Hivi shule kama hii ina walimu kabisa watakaoweza kuidai Serikali iwaongezee mshahara bila aibu?

Bora umesema kaka
 
Tatizo katiba
Hao wote walitakiwa kusoma ufundi sio secondary.,..
 
Ndugu zangu, kada ya UALIMU siyo kama kada nyingine unazoweza kuzifanyia masihara. Ikumbukwe kuwa ili watoto wafaulu vizuri mambo mengi yanahitajika ili kufanikisha lengo kuu la shule ambalo ni utoaji wa Elimu Bora..
Mambo hayo ni:
Miundombinu Bora ya kufundisha na kujifunzia * Uwajibikaji wa walimu na umahiri wao katika mchakato wa kufundisha * ushiriki wa wazazi katika kufanikisha mchakato wa uboreshaji wa mazingira na Taaluma. * Nidhamu ya wanafunzi(self discipline) * Motisha kwa waliofanya vizuri (wanafunzi na walimu) Uongozi Bora wa shule (transparency, accountability,etc.
Kwa kuwa shule nyingi zipo chini ya mamlaka za halmashauri na miji au wilaya basi majukumu hayo yanamuhusu kila mmoja katika mamlaka hayo na WA mwisho ni mwalimu mkuu/mkuu wa shule.
Hivyo kuwananga walimu hao siyo uungwana japo nadhani wanaohusika Moja kwa moja kama watumishi..
Matokeo haya yanahitaji kufanyiwa research na kujua ni factors zipi zimechangia kufikia hatua hii..
Mwisho ila si kwa umuhimu wazazi lazima tufikirie kuchangishana kwa hali na mali, tuwajengee watoto wetu mabweni , au tununue mabasi ya kuwapeleka watoto shuleni , tusijifanye manunda wa kutumia mzigo bara na bebes wakati watoto wetu Wanaendelea kupata four na zero ..
Generally ni kuwa tutaendelea kuwa wapiga kura kila wakati kwa wenzetu wanaosoma shule za div 1. ...
Nawasilisha kwa unyenyekevu@ mzee wenu kutoka Kijiji Pomerin Dabaga Iringa Tanzania
 
Aisee
 
Acha kabisaa Yaani sifundushi waelewe nafundisha Ili nimalize syllabus na uzuri wa hesabu no ya wateule baasii only class A Ndo nakomaa kungine nahakikisha natoa notisi tu,Yaani nikianza kusahihisha Sasa[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]jus imagine Kwa siku nna madarasa manne na yote Yana 80 +watoto na maths kusahihisha lazima Yaani Mimi sikai ofisini nakaa Nje ,ila huwezi amini hakuna Mwaka form two hatutoi A na form four...
Kuna dogo alihama kwetu akaenda mburahati hapo,Yaani hiyo shule watoto wa manzese,kigogo,mburahati yenyewe,wahuniii,wavuta bangi hapo amakuambia Yaani hapo full utawala maana Wana tabia ya kuzingua walimu hapo shuleni Ndo maana walimu hawawafatilii hapo waweza pigwa na wanafunzi kirahisi tu hapo
 
Ila lengo kuu la Shule za kata ni kupunguza ndoa za utoto na child Labour at least wamefanikiwa na Wala siyo watoto wafaulu,serikali imefanikiwa Sana kupunguza early pregnancies na early marriage Sana tu maana zamani hata huko vijijini mtoto wa miaka 12 anaolewa Sasa hivi walau Mpk amalize la 12 ana 18yrs akiolewa sio ishu Sana au akizaa
 
Nakuelewa pole mnoo..ila una wito hongera sana..hata kuchagua tuu wanafunzi wanaokuelewa na kudeal nao ni jambo zuri unaona A zilikuwepo..hyo shule hapo walimu waliwasusaa wakaendelea na mishe zao na wanafunzi wakajiachiaaa
 
Mwalimu hata akiwa 'mweupe' kiasi gani, kama kuna mwanafunzi ana akili na akipata material sahihi, anapasua paper...

Chanzo namba moja cha mwanafunzi kufeli huwa ni yeye mwanafunzi na mazingira yaliyomzunguka...
Nakubaliana na wee mzee.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaaa
 
Hizo shule ulizotajaa wanaenda wanafunzi Cream tyuuh, afu sasa wanafundishwa kujitegemea wao wenyewe ktk masomo yao. Walimu wa kule hawapati tabu hata
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ila n kweli.
 
Shule nyingi walimu wa Math huwa wana wateule wao wa kwenda nao. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Swala la watoto kufaulu linahitaji nidhamu ya malezi,Sasa wenye watoto waliwaachia walimu walitegemea Nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…