Hivi ni sawa kuzaa watoto kwa matarajio ya watakuja kukusaidia baadaye?

Kupitia huu uzi najifundisha kuona watu wanatokea kwenye familia za aina gani?
Utamtambua mtu kwa emotion yake tu kwenye uchangiaji wake,wengine wanajibu kwa hasira kama zote dhidi ya wazazi wao!

Ndio mkuu, huu ni uzi "chokonozi".. 😊
Mtu anachangia kulingana na nini amepitia au anapitia na wazazi wake!
Ngoja tupate vitu kutoka kwa wadau.
 
Wewe sio mgeni kwangu hujawahi kabisa kukubali mawazo yangu mara nyingi ni kuzodoa 🀣

na hilo sio kosa kabisa so nitakuzoea hivyo hivyoπŸ™πŸ™ karibu tena
 
Kilimanjaro sio kweli, katika jamii hawazaliani kwa sasa ni Kilimanjaro, shule nzima ya msingi kukuta ina watoto 50 tu ni kawaida
Wilaya ya Moshi vijijini kata ya Kishimundu siwezi kutaja kijiji, nimemkuta mzee wa miaka 80, mwanajeshi mstaafu ana idadi hiyo ya watoto.
Mi mwenyewe nilishangaa.
Na mmoja wa watoto wake ni mtu wangu wa karibu.
 
Kupitia huu uzi najifundisha kuona watu wanatokea kwenye familia za aina gani?
Utamtambua mtu kwa emotion yake tu kwenye uchangiaji wake,wengine wanajibu kwa hasira kama zote dhidi ya wazazi wao!
Sio poa
Wenye hasira nawaelewa sababu mimi ni muhanga wa hili swala, ukizingatia nimelelewa kwenye familia mbili tofauti upande wa mzee na wa mama, kila moja anavutia upande wake
Na upande uliosema kwamba siwajali sababu najali upande mwingine ndio upande ambao nimeshatoa zaidi japo wao wanaona ni kidogo hadi kusema sitoi
 
Waiaya ya Moshi vijijini kata ya Kishimundu siwezi kutaja kijiji, nimemkuta mzee wa miaka 80, mwanajeshi mstaafu ana idadi hiyo ya watoto.
Mi mwenyewe nilishangaa.
Na mmoja wa watoto wake ni mtu wangu wa karibu.
Wazee wa zamani ni sawa na karibu wote walimudi kuwatunza kupitia zao la kahawa ,ila kwa sasa kukuta binti wa kichaga mwenye miaka 30 na hana mpango wa kuzaa ni kawaida
 
Wazee wa zamani ni sawa na karibu wote walimudi kuwatunza kupitia zao la kahawa ,ila kwa sasa kukuta binti wa kichaga mwenye miaka 30 na hana mpango wa kuzaa ni kawaida

Anachanganya vizazi, wazee wetu sio sawa na millennials au Gen-Z. Life ya uchaggani imeshabadirika, na imebadirika miaka ya 90's kuja juu huku. Watoto kibao sio tena priority uchaggani.
 
Yeah na mi nitakua mama nisie na gubu la kusaidiwa
Mtazamo mzuri sana huu, ukiwalea watoto kwa upendo bila kuwabebesha mzigo wowote, nafasi ya wao kuja kukusaidia kwa hiari huwa ni kubwa zaidi.
 
Wewe sio mgeni kwangu hujawahi kabisa kukubari mawazo yangu
Umetoa kwangu mawazo au shutuma? hujatoa wazo lolote kwangu,labda utakua hujui maana ya neno Mawazo ''Suggestion''
na hilo sio kosa kabisa

Kosa gani?
so nitakuzoea hivyo hivyo
Wala sijawahi kuhitaji mtu anizowee hapa JF
πŸ™πŸ™ karibu tena
Kuwepo kwangu JF wala hakuhitaji ukaribisho kutoka kwa mtu yeyote yule bali ni maamuzi yangu binafsi.
 
Kumekucha haya endelea mkuu mie pamoja na kua mwanamke siwezi majibishano so kama nimekukosea nisamehe mimi bureπŸ™πŸ™πŸ™πŸ™
 
Kumekucha haya endelea mkuu mie pamoja na kua mwanamke siwezi majibisha so kama nimekukosea nisamehe mimi bureπŸ™πŸ™πŸ™πŸ™
Kwani nani anabishana? mimi sibishani bali najadili mada,
Mimi ninapojadili jambo hapa JF hua naangalia zaidi kinacho ongelewa na sio kuangalia ID gani inaongea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…