Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyu ndo zake hizo. Asubiri uteuziNamba ya simu unamwekea nani?
Naomba nikupe ufafanuzi kuwa katika hiyo miezi sita haimaanishi kuwa umeme hautakuwepo ,bali katika hiyo miezi sita ndipo patakuwa na utengenezaji wa mitambo yetu ili ifanye vyema zaidi kazi.lakini pia ndani ya hiyo miezi serikali yetu itaendelea kutumia vyanzo vingine vya umeme kama vile gas na jua, lakini baada ya hiyo miezi sita hakutakuwa tena na tatizo hili la kukatika kwa umeme kama sasa,kwa kuwa tutakuwa tumejiimarisha kama nchi kuwa na umeme wa kutosha na toshelezi kwa kutumia vyanzo mbalimbali tofauti na sasa tunapotegemea kwa kiasi kikubwa umeme wa maji ambao unakuwa ni changamoto panapokuwa na ukame kama ilivyo kwa sasa.Miezi sita...????Wafanyabiashara wanaohitaji umeme, hasahasa hawa wa uwezo wa kati na chini..hiyo miezu sita hali itakuwaje???
Mama awe makini sana na hao wanaomletea hizo taarifa...wafrika sio watu wa kuwaamini hata kidogo...hawakawii kukudidimiza....
Kwa hiyo kipindi cha mwandazake ukame haukupiga na hizo maintenance zilikua hazifanyiki....???
Kweli mpaka miaka hii bado tunaongelea umeme wa maji kweli na wakati tumejifunz ukame unavyosumbua??
Tanzania ya viwanda utawezekana kweli kwa stahili hii??
Hivi serikali haijaona umuhimu wa kuhamia seriously kwenye vyanzo vingine mpaka tuongelee maji miaka yote??
Hivi kama mpaka karne hii tunashindwa kutatua suala la umeme 100% tutaweza kweli ku-assemble achilia mbali kutengeneza magari, nguo, pikipiki...Tunamipango ya exploration na uwekezaji kwenye teknologia mpya kwa ajili ya vizazi vyetu??
Hivi sisi, tunaweza kitu gani aisee....Nyerere alijitahidi kaanzisha viwanda..karibia vyote vimepotea...Mama awe makini yaani atashtuka hata hayo ma-turbines watu wameng'oa na kupeleka kusikojulikana...
Serikali na viongozi wetu wako bizy sana...Vikao vya kutosha, uteuzi mwingi, semina nje ya nchi, watu wanabadirishana tu, vitengo na vyeo ni vya kutosha lkn hakuna mabadiriko yenye uhakika....Mfano mara huyo Ndugu Maharage katolewa TANESCO, kaenda TTCL, then Posta..hivi tunatarajia mabadiliko yoyote kweli??Na watanzania walio wengi hata hawafuatilii hayo mambo ni kama wamesusa..
Daah..tutafika tumechoka sana...
Mganga njaa ccm bila kujipendekeza upewi teuzi,ccm ina wenyewee na wenyewe ni kina Nape. Weka number ya baba na bubu zako utazeeka na njaa yako.Namba ya simu unamwekea nani?
Una njaa tena ile njaa mbaya sana ina maana gani kuweka number yako ya sim.Siyo kila mtu ana njaa kama ilivyo kwako.wengine Tunafanya kazi kwa uzalendo na siyo kwa malipo.
Ndio ndugu yangu watu wanamatumaini makubwa na Rais samia pale afunguapo kinywa chake wanatambua kuna Tumaini litakaloponya na kufariki mioyo yao wanakuwa Rais samia ni mkweli na mwenye hofu ya Mungu asiye tayari kuwalaghai watu kwa uongo.Ndio maana nikasema Ameleta matumaini kwa watu wengi sana kwamba hata wakiwa na changamoto wanajuwa akitamka neno mama yao watapata suluhisho na majibu ya kueleweka Ndio maana leo kiu ya watanzania imekatwa na Rais samia na Taifa linaendelea kuwa Tulivu na lenye amani kama iivyo kawaida yake.Mkuu sio wewe jana ulisema kwamba SAMIA amewatia watu matumaini ya maisha yao....
Leo unasema Hotuba imelituliza Taifa.....; Which means ulichosema jana kwamba Watu walikuwa na matumaini sio kweli sababu walikuwa hawajatulia ambapo wametulizwa leo....; Kwahio in short unachosema wala hakina mtiririko.... it does not add up
Mama Abdu angekuwa mzalendo angekuwa anateua Wazalendo kama wewe.Hapana mimi nafanya kazi kwa uzalendo na siyo kwa ajili ya kusaka uteuzi.sisi sote hatuwezi kuwa viongozi ,hivyo tusio viongozi tuna mchango kwa taifa letu.
Karibu kila Waziri mwenye dhamana ya Nishati anapotoa hotuba yake anaeleza kwamba ndani na miezi kadhaa tatizo la kukatika umeme na pia mgao wa umeme utabaki kuwa historia. Haya maneno tumeyasikia sana masikioni mwetu utadhani ni santuri ya muziki ambayo inajirudia kama kasuku aliyechoka. Wananchi wanachotaka ni umeme, haya mambo ya historia yatajulikana huko mbele ya safari.Kawadanganye watoto wa chekechea.
Inaelekea kuzuri sana.mahali ambapo kila mtanzania atapata milo mitatu bora na yenye virutubisho vyote mahali ambapo vijana wote watapata ajira bila shida.mahali ambapo Taifa letu litakuwa kapu la chakula kulisha Bara zima la Afrika,mahali ambapo wawekezaji na watalii watakuwa waapishana angani kuja kutalii na kuwekeza Tanzania,mahali ambapo kila mtu atakuwa na uhakika wa kutimiza ndoto yake kama ilivyo sasa,mahali ambapo barabara zote zitatandikwa lami na upanuzi wa barabara na hivyo kupunguza ajari za barabarani.Hii nchi inapoelekea.....
Macho ya mama yanaona na kutizama miaka mia mbele kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu.mama anamaono makubwa juu ya hili taifa
Kilimo unakijua wewe ..mwanaume mzima kutwa mtandaoni kutetea ujinga ujinga ..jitafakari real men hawezi kuwa chawa
Sent from my CPH2349 using JamiiForums mobile app
CHAWA.mwendazake alikuwa hafahamu maana ya "maintanance" ni nini.
Ndio maana serikali ya Rais samia imedhamiria kumpatia Mtanzania umeme wa uhakika na toshelezi.ndio maana inachukua hatua za kutumia vyanzo vingine vya umeme badala ya kutegemea maji pekee ambayo yanakuwa changamoto kipindi cha ukame kama ilivyo kwa sasa .Ndio maana Inaendelea na kasi ya ukamilishaji wa bwawa la mwalimu Nyerere ili lianze kazi mapema mwakani.Karibu kila Waziri mwenye dhamana ya Nishati anapotoa hotuba yake anaeleza kwamba ndani na miezi kadhaa tatizo la kukatika umeme na pia mgao wa umeme utabaki kuwa historia. Haya maneno tumeyasikia sana masikioni mwetu utadhani ni santuri ya muziki ambayo inajirudia kama kasuku aliyechoka. Wananchi wanachotaka ni umeme, haya mambo ya historia yatajulikana huko mbele ya safari.
Taarifa ya shirika la umeme nchini TANESCO imeeleza kuwa hali hii inatokana na kupungua kwa uzalishaji wa umeme wa maji kwenye vyanzo vya bwawa la Hale, Kihansi, Nyumba ya Mungu na Pangani kutoka MW 256 mpaka MW 34.