Hizi ndizo sababu za kutopokea simu za baba yangu mzazi

Lambisha asali mkuu, kwani zamani kipindi wenzio wanaoana humu we ulienda wapi? Pole sana mkuu😅
Sasa hivi nimeanza kutafuta mialiko mbalimbali ya warsha na matamasha ya wamama najua huko sitakosa .

Juzi nilikuwa Rungwe kwenye tamasha fulani ,nikakuta mimama ni mibonge mibonge tu alafu inatembea kwa shida ,nikajiwqzia mimi na hili tumbo langu ,nimpate tena mwanamke mwenye kitambi na anatembea kwa shida mbona itakuwa vichekesho basi namba sikuchukua ila bado nasaka
 
Mkuu tatizo kujibu hvo unaona ni sawa kabisa
 
Nje ya mada: Siku baba huyo akivuta shuka "akifa", at some point kwenye life yako, utatamani upate mtu wa kumpigia simu, umuite baba hutampata.

Ushauri: Mtendee vizuri baba yako bwamdogo, hutakuwa nae muda wote wa maisha hako baba yako. Na yeye, alikuwa anakutana na hali ngumu kama mwanaume. Hali unayopitia wewe hakuna mwanaume hapitii, lakini usikubali uanaume ukutoke. Kamata simu ya mshua, mweleze situation yako, yeye pia anayajua maisha ya kiume.

Kuna watu wanatamani wapate baba hata wa kufikia, hawana.
Punguza utoto, grow up, be a man.
 
🎤 Iceberg9 Njoo
 
Mimi huwa nashangaa sana, waafrika wametengeneza utamaduni wa kutaka kusaidiwa, utafikiri msaada ni haki yao.

Mtu ashafeli huko, amechezea ujana wake anaanza kufosi kusaidiwa utafikiri ni haki yake.

Msaada ni hiari.

Msaada si lazima wala si haki.

Wazazi wapumbavu wanaozaa bila malengo ndio huwageuza watoto vitega uchumi.

Wao walishaharibu huko ujanani, wanaanza kusumbua watoto uzeeni.

Wazazi wa namna hii ni kuwaacha, wakafie mbelee!!

Hii Dunia kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe.

Wakusaidiwa na kupewa matunzo ni mtoto kwanzia amezaliwa mpaka umri wa miaka 18 to 20 years.

Baada ya hapo kila mtu ajipambanie mpaka kufa.

Kusaidiana kupo kwenye hali za dharura na za msingi tu, Sio kila wakati li mtu linataka kutumiwa hela tu!
 
Nimecheka jmn😂 kila siku mnatushauri tusichague sana, ona wewe ambavyo hutaki walioshiwa uroto🤣

Sikukuu ya wanawake imepita walikuwa wamekusanyana sana ungecheza mitaa hiyo faster sana unajiokotea kitu🤗
 
Mkuu hiyo hali hata nimi nilipitia wakati ndio nimepata kibarua, ndugu walinisakama sana kutaka misaada. Ilikuwa mbinde kwa sababu wakati nahitaji kujipanga ndugu wanataka kunipa majukumu ya familia zao.

Sio hali nzuri hata kidogo kuikubali. Ukweli utakuweka huru. Tafuta muda wa kumchana ukweli mzee, atachagua mwenyewe kama aelewe au asielewe, lakini wewe umempa ukweli
 
Mkuu tatizo kujibu hvo unaona ni sawa kabisa
Unapotaka kumuelezea mtu kweli unamchana live, hata kama ni mzazi.

Mwambie wewe bado unajitafuta, bado huna uwezo wa kumsaidia yeye.

Afikirie namna nyingine ya kuendesha maisha yake. Asiweke matarajio makubwa kwako.

Kama haelewi sasa, una mblock kila mahali. Akafie mbele!
 
Dahh watupe ajira tu tuone kama kweli tuna matatizo ya namna hii au ni stress za maisha kiujumla..
Maviongozi mafisadi kazi yao ni kujaza minofu ya kuku kwenye matumbo yao , hayaweki mazingira mazuri ya maisha bora kwa kila mtanzania , vijana wana ishi kwa kutegemea kubeti tena wasomi , jumapili nao wachungaji wanakazia shida zao ni matatizo ya kiroho wasali sana, wewe unaona hapo kuna mabadiliko?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…