Hongera Haji Manara kwa kupewa kazi ya usemaji wa kampuni ya Tigo

Hongera Haji Manara kwa kupewa kazi ya usemaji wa kampuni ya Tigo

Una hekima, japo Manara simpendi ila nilitaka kusema hivyohivyo kuwa hizo ni harakati ktk utafutaji ambazo kila mmoja anapitia kwa namna yake.
Kuna watu wanapenda kumdhalilisha mtu kwa madhaifu ya nyuma.

Kwangu mimi udhaifu uliopita ndio uliyemjenga Glenn wa leo.

Magumu yaliyopita ni udhuhuda wangu kwa Mungu.

Nikumbushe madhaifu yangu yaliyopita nipate sababu ya kumwambia Mungu asante
 
Unajua maana ya title ya MSEMAJI wa kitu fulani?

Huyo Haji anajua hata basic za Sheria? Maana unaweza ulizwa swali la kisheria mbele ya watu wakubwa ukachomesha kampuni.

Ni tofauti na Mwanahabari regular.. Mwanahabari yeye atatuhabarisha tu na sio KUSEMEA taasisi.

Kusemea taasisi inamaana una Mamlaka makubwa mno mno..

Mkuu naona wewe ndiye unayepaswa kujiuliza hayo maswali...

Kuna majibu mengi bado huna...
 
Kuongea siyo hoja. Hoja ni unaongea nini? Mtu unayejitambua sidhani kama unaweza kupata chochote kwenye porojo zake zaidi ya ujinga. Ni kama Makonda.
Mh
Maisha haya usiyachukulie sana serious bro,hata unaejitambua kuna muda wa kusikiliza ujinga ili upate tabasamu na ikibidi kicheko sio kila saa we uko serious ili uonekane una akili
 
Unajua kuitwa MSEMAJI ujue ni jina zito sana.

Lazima Biashara uijue haswa, ujue mambo ya kiteknolojia ujue taasisi mipango yake yaan Strategic plans..

Huyu jamaa kule kwenye Mpira palimfaa kwa kuwa anafaham Mpira maana amezaliwa na kukulia ktk Mpira.

Ila huku kwenye maswala ya 5G mara 4G na unaenda ktk midahalo ya kimataifa kuzungumzia kampuni yako. Una content..?
sidhan kama hajaiva nadhani kabla hajapewa deal alikua class, hawawezi mtangaza tu wakat hajaiva.

kutangazwa kwake ni kama mwanafunzi anae hitimu,mtihani kwanza, una clear SAP zote ndipo una graduate.

Manara kashaiva huyo deal hajalipata jana alilipata muda kidogo ila alikua darasani ndio mana siku zote alionekana mwenye furaha na kuringa kwani alishaanza mpaka na Kulipwa kabla hajawekwa hadharani.

Wana jamvi ndio tumejulishwa jana baada ya SEMAJI ku clear SAP zote.
 
Back
Top Bottom