So Mungu anaruhusu uovu utokee duniani?
Mungu amempa mwanadamu uchaguzi huru kati ya giza(shetani au nuru(Mungu)
Aliyeleta uovu ni shetani si Mungu, mwanadamu anafanya on his/her own emwill.
Warumi 1 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²⁸ Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
²⁹ Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,
³⁰ wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao,
³¹ wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema;
³² ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.
“ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.
”
— 2 Wakorintho 4:4 (Biblia Takatifu)
Kwa maandiko haya utagungu zipo sheria 2 zinakinzana, yenye nguvu ndiyo inayotawala vyote automatic. Mnyukano wa sheria hizi mbili ndizo zinamfanya Mwanadamu afanye uovu kama roho ya shetani ilivyo au afanye mema kama roho ya Mungu ilivyo.
Warumi 8 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
² Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.