View attachment 1472025
BAADHI YA ALIYOYAONGEA:
- Naamini ninazo sifa zote shahiki za kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
- Nikipewa nafasi hii na kuchaguliwa, sitolipiza visasi kwa yote yaliyofanywa na walionitangulia. Nitatafuta muafaka wa kitaifa
- Nikipewa nafasi ya kugombea urais na nikashinda, nitahakikisha mihimili ya Dola inakuwa huru
- Uamuzi wa Ndugai kunifutia ubunge haujaniondolea sifa za kuwa mgombea Urais. Aidha, sijawahi kuwa na mashtaka ya aina yoyote yanayoniondolea sifa za kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa Tanzania
- Amesema akipata dhamana ya kuongoza, Serikali haitatumia Vyombo vya Dola dhidi ya Wapinzani na Wanahabari
- Atakuwa mfariji Mkuu, hatakimbilia kijijini kwao wakati wa majanga kama tetemeko au #COVID19