Hotuba ya Rais Samia yalituliza Taifa na Kukata kiu ya Watanzania juu ya changamoto ya umeme

Mkuu sio wewe jana ulisema kwamba SAMIA amewatia watu matumaini ya maisha yao....

Leo unasema Hotuba imelituliza Taifa.....; Which means ulichosema jana kwamba Watu walikuwa na matumaini sio kweli sababu walikuwa hawajatulia ambapo wametulizwa leo....; Kwahio in short unachosema wala hakina mtiririko.... it does not add up
 
Naomba nikupe ufafanuzi kuwa katika hiyo miezi sita haimaanishi kuwa umeme hautakuwepo ,bali katika hiyo miezi sita ndipo patakuwa na utengenezaji wa mitambo yetu ili ifanye vyema zaidi kazi.lakini pia ndani ya hiyo miezi serikali yetu itaendelea kutumia vyanzo vingine vya umeme kama vile gas na jua, lakini baada ya hiyo miezi sita hakutakuwa tena na tatizo hili la kukatika kwa umeme kama sasa,kwa kuwa tutakuwa tumejiimarisha kama nchi kuwa na umeme wa kutosha na toshelezi kwa kutumia vyanzo mbalimbali tofauti na sasa tunapotegemea kwa kiasi kikubwa umeme wa maji ambao unakuwa ni changamoto panapokuwa na ukame kama ilivyo kwa sasa.

Kwa hiyo hali itaendelea kuwa nzuri kila siku kunapokucha kutokana na mikakati ya serikali yetu katika kuliangazia Taifa letu mwanga muda wote.
 
Ndio ndugu yangu watu wanamatumaini makubwa na Rais samia pale afunguapo kinywa chake wanatambua kuna Tumaini litakaloponya na kufariki mioyo yao wanakuwa Rais samia ni mkweli na mwenye hofu ya Mungu asiye tayari kuwalaghai watu kwa uongo.Ndio maana nikasema Ameleta matumaini kwa watu wengi sana kwamba hata wakiwa na changamoto wanajuwa akitamka neno mama yao watapata suluhisho na majibu ya kueleweka Ndio maana leo kiu ya watanzania imekatwa na Rais samia na Taifa linaendelea kuwa Tulivu na lenye amani kama iivyo kawaida yake.
 
Kawadanganye watoto wa chekechea.
Karibu kila Waziri mwenye dhamana ya Nishati anapotoa hotuba yake anaeleza kwamba ndani na miezi kadhaa tatizo la kukatika umeme na pia mgao wa umeme utabaki kuwa historia. Haya maneno tumeyasikia sana masikioni mwetu utadhani ni santuri ya muziki ambayo inajirudia kama kasuku aliyechoka. Wananchi wanachotaka ni umeme, haya mambo ya historia yatajulikana huko mbele ya safari.
 
Hii nchi inapoelekea.....
Inaelekea kuzuri sana.mahali ambapo kila mtanzania atapata milo mitatu bora na yenye virutubisho vyote mahali ambapo vijana wote watapata ajira bila shida.mahali ambapo Taifa letu litakuwa kapu la chakula kulisha Bara zima la Afrika,mahali ambapo wawekezaji na watalii watakuwa waapishana angani kuja kutalii na kuwekeza Tanzania,mahali ambapo kila mtu atakuwa na uhakika wa kutimiza ndoto yake kama ilivyo sasa,mahali ambapo barabara zote zitatandikwa lami na upanuzi wa barabara na hivyo kupunguza ajari za barabarani.
 
Kilimo unakijua wewe ..mwanaume mzima kutwa mtandaoni kutetea ujinga ujinga ..jitafakari real men hawezi kuwa chawa

Sent from my CPH2349 using JamiiForums mobile app

Alafu usikute hili jamaa ni dingi na lina wajukuu. Hii nchi ina midingi inayozeeka vibaya sana.
Watu wameingia hasara kwa ajili ya mgao alafu analeta upumbavu kwenye mambo sensitive.
 
Via Yetu kaja kivingine huyu chawa
 
Official Statement ya TANESCO mwaka Jana.

07 Septemba 2022

Ni kweli kumekuwepo uhaba wa mvua uliojitokeza kwenye maeneo mengi ya nchi yetu kwenye miezi ya hivi karibuni, uhaba huu umesababisha kuwepo kwa upungufu wa kina cha maji kwenye mabwawa ya kufua umeme kwa kutumia maji hivyo kuathiri hali ya uzalishaji wa umeme kwenye baadhi ya vyanzo vinavyotumia maji.

Aidha, ili kuhakikisha kuwa utoaji wa huduma ya umeme inaimarishwa nchini, Shirika limeshachukua hatua mbalimbali za muda mfupi na za muda mrefu kama ifuatavyo;

Mipango ya muda mfupi

Kuanzisha kituo cha kuzalisha umeme kwa njia ya Gesi asilia cha Ubungo III ambacho kimeshakamilika na kuingiza jumla ya Megawati 112 za umeme kwenye Gridi ya Taifa tangu mwanzoni mwa mwaka 2022.

Kuanzisha kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia Gesi asilia cha Kinyerezi I Extension kitakachozalisha jumla ya megawati 185.

Tayari megawati 45 zimeshaingizwa kwenye Gridi ya Taifa na megawati zilizobakia zitaingizwa kwenye Gridi ya Taifa hadi kufikia mwanzoni mwa mwaka ujao.

Mradi wa kufua umeme wa Rusumo kwa kutumia maji.
Mradi huu unaozihusisha nchi tatu (Tanzania, Rwanda na Burundi) utakapokamilika, unategemewa kufua jumla ya megawati 80 za umeme, ambapo kwa upande wa Tanzania, tutapata megawati 27 za umeme zitakazoingizwa kwenye Gridi ya Taifa.

Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya jua wa Kishapu, Shinyanga.
Mradi huu unategemewa kuanza ujenzi wake Novemba 2022 na kukamilika Disemba 2023, utaingiza jumla ya megawati 150 za umeme kwenye Gridi ya Taifa.

Mradi wa kupeleka Gridi ya Taifa kwenye wilaya za mkoa wa Kigoma.
Tayari umeme wa Gridi ya Taifa umeshapelekwa kwenye wilaya ya Kibondo.
Serikali imeanza kuokoa jumla ya Tsh.9.44 bilioni kwa mwaka zilizokuwa zikitumika kununulia mafuta ya dizeli na kutengeneza mitambo (jenereta).
Mpango uliopo ni kuufikisha umme wa Gridi ya Taifa kwenye Wilaya ya Kasulu hadi Kigoma mjini kabla ya mwisho wa mwaka huu wa 2022 kufika.

Mipango ya muda mrefu

Mradi wa kufua umeme kwa kutumia maji wa bwawa la Julius Nyerere (JNHPP).

Mradi huu umefikia asilimia 71 ya utekelezaji wake.
Mradi utakapokamilika mnamo mwezi Juni 2024, unategemewa kuingiza megawati 2115 za umeme kwenye Gridi ya Taifa.


Kwa hatua hizi Shirika ilizozichuka zimesaidia kuimarisha hali ya upatikanaji umeme nchini na iwapo jitihada hizi zisingechukuliwa, basi ya upatikanaji umeme nchini kwa sasa ingekuwa ipo vibaya zaidi.

Sasa basi kama kuna sehemu walikosea watoe Tamko tuelewe kwamba walikosea na kumtaka Radhi SSH kwa kumpa taarifa za Uongo au kwa kutoa Taarifa za Uongo Wizarani. Someone and Somebody should be accountable and responsible. Kufanyike tathmini ya hasara zilizopatikana kutoka kwa watumiaji umeme nchini kutokana na Uzembe, Uhujumu na Rushwa zilizotokea...
 
Ndio maana serikali ya Rais samia imedhamiria kumpatia Mtanzania umeme wa uhakika na toshelezi.ndio maana inachukua hatua za kutumia vyanzo vingine vya umeme badala ya kutegemea maji pekee ambayo yanakuwa changamoto kipindi cha ukame kama ilivyo kwa sasa .Ndio maana Inaendelea na kasi ya ukamilishaji wa bwawa la mwalimu Nyerere ili lianze kazi mapema mwakani.
 
Magufuli Toka March 2021 hayupo
Ajabu bado amekuwa chaka la watu kujifichia!
Wewe Mama muogope Mungu,pambana kivyako bila kujifichia kwenye kichaka cha JPM.
 
Taarifa ya shirika la umeme nchini TANESCO imeeleza kuwa hali hii inatokana na kupungua kwa uzalishaji wa umeme wa maji kwenye vyanzo vya bwawa la Hale, Kihansi, Nyumba ya Mungu na Pangani kutoka MW 256 mpaka MW 34.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…