaada unatoa huku umefrahi na sio unatoa kwa manung'uniko moyoni. Anyways nachepuka kidogo nje ya mada,..wakati tunawaza kuhusu issue ya msaada kwa mzazi/ wazazi tunatakiwa kujua kua na sisi siku moja tutakua wazazi ama ni wazazi tayari na kuna siku tutazeeka, je tumejiandaaje kutokuja kua tegemezi kwa watoto wetu, familia zetu na jamii zetu kwa ujumla. Kuna mdau hapo juu kaongelea mambo ya bond, mahusiano na nature ya familia yenu ilivyo kitu ambacho ni muhimu sana kukifanyia kazi. Mahusiano na mzazi/ wazazi toka ukiwa mdogo adi anakusomesha unapata kazi inategemea bond yenu ikoje. Kama mzazi alifanya hilo kama jukumu lake hata kama hakua na uwezo mkubwa but kapambana adi umefika hapo.,sioni kama anaweza kukupa pressure ya kukudai fadhila alizokufanyia, sielewi itafikaje kwenye hiyo level lazima tu hayo mazingira ya kuvutana vutana na kushindana yalianza toka enzi hizo na hapakua na clear line of good terms kati yenu toka utotoni kwako. On the flip side, mzazi ashazeeka hata kama hujafanikiwa kiivyo but unaona kuna sehemu anakwama labda makazi sio mazuri, chakula changamoto, afya na mengineyo hapo huhitaji hata kuambiwa na mtu Mzee lazima tu itakugusa toka moyoni. Mzazi wako anapata shida asaidiwe na nani sasa kama sio wewe kwanza? Shida ipo kwa wale ambao wanatengeneza mazingira ya kusaidiwa as if anakudai madeni ulipe alivyokusaidia adi ukafika hapo. Let say mtu ni mstaafu, ana pension kila mwezi anapata chochote, ana mahala la kuishi, ila tu anataka kuishi kifahari kwakua tu alikusomesha hiyo hapana siungi mkono, kama atakua na busara atapambana kwanza ujijenge usimame vizuri, wewe mwenyewe tu utaona ni wapi unatakiwa kufanya kitu home kwa mzazi
 
Watu wanapuuza ulichokiandika hapa, ila majibu ya mada yote yako hapa. Background ya mahusiano na mzazi wako ndo itaamua tafsiri ya msaada kama ni hiyari ama lazima. Mzazi ambae anakupenda hawezi kukulazimisha umlipe fadhila. Lakini na wewe huwezi kua na kichwa kama cha kuku, mzazi wako anapata shida na una uwezo wa kumsaidia hufanyi ivyo unataka asaidiwe na nani?
 
Ushauri kama huo ilitakiwa kumpa mkiwa peke yenu aisee, ni jambo personal sana
 
Sasa kama nimemsomesha,nimemlea vizuri na kumwandalia maisha mazuri kwa nini asinisaidie pale ambapo mimi nimekosa nguvu(nimezeeka)?Unataka anitelekeze wakati yeye nilimpa kila kitu?
Ila hajakuomba umlete duniani, ni shobo zako tu, hivyo kumlea una wajibu lakini yeye kukulea ni hiyari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…