Hongera Haji Manara kwa kupewa kazi ya usemaji wa kampuni ya Tigo

Hongera Haji Manara kwa kupewa kazi ya usemaji wa kampuni ya Tigo

Jackson Mmbando PR Airtel na zamani Tigo ni mwanahabari na hana cheti chochote cha chuo kikuu cha uhandisi wa mawasiliano na anafanya kazi vizuri tu huwezi jua kama ni mwanahabari...

Hassan Bumbuli aliye NMB sasa hivi ni mwanahabari, mifano ipo mingi

Ikija midahalo au summits za kimataifa kama TAIC, MWC, AfricaCom, TowerXchange, ConnectedAfrica n.k wanaowakilisha kampuni za mawasiliano huwa ni wenye taaluma ya telecom kama CTO's, CEO's n.k...
Unajua maana ya title ya MSEMAJI wa kitu fulani?

Huyo Haji anajua hata basic za Sheria? Maana unaweza ulizwa swali la kisheria mbele ya watu wakubwa ukachomesha kampuni.

Ni tofauti na Mwanahabari regular.. Mwanahabari yeye atatuhabarisha tu na sio KUSEMEA taasisi.

Kusemea taasisi inamaana una Mamlaka makubwa mno mno..
 
Maswali yako ni mazuri kabisa na wangetakiwa wajiulize hivyo. Ila kama tunavyojua ni kwa Tanzania, watu wenye porojo za kijinga ndiyo huonekana kama ni majembe. Haki ya nani tumekwama sehmu mbaya sana sana na aliyetufikisha hapa ametuweza. Yaani ili kiongozi au mtaalam, ''elimu'' unayotakiwa kuwa nayo ni ujinga na porojo.
Ukiweza kuongea ujinga kwa confidence baasi umetoboa. Kama kweli ni MSEMAJI. Basi kazi ipo.
 
Hongera sana Haji Manara kwa nafasi hiyo adhwimu.God bless!!!

Aliyepewa kapewa.

Itoshe kusema kwamba Mganga wa Haji sio tapeli.
---
Kupitia Ukurasa wake rasmi wa Instagram HajiManara anathibitisha kupata usemaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya tigo. Katika kulieleza hili Haji Manara anaandika:

Alhamdulillah 🙏🏻🙏🏻

Unadhani mimi ni hodari sana kiasi cha kuendelea kupata hizi deals za Makampuni? Hapana ni Mungu tu anaeniangazia na pengine kuuvaa uhusika nnapokabidhiwa jukumu na wao au Taasisi nnazofanya nao kazi.

Kuisemea Kampuni kubwa kama hii hususan katika kipindi hiki cha Holiday na kwa namna walivyojipanga na hizi Zawadi kubwa kubwa ni zaidi ya Mipango ya Mungu, na ni heshma kwetu ndugu zangu.

Sisi tumetoka Uswahilini huko kuja kupewa fursa kama hizi ni ushindi kwa Mahaslers wote.

@tigo_tanzania mmepata Semaji, Mmepata Mwanamme hasa anaejua kazi yake, Mtaenjoy mwaka huu.
Mjomba ako Haji hanaga dogo😂😂😂
Zaramo tukuka
 
Hance Mtanashati somaaaa hiyooooooooo....

Big up Mr. Haji....👊👊👊
 
Pamoja na madhaifu yake yote, matusi na lugha chafu ila ukweli Manara ana karama ya umashuhuri.

Kila anachogusa na kufanya ni habari. Sijajua usemaji huo utakuwa wa aina gani hasa kwenye mtandao wa simu ila sina mashaka na utekelezaji wake.

Manara alizaliwa kufanya anachokifanya.
Siku akikudate utakuwa maarufu kama rushyna
 
Back
Top Bottom