Hizi ndio kauli zangu pendwa kutoka kwa mshana Jr

Hizi ndio kauli zangu pendwa kutoka kwa mshana Jr

Burn the bridge _Tz

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2021
Posts
2,319
Reaction score
6,878
Kupitia post na mazungumzo na Mr IQ intelligence mshana Jr The platinum nimejifunza haya hapa.

01.Waganga wanafanya KAZI kwa kumuomba Mungu, na wewe usimuombe Mungu kupitia mganga(Muombe Mungu moja kwa moja utafamikiwa)

02.Sema sana ongea sana ila Usiombe yakukute.

03.kwenye maisha Kuna kupata na kukosa, jitahidi uwe fungu la kupata..

04.Mimi naweza kusema ndio ni mchawi ila naweza kusema hapana Mimi sio mchawi😂

05.Ukifika wakati wako wa kuoa, utaoa tu akili inakuambia oa, hakuna haja ya kuwa na haraka.

06.Ukifanya makosa usijilaumu, jifunze sana kupitia makosa Yako.

07.Kama kijana usiendekeze sana masuala ya siasa, komaa sana na mafanikio Yako.

08.No reform no Election

09.Ukitaka kuwa na hekima Muombe sana Mungu.

10.Kama mambo hayaendi, tumia chumvi.

11.Usitumie uchawi kupata hela, ila itafikia hatua utatumia uchawi kulinda hela.

12.Jitahidi kupunguza sana maaadui kadri uwezavyo.

13.kusaidia sio utajiri, kusaidia ni moyo, basi ikifikia hatua mtu amekusaidia na wewe jitahidi kusaidia wengine.

14.Utapata tu mafanikio, ila jipe muda ukiwa na haraka utaharibu.

15.waganga wengi waongo.

16.Tafuta kwanza pesa, wanawake wapo.

17.omba Sana amani kuliko hela.

18.Hela sio chanzo Cha furaha.

19.karibu pwani.

20.Tumia pombe kama starehe, usitumie pombe kupunguza stress au matatizo

21.ukifanya wema usisubiri malipo, Mungu atakulipa kwa wakati wake.

Bado naendelea kujifunza.
 
Back
Top Bottom