Hoja za Lissu ni zilezile za tangu aje Tanzania kugombea Urais 2020

Kama agenda yake ni KATIBA mpya basi huyo ndiye mwamba tunayetaka kumsikiliza.Maana katiba ndio inayotengeneza mfumo wa utawala na namna ya kuwajibika. Labda Kama hujui nguvu ya katiba katika maisha ya kawaida, ukadhani NI kakijitabu tu basi, ninakupa pole Sana. Na hiyo ndio 95% suruhisho la matatizo yetu
 
Wewe una hoja gani zaidi ya Uchawa? Naona Wajinga mnaongezeka kwa Kasi ya kitisha
 
Eti kaenda kijijini kwao kuonyesha makovu yake, duh. Hilo lijamaa limeshageuza makovu kuwa agenda kuu.


πŸ˜›πŸ˜›πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜Œ
yaani kama namsikia na kumuona vile, akiwa anageugeuka kuonyesha na kusema, '....hapa ndio ya kwanza ilipoingia'....', hapa ndio dereva aliponiambia geuka, alinichuuza nikapewa nyingine!, '....nikajilalia...', wakendelea kumwaga aisee mijamaa mikatili, mmh nyingine imeingia wakati najaribu kuangalia wapi cctv ipo....duh!

Jokes aside aliumia kweli na simwombei kiumbe chochote machungu anayo yapata au aliyoyapata,kwani majeraha aliyopata mhhh manake hata katika mchepuko anaulizwa na '...hapa je? Yaani anatoneshwa kidonda na mchepuko...

Hatahivyo na yeye ajaribu kupata usaidizi wa majeraha yake badala ya kuendelea kuchokonoa kidonda kwa kutoa dukuduku hadharani wakati anajua Hayati magufuli alikuwa na Familia, aidha walikuwa hawajui hulka zake au wameanza kujua baada ya mauti, kwa vyovyote vile inauma.

Wananchi wameumia, hatuwezi kuendeleza kutoneshana vidonda sababu tu ya kutaka dola, sababu ya kutaka huruma.

Tundu Lissu anaweza kupaa bila kinyongo au kisasi.

Amani
 
We we magonjwa mtambuka unacheka unaona haya ya kucheka😁
😁😁😁😜😏😝
 
Jee hayo anayazungumzia kwenye mikutano? Hapana usipotoshe makusudi.
Kwenye mikutano kazungumzia hali ya nchi na ugumu pamoja na utatuzi.
Hayo ya kushambuliwa kayasemea kwenye mahojiano mbalimbali na yameendana na maswali yaliyo andaliwa na walio mwalika.
Mlitaka aulizwe hali ya afya yake yeye ajibu kuhusu kilimo cha umwagiliaji? Msiwaze kijinga namna hiyo!
 
Za CCM ni zipi ambazo ni mpya kwa zaidi ya miaka 50? Ujinga
 
Mbona ccm toka mwaka 1977 hoja zile zile ni maji,barabara Na madawati [emoji3]
 
Kwani matatizo yenu watanzania yamebadilika?

1.UJINGA.
2.MARADHI.
3.UMASIKINI.
 
Kwani matatizo yenu watanzania yamebadilika?

1.UJINGA.
2.MARADHI.
3.UMASIKINI.
Bora hayo kuliko makovu ya mtu kwani kuna mtu hana kovu makovu yapo kwa watu wengi tu

USSR
 
Hivi hiyo katiba ndo itaitoa CCM madarakani ?

Lissu alituachia nchi leo anakuja na complications kibao

Mwambieni tufanye kazi kwanza, maneno yote tunayajua.

Sijasikia hata akitushukuru tuliompigia kura.
 
Japo umechangia kiutu uzima, nakukosoa kidogo. Tusimchagulie Lisu namna ya kulia. Mwacheni alie kadri atakavyo kwani ndio njia pekee ya kuponya hisia chungu. Hao wanaoumizwa na kulia kwake wavumilie tu kama yeye alivyovumilia maumivu makali kabisa kuwahi kumtokea maishani.
 
Sidhani kama kuna mtu anakataa Tundu Lissu kulia.

Sidhani kama kumtaja taja Hayati Magufuli ni hivi na vile ni kulia-
...binafsi naweza sema anamchafua ili yeye aonekane ni bora yake- kumbe jamaa ni lidikteta hatare.

Maumivu yalioipata nchi hii ni makubwa kwa.namno yeyote ile unayoangalia jambo la Kuumia, kuumizwa. ..Machozi hayakuwa ya mamba wala vilio havikuwa vya fisi tuliyoyaona na vilio tulivyosikia ndii ulikuwa mustakabali wa nchi.... Vidonda bado vibichi, yeye anakuja kutonesha tu. Kuna watu na ndevu za masikioni wanaona hayo

Naamini ana uwezo wa kufikisha ujumbe bila ya kutaka/kulazimisha huruma huruma. Kumbuka alikuwepo 2020 kwenye kinyanga'nyiro hatukusikia haya tunayoyasikia, kulikoni?

Nikupe nayoyaona?

Wamefinywa midomo- gagged-kuzungumzia CCM au Raisi moja kwa moja;amekiri hayo juzi kiaina kwa madai yeye hawezi kuzungumzia mambo ambayo mwenyekiti wake anajadiliana na CCM! kwa hivyo yeye hana issue zaidi ya kuonyesha makovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…