Hivi utotoni hasa wanaume hamjawai fanya hii kitu

Na mama alikua ananitupia mimi zaidi majungu kwa sasabu tulikua watoto wa mama na wa mama mkubwa mke mkubwa wa mzee ambae alishafariki kitambo na karibu wote tulikua karibu marika🤣
Itakua kuna namna ulikua sturbbon😁afu watoto wa maza mkubwa walikua humble mazaako akawa anawish uwe kama wale tatizo lako ukawa bize na ubwabwa
 
Itakua kuna namna ulikua sturbbon😁afu watoto wa maza mkubwa walikua humble mazaako akawa anawish uwe kama wale tatizo lako ukawa bize na ubwabwa
Itakua ni swaga za mama yangu kutaka kuonekana sio mama wa kambo tu , sie wa kwake tulibamizwa kama ngoma, ila kwa sasa tunabamizwe wote tu kila mmoja aliza atume pesa 5% ya kipato chake kwake na hataniii wala hacheki ya yeyote
 
Zamani mchele utauonea wapi bei yake ilikia ni mara 3 ya unga, unga ilikua kilo ni Tsh 50/= mchele kilo ilikua ni Tsh 150/= hii 150 ukiwa nayo ilikua unaweza kununua baiskeli mpya, kwahiyo kilo moja ya mchele ilikua ni sawa na bei ya baiskeli
Ngoja vijana wa juzi Poor Brain Monetary doctor Nomadix na Al-mukheef waje kubisha kama hatujawatia stiki za kutosha.

Tumechoka kuwaelekeza vijana kidiplomasia.
 
Zamani mchele utauonea wapi bei yake ilikia ni mara 3 ya unga, unga ilikua kilo ni Tsh 50/= mchele kilo ilikua ni Tsh 150/= hii 150 ukiwa nayo ilikua unaweza kununua baiskeli mpya, kwahiyo kilo moja ya mchele ilikua ni sawa na bei ya baiskeli
ni kweli mchele ulikuwa hauzoeleki wakati huo. Sherehe nyingi ziliishia kula ugali wa sembe nyeupe pee na makande. Ikitokea sherehe kuna wali basi mtapangwa makundi ya watu kuanzia watano na kuendelea kisha mnatengewa sinia au karai la wali mle. Ulaji wenyewe mnakula kwa fujo, wadogo wanapunjika maana wakubwa wanamega matonge makubwa
 
Itakua ni swaga za mama yangu kutaka kuonekana sio mama wa kambo tu , sie wa kwake tulibamizwa kama ngoma, ila kwa sasa tunabamizwe wote tu kila mmoja aliza atume pesa 5% ya kipato chake kwake na hataniii wala hacheki ya yeyote
Haya mambo ya mama wa kambo ni siku hizi tu zamani wote dabi dabi mnapiga kazi kama wafungwa
 
Wewe ni kijana wa 2000 itakuwa , zamani zetu huo mchele wa mpaka wewe utumwe ukaupime utakua umefanya jambo la ushujaa kijiji kizima🤔
Tena hata kutumwa anatumwa kaka mwenye akili ili asije kumwaga kipindi hiko mifuko ya rambo. Ubwabwa ulikua unanukia balaa
 
Honestly nyumbn ilikuwa kawaida sana, japo sio kila siku Ila hatujawah ku concentrate kwenye mapishi ety siku wali umepikwa nat,

Nyumbn tulikuwa tunajua kabisa wali unaliwa lini na pilau, lini au wali mix maharage lini so hatukuwa hivyo wa kushangaa sana sana ni kuwa upikwe mwingi tushibe,


even chapati nimekua nakuta hizo

Me favorite foods ni ugali nyama mboga mboga hv, ndz nyama, au maharage ama njerege mix viazi,

Pilau, chapati, ndo the best basi mm sio shabiki wa wali kiuhalisia nakula sababu ya njaa
 
Tena hata kutumwa anatumwa kaka mwenye akili ili asije kumwaga kipindi hiko mifuko ya rambo. Ubwabwa ulikua unanukia balaa
Yani mama yangu hadi ratiba ya leo kipikwe nini ilikua ukutani , akianza mharage ni ndizi maharage za kusonga, ugali maharage , makande maharage, kuna mahindi ya maharage ya kichaga yanaitwa ngararimo, mara kiburu nacho ni maharage ya kusonga, akitoka hapo anapika mtango wa maharage wa kirombo tofauti ni huu hauna magadi tu😛
 
Kuna mwamba alishawahi kula wali hadi akashindwa kusimama kurudi kwao akaanza kurudi kwa kutambaa, maana wali haikua ni chakula cha kawaida kama siku hizi ilikua ukiona wali unakula hadi tumbo likaribie kupasuka maana hauna uhakika kama utawahi kuuona tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…