One on two....
Nanukuu,
"Punde SI punde marafiki zake binti wakafika, Basi ikawa Ni wanaume 3 na wanawake 3, mezani kumebalance. Basi Pombe zikaongezwa na nyama zikawa Ni mwendo wa bandika bandua mpk MDA flani nimeimaliza bapa ya 2,nmeianza bapa ya 3 nainuka Kwenda chooni haja ndogo, nikaanza kujihisi Kama network kichwani hazisomi vizur, najhs kizunguzungu."
Siku nikifanya hayo mliyo yafanya wewe, muhaya na mnyakyusa ntajiona na mdhambi zaidi ya shetani.....[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Siku Moja nilipatwa na tukio sijawai kusimulia mtu mfukoni nilikua na kama laki 5,
Nikawa na appointment na rafik angu let say y nikiwa ma msubir mida ya saa Moja na nusu kuelekea mbili usiku lile eneo nilikua stranger....
Nikatafuta kijieneo nikae walau nisogeze muda wa kumsubir rafik angu y
Nikaona sehemu ya wazi wameweka viti na watu wanapata kinywaji so nikajongea Nika agiza flying fish Moja nikaanza kuinywa......
Yule mdada akaona Nina mapene mfukoni so akaja akawa ananisemesha na kunizoea
am 4 real nipo cool na sinaga shobo na mazoea....
Nikamaliza flying fish Moja nikamwambia aniongeze ingine kumbuka jamaa y still hajafika....................
Nilipo kua naendelea kuburudika flying fish ya pili...
Wakawa wanapita jamaa watatu wanaonyesha wamelewa sana gafla mmoja wao alipo fika kwenye MEZA Kwa bahati mbaya akaigonga grass yangu ikadondoka chini....
Jamaa wakaniomba radhi muhudumu akaja akanibadilishia grass ikiwa na unyevu unyevu.....
Nikamimina kinywaji chote kwenye grass na kukinywa na kukimaliza....Nikapata wazo fasta ninyanyuke niende nyumbani nikanyanyuka nikaenda kupanda bajaji......
Nikafk mitaa ya karibu na home najulikana pale Huwa naendaga several times nikaenda sehemu wanauzaga chips mishikaki na kuku
Nika agiza waniandalie nikatafuta position ya pembeni kwenye kiti nikakaa....
Lahaula!! Nilikuja kuamka saa 8 usiku nikashituka nilileta tahamaki nyumbani kwetu...Kwa wife missed call kama 100 maana haikua kawaida [emoji851][emoji4]
Kujisachi Kila kitu changu kipo sawa na kumbukumbu zangu hazina twakwimu ndipo nikaenda kwangu nili tafakar sana hiki kitendo....wale watu waliniwekea madawa SEMA Mwenyezi MUNGU alikua upande wangu....