Hivi siku hizi hakuna majambazi?

Ww lazma hukai kanda ya ziwa usinge andika bandiko hili...
 
Si 2014? Au ile ilikuwa awamu ya pili?
 
Mkuu
Usiwastue wakaanza kuzingua. Hawanaga akili hao
 
Mdomo koma kazi yako kula
 
Kuna wale walikuwa wahaishi mapangoni kule mwanza, siku wanapelekewa moto ilikuwa ni zaidi ya vita. Zilirindima risasi z kutosha hadi wakawa neutralized.
Kuna tukio moja ni Mungu tu alituvusha, kipindi hicho niko chalii mdogo nikiwa na wenzangu pamoja na mbwa tukaingia kwenye hayo mapango kwenda kuwinda.

Ebwana weee si tukakutana na wajomba wametulizana wanapiga vitu vyao. Na vile mbwa hawana siri wakaanza fujo za kubweka ovyo, ajabu wale wajomba walibaki na utulivu wao na kutuelekeza cha kufanya kwa urafiki kabisa. Niliwachukulia tu ni ma bro wanapiga mjani.

Baada ya miaka kupita nikapata habari kumbe ile ilikuwa ni kituo cha wazee wenyewe.
 
No. siwezi kuwa jambazi, Mungu anakataza.

ushwari huwa hausababishwi na uwepo na uimara wa mabunduki na askari (Jeshi). ushwari unaletwa na Mungu mwenyewe baada ya sisi watu wake kumuomba. Ushwari huanzia katika ulimwengu wa roho
Acha mlango wazi nyumbani kwako alaf sema mungu nilindie sifungi milango wala geti
 
Umenikumbusha kuna kipindi nilikuwa Mombasa mtaa wa Ronald Ngala asubuhi mapema tu Nikakuta mtu kalala chini kafa kashika panga Mtaa wa Ronald Ngala, mombasa wakasema huyo ni jambazi alikuwa anakata watu na mapanga askari wa Kenya wamemuua wamemuacha sehemu ya wapita njia wengi ambayo hata majambazi hupita ili wamtambue mwenzao kuwa na wao zama yao inakuja wakithubutu

Hiyo maiti polisi waliiichukua muda wa saa nane mchana toka wamuue usiku akipora usiku akipora wapita njia na panga lake.Walimtandika risasi wakamuacha hapo

Niliporudi siku ingine miaka miwili baadaye niliambiwa hilo eneo hajaawahi porwa mtu hata ndala iliyochakaa ujambazi ulishaisha majambazi wanauogopa huo mtaa wa Ronald Ngala kama ukoma kama eneo hatarishi na nuksi kwao

Sasa Tanzania kwa sasa ni nuksi kwa majambazi na magaidi hilo wamegundua hilo
 
Majambazi bado yapo yalichobadili ni mbinu tu , ukisikia kiongozi fulani kachota pesa za umma huo ni ujambazi.


Mengine yanauza maji ,mafuta na udongo wanaoita wa upako ,majambazi yapo kila kona na yanabamiza kama kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…