Hivi utotoni hasa wanaume hamjawai fanya hii kitu

Hivi utotoni hasa wanaume hamjawai fanya hii kitu

Ila kwa sisi tuliokulia Mbeya wali tulikua tunaona kitu special kuliko vyote hapa ulimwenguni.... uupunga
 
Ndio mkuu tangu mwanzo
Hongera mkuu.
Sote humu tulijua labda ulianza kupenda upishi ukiwa na miaka 61 baada ya kustaafu, ndiyo maana Kuna watu wanasema jamaa hakutumia mshahara na pension vizuri ndo maana ameanzisha mgahawa.
 
Kuna mwamba alishawahi kula wali hadi akashindwa kusimama kurudi kwao akaanza kurudi kwa kutambaa, maana wali haikua ni chakula cha kawaida kama siku hizi ilikua ukiona wali unakula hadi tumbo likaribie kupasuka maana hauna uhakika kama utawahi kuuona tena
sijui kwa nini wali ulikuwa ni chakula ghali sana miaka hiyo, ina maana nchi ilikuwa inalima mpunga kidogo?
 
Umenikumbusha jamaa mmoja alikuwa anaula wali kwa mikono miwili ili tu awashinde wenzake..... Walikuwa wanakula kwenye sinia.

Ilikuwa miaka ya 90 kwenye msiba wa katibu kata wetu.
kwenye magrupu ya kula huko shereheni watu walikuwa wanakula kichafu na wenzao hawaoni kinyaa, bora mtu abugue madonge ya wali tu
 
Ulaji wali una wataalamu wa kula chakula hicho. Jamaa yangu mmoja toka bara yeye alikuja pwani. Kukawa na tukio la kula wali jamaa akajumuika kula. Mara akashiba akajiondoa grupuni, wazee wakamaindi na kumuambia hajui kula wali, inakuaje anashiba haraka na kuacha sinia bado lina wali? Wale wataalamu wa kula wali wana namna yao ya kupakia. Wakiona upande mmoja wa tumbo umejaa wanabadili mkao ili chakula kikae levo huko tumboni. Tumbo linasetiwe lijae kisawasawa ndio mtu anaona kala wali inavyotakiwa!
 
Kituko, kuna mzee mmoja kwenye harusi yeye alivamia grupu la watoto la kula wali ili amsaidie mtoto wake asipunjike kumega matonge. Ikabidi amege matonge makubwa na kuyaweka kwenye kanzu yake ili mtoto wake aje kula taratibu kwa muda wake, maana kwenye grupu lao ulaji ulikuwa ni wa fujo sana kugombania kumega matonge
 
Kuna mwamba alishawahi kula wali hadi akashindwa kusimama kurudi kwao akaanza kurudi kwa kutambaa, maana wali haikua ni chakula cha kawaida kama siku hizi ilikua ukiona wali unakula hadi tumbo likaribie kupasuka maana hauna uhakika kama utawahi kuuona tena
Kipindi hiko mzee wali ulikua hauna siri ,unapikwa hapa mpaka nyumba ya 10 wanahisi hiyo harufu mchele unavyonukia ...halafu unapikwa na lile ndondo og dah oya noma.
 
Sijui kwanini wali ulikua issue kubwa. Nakumbuka miaka ya 96 mpaka 2000 ilikua ni mara moja mwezi mzima.
 
Nyakati zile kwenye harusi wali uliliwa high table tu tena kwa bwanaharusi, bi harusi, padri/mchungaji na wapambe wa harusi tu. Wahudhuriaji waliishia kula makande na ugali
 
Hata sasa hvi bei ya piki piki ni sawa na bei ya laptop 💻..
Bei ya i phone ni sawa na piki piki tatu
Mkuu tunazungumzia bei ya mchele wala siyo habari ya pikipiki na laptop 😅😂.

Umeshawa kuishi katika zama ambapo bei ya kilo ya mchele ni sawa na bei ya pikipiki mbili?.

Sema ukweli wako na mola atakujalia.
 
Ngoja vijana wa juzi Poor Brain Monetary doctor Nomadix na Al-mukheef waje kubisha kama hatujawatia stiki za kutosha.

Tumechoka kuwaelekeza vijana kidiplomasia.
nakumbuka mchele kijijini ilikuwa kuuona mpaka krismas au mwaka mpya, au kwenye harusi tu. Kuna wahuni enzi hizo wanavizia umepikwa kwenye harusi, ukishaiva wanabeba sufuria wanasepa nalo msituni!
 
Back
Top Bottom