min -me
JF-Expert Member
- Jul 20, 2022
- 23,322
- 64,738
😁😁 ukiondoka unaondoka tu kama unavyokula kukuTukipndoka hapq duniani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😁😁 ukiondoka unaondoka tu kama unavyokula kukuTukipndoka hapq duniani
Roho wa Mungu hawezi kufanya kazi na Watu wachafu...!Ni huyo huyo roho mtakatifu aliyekuwa anamuongoa nabii Dominik (kiboko ya wachawi) na akapata wafuasi wa kutosha.
Huna akili kabisa.Hakuna haja ya kuwauawa watu wenye mapepo kwa sasa kwa sababu Jina la Yesu Lipo. Unalikemea pepo linatoka na mtu anabaki huru.
Hongera sana mkuu, nimekuelewaRoho wa Mungu hawezi kufanya kazi na Watu wachafu...!
Kila mtu anayo Nguvu ndani yake pale Moyo wake ukiamua...!
Na ukaamua kupita kwenye Kanuni za Mungu, unaweza kuhamisha Mlima, means
-Ukaacha Dhambi.
-Ukawa ni mtu wa kuomba.
-Ukasimama kwenye Njia za Mungu etc.
Sasa Watu hawataki kufata Kanuni, wanataka Shirt cut, ndo wanakutana na Mataperi, ndo wanauziwa Mafuta, ndo wanauziwa Maji etc.
Mungu hana Udalali.
Sijamdharau mtu. Asiye na akili ni amdharauye mwenzake.Huna akili kabisa.
Mimi ni mpumbavu au mjinga??? Lazima uchague neno moja Kati ya hayo maana mtu mmoja hawezi kuwa mjinga na mpumbavu Kwa pamoja..Au ulisoma kisomo cha ngumbaru ukubwani.??Wapumbavu kama wewe kwenye nyuzi kama hizi lazima muwepo. Rais anaitwa MamaSamia2025? Mbona wewe ni mjinga kiasi hiki? Huu uzi ni kwa watu wenye akili tu. Haukusu wews.
Quran kariim ni fiksi?, kime jaa ukali?,Biblia ni fiksi tu.
Kurani ni fiksi influenced na fiksi za biblia.
Vitabu vyote viwili vimejaa ukatili wa kutisha kwa vile viliandikwa enzi wanadamu wanafanyiana ukatili huo.
Mf. Kuteketeza mji mzima ilikuwa inawezekana kwa vile watu waliiishi ndani ya miji imezungushwa kuta (hata movies zinaonesha).
Mambo kama Kusulubishwa ilikuwa kawaida enzi hizo.
Ukatili mwingi sana ulifanyika.
Yaani una maanisha mungu na yesu ndio waliuumba ulimwengu?Ukisoma Yohana 1: 1 - 18
Utaona inatoa majibu ya kwamba wakati wa uumbaji wa ulimwengu na vitu vyake, utaona ulimwengu ulifanywa na Mungu baba na mwana, huyu mwana katajwa kama Nuru au Neno aliyekuja kufanyika mwili (Yesu Kristo)...
Yaani una maanisha mungu na yesu ndio waliuumba ulimwengu?
Biblia huwezi kuisoma kama vitabu vingine ukaielewa. Kuna vitu vinaitwa parables na allegories nyingi kwenye biblia na pia unahitaji neema ya Mungu ikuangazieMimi ni mkristo na ninaamini Mungu yupo na anatenda. Ila kuna mambo ukisoma kwenye biblia lazima ujiulize maswali mengi sana yanayokosa majibu. Leo nitashea nanyi mambo ambayo naona kama yana ukakasi;
1. Kwenye Mwanzo 1:26 imeandikwa kuwa Mungu alisema tuumbe mtu kwa mfano wetu. Nimejiuliza ina maana uumbaji ulifanywa nae kwa kushirikiana na wengine? Hakuwa peke yake? Hao wengine kina nani?
2. Mwanzo 6 - 10 kuna stori maarufu ya Nuhu. Hii ni stori ina ukakasi zaidi. Nikiandika maswali yote niliyojiuliza uzi utakuwa mrefu. Ninashauri mkaisome ili tuifungulie uzi wake.
3. Kutoka 11:5-6 kuna maandiko yanayosema kuwa wazaliwa wa kwanza wote wa wamisri kwa upande wa binadamu hadi wanyama watauwawa na Mungu mwenyewe ili waisraeli wapewe ruhusa ya kwenda nchi ya ahadi. Kiukweli haya yalikuwa ni mauaji ya halaiki kwa wasio na hatia. Unaambiwa hadi mzaliwa wa kwanza wa mbuzi, kuku, ng'ombe, mbwa na farasi waliuwawa. Kwanini isingetumika njia nyingine hao waisraeli wakaondoka?
4. Kitabu kizima cha Joshua kimejaa stori za mauaji matupu. Ikumbukwe Joshua alichukua nafasi ya Musa kwenye kuwaingiza waisraeli nchi ya ahadi baada ya kifo cha Musa. Nchi waliyoahidiwa ilikuwa tayari ina wakazi wake ambao ilibidi wauwawe wote ili kuwapisha waisraeli. Hivi ilishindikana vipi kufanya kama alivyofanya Mama Samia kuwatoa wamasai Ngorongoro na kuwapeleka Msomera kwa amani kabisa bila kumwaga damu? Kama leo 2024 bado kuna maeneo duniani hayajakaliwa na binadamu ilikuwaje enzi za Joshua? Ukisoma kitabu cha Joshua utaona kila sehemu waliyopita walikuwa wakiua wenyeji watakaowakuta. Kulikuwa na sababu zipi za msingi za mauaji haya yote?
5. Ayubu 1:6-12 utaona stori ya shetani alipojiunga na wana wa Mungu kupita mbele ya Mungu kumwabudu hadi Mungu akashangaa imekuwaje shetani akawa eneo lile? Baada ya hapo Mungu na Shetani wakakubaliana kwenda kumjaribu Ayubu kwa sharti la kutogusa mwili wa ajabu (kumuua). Katika yale majaribu watoto wa Ayubu waliuwawa na shetani. Naweza kusema ni mauaji yaliyokuwa na approval toka juu. Ilikuwa kazi maalum. Je, sio kwamba wawili hawa hukutana na kukubaliana baadhi ya mambo? Sio kwamba kuna kazi za shetani zina kibali maalum?
Hiki kichaka mnachojifichia tumeshakichoma. Njoo na sababu nyingineBiblia huwezi kuisoma kama vitabu vingine ukaielewa. Kuna vitu vinaitwa parables na allegories nyingi kwenye biblia na pia unahitaji neema ya Mungu ikuangazie
Who is an enemy of Gabriel?Say, ˹O Prophet,˺ “Whoever is an enemy of Gabriel should know that he revealed this ˹Quran˺ to your heart by Allah’s Will, confirming what came before it—a guide and good news for the believers.”
Mkuu halaka sana naomba hamisha mlima kilimanjaro uupeleke sudan wanateseka na joto ukishindwa mwambie mwamposa.Roho wa Mungu hawezi kufanya kazi na Watu wachafu...!
Kila mtu anayo Nguvu ndani yake pale Moyo wake ukiamua...!
Na ukaamua kupita kwenye Kanuni za Mungu, unaweza kuhamisha Mlima, means
-Ukaacha Dhambi.
-Ukawa ni mtu wa kuomba.
-Ukasimama kwenye Njia za Mungu etc.
Sasa Watu hawataki kufata Kanuni, wanataka Shirt cut, ndo wanakutana na Mataperi, ndo wanauziwa Mafuta, ndo wanauziwa Maji etc.
Mungu hana Udalali.
Kwenda zako huko.Biblia ni kitabu cha kweli na MUNGU anayetajwa kwenye hicho kitabu ndiye MUNGU wa kweli.
Sijajua kuhusu Quran mana sijawahi hata kuishika, ila huwa nasikia baadhi ya aya zake zikitajwa na watu mbali mbali.
Watu wanaosema Biblia ni kitabu kilicho jaa janja - janja ni wale ambao hawajawahi hata kuombea watu wenye mapepo na yakatoka.
Mtu mwenye mapepo anaweza akakusemesha baadhi ya mambo yaliyoko kwenye Bible.
Alafu baadaye ukija kumuuliza huyo mtu kuhusu hayo mambo alokuwa anakusemesha atakuambia Mimi sijaongea na wewe kuhusu hayo mambo.
Hi imewahi kunikuta zaidi ya maramoja.
Mimi sio Pastor ila watu wengi huwa wananiamini na sijaandika ili kubishana na watu ila nimeandika mambo ambayo nimewahi kukutana nayo.
Anza kutwambia huo ukweli wa biblia kwanza.Niambie kitabu tofauti cha KIROHO duniani kilicho Bora cha kweli kuliko Biblia. .
Anza kutwambia huo ukweli wa biblia kwanza.Niambie kitabu tofauti cha KIROHO duniani kilicho Bora cha kweli kuliko Biblia. .