Hotuba ya Pieter Willem Botha aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini ya Makaburu

Kwa kuwa nimetambua kuwa wewe umejiweka kwenye sehemu ya kushauli ila wewe hutaki kushauriwa, kukosoa ila hutaki kukosolewa.na kwa mtazamo wako naona unaona kwa kuwa mimi ni kiongozi basi mimi siruhusiwi kushauri au kutetea yale ninayoamini.

Mimi sio mwumini wa siasa nyepesi nyepesi, nivizuri kujadili mambo ya Taifa but with critical minds,sio mtu anakurupuka hana utafiti wa kutosha anaandika andika bila habari za kutosha,ilimradi watu waone ameandika, KWA KIFUPI NIMEAMUA KUISHIA HAPA KWANI KILA NIKIKUULZA SWALI UNAKUWA OUT OF CONTEXT.

NA MIMI MJADALA UNAPOKUWA OUT OF CONTEXT NASHINDWA KUUJADILI, By the way it was cool getting to chat with you ,
 
Kisiasa mkuu wangu JINO kwa JINO ndio inatakiwa kwa sababu haya ni maneno ya ushawishi yenye lengo la kuzungumziwa ukweli..Labda nikwambie tu ya kwamba Dr.Slaa amefanya makosa kutoweza kujibu tuhuma hizo kwa sababu watu wakipuuza haina maana ya kukubalika zaidi. Tuhuma zilizotolewa kwa Dr.Slaa ni za kipumbavu kabisa lakini zina nguvu kubwa ya mvuto ktk udini uliopo nchini hivyo labda nikuhakikishie ktk utabiri wangu kuwa Dr.Slaa hawezi kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 kama atagombea.. najua nawashitua kwa kusema hivi lakini hulka ya mnwafrika inasema wazi kwamba uongo ukizungumzwa sana hugeuka kuwa ukweli.

Kuna chuki kubwa sana ya wananchi huko mitaani kuhusu Chadema na hakuna sababu isipokuwa ni Dr.Slaa kwa sababu wameweza kuaminisha watu kuwa Chadema ni chama cha Kikristu na wapo watu wengi independent voters wanaamini hivyo! Dr.Slaa anatakiwa kuwa mstari wa mbele kukana, kupinga na hata kulaani vitendo vinavyotumiwa kujaribu kukiharibu chama tena kama ana uwezo kujitokeza zaidi ktk vyombo vya habari haswa television na kufanya mahojiano yanayomhusu yeye. Kujisafisha ni muhimu hata Obama alifanya hivyo baada ya kushutumiwa kwamba hakuzaliwa Marekani!

JK ni mvumilivu kwa sababu hakuna uongo unaozungumzwa, na hata kama kuna uongo basi kukaa kwake kimya ndiko kunakozidi kuimaliza CCM.. Kama kiongozi, huwezi kutuhumiwa ukakaa kimya, aliyafanya Lowassa na kijna Karamagi leo hii huwezi kuwasimamisha watu hawa mbele za watu wakaaminika. Lakini tazama mtu kama Zitto, yeye anakwenda jino kwa jino hakubali kusingiziwa vitu ambavyo hakuvifanya na mwepesi kukubali makosa kama yapo. Nakuhakikishia Zitto ni mbunge maarufu kuliko wote leo hii na wananchi wengi wana imani naye kuliko hata viongozi wa serikali na vyama hata kama hapa JF hana washabiki wa kutosha...

Siasa zinakuja na maswali mengi na majibu hutakiwa, sii jazba ama matusi kama kina Mkapa wananchi wanataka majibu kukana kwa mdomo na kuonyesha unyenyekevu kwao laa sivyo utapoteza umaarufu, unless iwe kweli - La kuvunda halina Ubani, kama ilivyo CCM.
 

Kuna hoja kadhaa nzuri katika utetezi wako Ndugu Mkandala. Ukimya nao huadhiri sana, kwa maana kwamba kukaa kimya kifalsafa inatafsiriwa kwamba unakubaliana na kinachhosemwa na hivyo huna hoja ya utetezi, au hukubaliani na kinachoongelewa ila umeishiwa pumzi ya kujibu mapigo. Lakini si kila kiongelewacho mtu ukurupuke kujibu, wengine wakishaona hivyo hujenga mazoea ya kupima saburi aliyo nayo mtu.

Kipimo cha uongozi bora moja wapo ni ustahimilivu, itokeapo kiongozi kulipuka haraka kama moto kwenye petrol ni kasoro kubwa ambayo inaweza leta madhara makubwa na kuja kuweka mambo sawa ipo kazi, maana kubomoa ni rahisi lakini kujenga tena itabaki historia kama ya word trade centre ya NY eneo lake kubaki makumbusho ya kutembelewa na watalii. Kwa vyo vyote busara kwanza inahitajika katika kukabiliana na tuhuma zenye harufu ya kuchafuliana kisiasa kuliko kashfa za kweli.

 
Ndugu Bongolander,

Hata Mlowezi Ian Smith, wa Rhodesia (Zimbabwe), alipata kunena kwamba mtu mweusi kamwe asingelitawala nchi hiyo katika kipindi cha miaka 100. Of course, mwenzetu 'Uncle Bob' i.e. Robert Gabriel Mugabe, ametawala (na anaendelea kutawala) nchi hiyo hata kabla ya robo ya kipindi ambacho Bwana Ian Smith alikitabiri.

Lakini matokeo ya utawala wa 'Mjomba Bob' hauna tofauti na tunachokiona leo nchini mwetu. Ninamaanisha kusema: mkoloni alichukua rasilimali zetu nchini kwake (Uingereza). Lakini kujitawala kwetu kulimaanisha mwisho wa unyonyaji huo kwa maana kwamba kile ambacho mkoloni alikuwa akikichukua nchini mwetu na kukipeleka nchini mwake, kingelibaki (baada ya kujitawala) kwa manufaa (maendeleo) ya wananchi.

Lakini miaka 50 baadaye, licha ya kujitawala, tunaona kinyume chake. What went wrong? Ninadhani kauli ya Bwana Botha ina imply ukweli kwamba 'Mvunja nchi ni mwanchi'; na, kama unavyosema: Mr Botha's statement is, frankly speaking, more of a challenge to our race than anything else.

Unajua, Ndugu Bongolander, inashangaza jamii ya kimataifa, hakika, kuona watawala wa mataifa yaliyo maskini wakiwa matajiri wa kupindukia kuliko viongozi wa mataifa yaliyoendelea?
 
Plan ya jmk ya muda mrefu ni kuvua watu magamba na naona mtendaji wake nape ameshindwa kuhihubiri vizuri,mwaka wa sita huu maisha bora kwa mtzania yamekuwa bora maisha tu kwa mtanzania sukar,unga,mchele,mkate vipo juu naungana na botha aslimia 100
 
Namimi natoa kauli yangu " Usipokuwa na mtazamo wa 'Kibaguzi' huwezi ukafanya maamuzi sahihi au ya kimaendeleo' Mnasemaje
 

Hukubaliani na nini ndugu ? Kwani hao viongozi wa kiafrika wanapigiwa kura na wazungu au sisi waafrika wenyewe ? Wakijitokeza watu wenye sera safi munawapiga vita na kuwaita wadini.wakabila,wachochezi au wavurugaji wa muungano. . .
 

Kama si kweli, nioneshe nchi moja ya Kiafrika iliyofanya/inayofanya vizuri (nami nitakuonesha kondoo mwenye mwanya wa meno!)
 
Mi naona mchizi botha alikuwa sasa kabisa wala hakukosea. Kwani si ndo tulivyo!
 
Kwanza kitendo cha kuona uhalali katika kauli hiyo ni tatizo tofauti na tatizo na ujinga ulioko kwenye kauli hiyo,ni mtu mwenye ufahamu ulio chini sana kufikiri ngozi ya mtu ndo inamfanya kuwa bora,kama ni hivyo tunaweza kusema wazunguni wajinga kutokana na kauli ya mzungu huyo kwa sababu ya ngozi yake!
 
Kuna ukweli katika tamko la hayati Botha, kwani nchi za kiafrika zimeingia kwenye system ya mifumo ya kiutawala kwa kufuata au kuiga nchi ambazo historia yake ni zaidi ya miaka 200 iliyipita, na wana reference ya kutumia mabadiliko ya kihistoria katika katika nchi zao kufanikisha demokrasia. Afrika imetoka kwenye stone age na kuingia kwenye iron age. Lakini kabla iron age haijakaa vizuri mara tumeingizwa na wazungu kwenye mzunguko wa maendeleo yao ambayo yameua kabisa mtiririko wa maendeleo yetu.

Hali hata mifumo ya utawala imeadhirika kwa kukosa misingi toka awali kwa vile tumeingizwa mkenge mkenge tu kwenye mifumo ya demokrasia wakati jumuia zetu za kiafrika zilikuwa na mfumo wa kiutawala wa kichifu (kingdoms).

Hawa viongozi tulio nao ni wale waliotokea katika familia za mababu zetu zilizoathiriwa na tawala za kikoo, kichifu, ambazo watawaliwa walitakiwa kuzilisha familia za kitawala bila ubishi. Kinachoendelea sasa ndo historia inajieleza.

Mapinduzi ya kweli ni kizazi kipya, chenye kuanza kwa system mpya yenye chama kipya na hivyo kusuka mfumo sahihi wenye kulinda maslahi ya taifa na watu wake. Lakini CCM na watu wake itabaki kirithishana madaraka na hakuna kitakachobadilika zaidi ya kucheza na maneno kasi mpya, nguvu mpya, tumethubutu tunaweza na sasa tunasonga mbele,
wakati huo huo belt kwenye engine inapiga kelele kuonyesha dalili kwamba inaweza katika wakati wo wote na hivyo badilisha na kuweka belt mpya.
 
Candid Scope, upo ulivyo sio kwa sababu ulizaliwa ulivyo bali ni ulizaliwa wapi, nanani, nafursa zipi, mfumo upi na mgawanyo upi. Rangi ya ngozi yako haina uhusiano na akili yako ila rangi ya ngozi, dini yako,na tabaka ulilomo hutumika kuhalalisha mfumu uliopo.
 
Japo maneno yake ni ya kibaguzi, ila yana maana kubwa.
Maneno ya botha yana maana kubwa. Hebu angalia maendeleo ya watu weusi walio marekani ikilinganishwa na jamii nyingine. Ingawa kuna vikwazo kwa mtu mweusi enzi hizo lakini bado utaona jamii kutoka Asia zinaedelea sana kuliko jamii ya watu weusi. TZ tuna miaka 50 ya uhuru. Sehemu nyingine unashindwa kuelewa kama ni kwanini inaitwa Tanzania badala ya Deustch Ostafrka. Viongozi wetu hata mpaka majeshi wao ni rushwa na anasa. Vimwana na magari ya kifahari na mengine mengi ya hovyo. Utawala mbovu. Kujilimbikizia mali. Kung'ang'ania madaraka hata kuwa tayari kuua. Ni wakati wa kuwa na kizazi kipya cha uogozi. Kizazi kipya kigezo kiwe si umri bali tuwe na viongozi wenye fikra mpya na za kimaedeleo.
 
Maulaga nashukuru unaelewa hivyo, na ni wachache wanaoweza tazama kwenye kioo kusoma undani wa walivyo zaidi ya kuona tu kivuli chake kilivyo. Rangi si hoja nzito sana katika mtazamo wangu ingwa hii rangi inawakilishwa watu wa utamaduni na mtazamo fulani katika maisha yao.

Binadamu hatutofautiani katika akili, ndio maana hapo nyuma nimesema;
a mind is like a parachute, if you don't open it, it don't work. Akili nayo kuna mengi yanayochangia hadi iweze kufanya kazi vizuri, ila inategemeana na makandokando ya mtu, silika ya mtu, utamaduni wa mtu, malezi, nk.

Ideology ya waafrika wengi tangu mababu zetu mwenye mali ni kuoa wake wengi. Watawala ni kujichakulia vimwana anavyopenda, mwanamke kutokuwa na haki za msingi katika jamii ila ni chombo cha kumstarehesha mwanaume nk. Mambo kama hayo na mengine ndiyo aliyoyaona Botha, na tunashuhudia mambo yanavyokwenda na huhitaji kuambiwa kwa vile mwenye macho haambiwi tazama.

Athari za utamaduni wetu, mapokeo, yanatuweka katika hali hii na siyo akili. Elimu ya awali anayopata binadamu ni
informal education
ambayo inaambatana na kuona yanayoendelea katika jamii yake, familia yake na anakua katika mazingira hayo, kwa vyo vyote anaathirika na mazingira, mila na desturi za maisha ya wanaomzunguka.

Kwa bahati nzuri kizazi cha leo licha ya kupitia mazingira hayo, lakini wananafasi ya kufunguka zaidi akili zao na kujifunza njia bora zaidi ili kujenga jemii yenye misingi bora ya maisha na utamaduni endelevu kiuchumi. Hali hiyo inatokana na mwingiliano wa kimataifa na hivyo kubadilishana fikra na kuchuja yaliyo mabaya kuyaacha na kuendeleza mema na papo hapo kuiga mazuri toka nje.

Na hii tunapoongelea kizazi kipya hatuna maana ya vijana tu, ila ni pamoja na hata wenye umri mkubwa wenye upeo endelevu kijamii kutokana na kufunguka akili zao kama wengi wanavyotoa comments zao hapa, nakubaliana nao kwa sana tu. Kufikia hatua ya kuua raia kwa ajili ya kulinda maslahi binafsi ya watawala sikutegemea kisiwa cha amani tulichozoea kukiita Tanzania kigeuke kuwa madimbwi ya damu za watu wanaouawa kwa unyama na wenye uchu wa kuendeleza himaya yao ya madaraka.
 
surely the best post.....yani nikifikiria mambo anayowaza na kuyafanya mtu mweusi natamani kulia sijui ni nani ameturoga
Wachawi ni sisi wenyewe. tumeamua kuacha kutumia vichwa vyetu, sasa unafikiri itakuwaje. unajisikia vipi kama kiongozi mkubwa wa nchi anaongozwa na waganga wa kienyeji badala ya proper advisors?
Na hao waganga wanamshauri nini kama sio kuloga wenzake anaowaona tishio? na huo muda wa kufanya haya matakataka tunaufidia vipi?
 
Shida kubwa la viongozi wetu wa CDM wanamambo ya kitoto sana!!!!!!!!!!!yani nashindwa kuamini kabisa mtu kama MSIGWA anaweza nae akakomaa na mambo ya kitoto kama haya kwani akisema wewe ndio umeanzisha ni kinafuata....................??????????wewe ni mbunge na memba wa muda mrefu sana umo jf lakini cha ajabu una post ambazo hazizidi hata kumi,leo umeona SCOPE kaleta mada umekulupuka mishipa ya shingo imekutoka na kupigania mambo ya kitoto kabisa.
OK UMEANZISHA WEWE,WEWE NDIO MSHINDI!!!!!!!!!!KUBWA ZIMA OVYO!!!!!!!!!!wanajf ebu mpigieni makofi huyu kilaza wetu ili nae apate furaha hiyo anayotaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…