Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Lissu ni mtu mweye akili sana hasa kwenye nyaja ya sheria; ila alipoingia kwenye siasa, alitumia mlango mbaya sana uliokuwa unaongozwa na hasira, na hivyo akakosa element yoyote ya compromise, ambayo ni ya muhimu sana kwenye siasa. Akaendesha siasa za Ben Mtobwa: Ama zao ama zangu, which doesn't work. Namwonea huruma sana hasa kwa vile bado ana watoto wadogo wa kulea ambao sijui sasa hivi anawatunzaje; nimeona picha ya mtoto aliyochora ama kindergarten au elementary school, na huenda anawalipia kwa michango ya wenye huruma, ambayo inaweza kuwa na effect kwenye prestige yake. Alichokosea Lissu, Zitto na Mbowe ni kuwa ni vizuri siku zotekwenye siasa kuongea vizuri na aliyeshika mpini hata kama hamkubaliani kwenye sera; na kumkosoa kisera siyo lazima umtukane. Wakati wa Operation Thunderbelt ya kuokowa waisralei waliokuwa wameshikiliwa Entebbe, Waziri mkuu wa Israel pamoja na kiongozi wa upinzani walikubaliana hata kabla mada ile haijaenda kwenye bunge; waziri mkuu yule asingemuita kiongozi wa upinzani kuzungumza naye kama angekuwa anajua kuwa atakaidi tu na kutoa matusi