😛😛😂😂😂😌
yaani kama namsikia na kumuona vile, akiwa anageugeuka kuonyesha na kusema, '....hapa ndio ya kwanza ilipoingia'....', hapa ndio dereva aliponiambia geuka, alinichuuza nikapewa nyingine!, '....nikajilalia...', wakendelea kumwaga aisee mijamaa mikatili, mmh nyingine imeingia wakati najaribu kuangalia wapi cctv ipo....duh!
Jokes aside aliumia kweli na simwombei kiumbe chochote machungu anayo yapata au aliyoyapata,kwani majeraha aliyopata mhhh manake hata katika mchepuko anaulizwa na '...hapa je? Yaani anatoneshwa kidonda na mchepuko...
Hatahivyo na yeye ajaribu kupata usaidizi wa majeraha yake badala ya kuendelea kuchokonoa kidonda kwa kutoa dukuduku hadharani wakati anajua Hayati magufuli alikuwa na Familia, aidha walikuwa hawajui hulka zake au wameanza kujua baada ya mauti, kwa vyovyote vile inauma.
Wananchi wameumia, hatuwezi kuendeleza kutoneshana vidonda sababu tu ya kutaka dola, sababu ya kutaka huruma.
Tundu Lissu anaweza kupaa bila kinyongo au kisasi.
Amani