Hivi utotoni hasa wanaume hamjawai fanya hii kitu

Hivi utotoni hasa wanaume hamjawai fanya hii kitu

Unasimangwa na haina kususa hiyo ukisusa wenzako wanaendelea kukifinya cha mtume
 
Ngoma mpaka ipikwe ilikua ni shughuli na likipikwa tulikua tunasugua ndala zetu za bata bata zinga'aa kinouma na kitaa tunatangaza bifu kwa wenetu kuwa hatuchezi nao yani🤔
Siku ya wali bila kuoga na kujisugua vizuri unaweza kuukosa kimasikhara kabisa na mazeri akaleta ukauzu mpaka uoge na sio kupiga pasipoti ili umdanganye.

Tuliokulia kwenye baridi vita ya kuoga ilikua ni kali kwelikweli.
 
Kuna ile una ambiwa kapime mchele vikombe 2 wewe unaweka 3 ili ubaki ule na kiporo kesho yake mchana au asubuhi ili tu usile ugali 😂😂 dah nimekumbuka mbali
Inaelekea kwenu mliishi maisha ya shida sana, pole muhanga.
 
Kuna ile una ambiwa kapime mchele vikombe 2 wewe unaweka 3 ili ubaki ule na kiporo kesho yake mchana au asubuhi ili tu usile ugali 😂😂 dah nimekumbuka mbali
Mkuu umenimbusha mbali Bado Kuna Ile ya kuiba mchele na kuweka mfukoni huku unatafuna kama Karanga au mnaloweka ila tulikua watundu Vibaya unapigwa makwenzi viboko wala husikiki kesho unarudia😂😂 hawa watoto wetu wa kizazi cha GEN Z na Gen Alpha sijui wanaficha nini labda Condom na P2😂😂
 
Kuna ile una ambiwa kapime mchele vikombe 2 wewe unaweka 3 ili ubaki ule na kiporo kesho yake mchana au asubuhi ili tu usile ugali 😂😂 dah nimekumbuka mbali
Huo ujinga ulikuwa nao peke yako huko uswahilini kwenu, kwa sisi tuliozaliwa maeneo ya kishua kama Tandare uzuri hatuna experience hiyo.
 
Ngoma mpaka ipikwe ilikua ni shughuli na likipikwa tulikua tunasugua ndala zetu za bata bata zinga'aa kinouma na kitaa tunatangaza bifu kwa wenetu kuwa hatuchezi nao yani🤔
Kijijini kwetu mchele haikuwa story kwakweli kwasababu karibu kila kaya ilikuwa ina miliki shamba la mpunga, lakini sasahivi sehemu kubwa ya yale mashamba zimejengwa nyumba za kuishi watu. Kijijini kwetu soda ilikuwa ndiyo story ya kuvutia
 
Pia wali wa zaman ulikuwa mtamu sana ukilala kipolo chake ilikuwa balaa na maharage yalikuwa matamu mno siku hiz havina ladha
 
Pia wali wa zaman ulikuwa mtamu sana ukilala kipolo chake ilikuwa balaa na maharage yalikuwa matamu mno siku hiz havina ladha
Pale kijijini kwetu ilikuwa ukipita jirani na bonde la mpunga basi you can feel the smell haswaaaa, na imani unaijua vyema harufu ya mpunga mzuri.
 
Back
Top Bottom