Hujuma kubwa ajira za Serikali ya wanyonge

Hujuma kubwa ajira za Serikali ya wanyonge

Nachokizungumza hapa nina uhakika nacho asilimia 100% naombeni msinichukulie kama nalalia mlango wazi bahati za wengine.

Kwanini mimi mwenye GPA ya 4.5 ya UDSM sijapangiwa shule japokuwa nina uwezo mzuri wa kufundisha?

Huu ni mwaka wa pili nimekaa mtaani. Sawa, sijajitolea. Hebu fikirieni ningewezaje kwenda shule km. 5 kila siku nakurudi wakati sijui nitakula nini? na wazazi wanataka niwasaidie kazi za shamba kufidishia pesa nilizowagharimu kunisomesha?

Sawa, mmeangalia wale wenye miaka mingi, mbona mmemwajiri mwenyekiti wa UV CCM, katibu na Mhazini waliomaliza vyuo mwaka 2019 udsm na matawi yake yote? Na wakati tunajua wengine walikuwa na carry over karibia miaka yote?

Sawa, tuachane na kada ya ualimu. Mbona JKT mpwa wa general X mmempangia ajira JW na wakati hakuwa na sifa. Maana hakujenga ukuta wala nini. Na amewaacha Ma-service man aliyowakuta? Hii ndio Tanzania ya wanyonge?

Haki ya nani siwashitaki popote pale...lazima nichukue hatua mwenyewe na Mungu wangu.
Mitano Tena Mkuu.
 
Wewe kama unashabikia CCM ni umbwa kama umbwa zingine!
 
Mkuu pole sana kwa hoja nzito. Ila ukweli ni kwamba ajira zinazotolewa ni chache mno ukilinganisha na uhitaji kwenye shule za msingi pamoja na sayansi, hisabati na ufundi kwa sekondari. Walimu wanaostaafu ni wengi sana lakini walau tu hata kujaza hizo nafasi za wastaafu imeshindikana. Sasa na hapo tusemeje? Vyeti feki na watumishi hewa vipi. Zile idadi hadi leo nafikiri bado hazijajazwa. Hivi kweli kwa mtindo huu tutafika wapi?
Wakuu wanadai kuwa tujiajiri! Sawa ni wazo zuri ila kwa mtaji upi na soko gani? Hili la kuuza debe la mahindi kg 20 kwa sh. 6000 ili ununue mbegu kg 2 kwa sh. 13000, serious kabisa. Kweli namba tutaisoma kwa mda mrefu zaidi kuliko tunavyotarajia. Mtu ameshindwa kujaza nafasi za wastaafu halafu useme atatoa ajira mpya!
 
Mkuu Nina elimu ya form six Ila now Niko zangu BOT nakulaa mpunga mrefu sanaa....pole John kisomo.kusoma sio kukariri makaratasi Ni kupata ujuzi.naakika naiyo unaita GPA yako ukija lazima nikufundishe kazi maana hujui chochote
 
Kwanza kabisa naomba nikupe pole kwa kipindi kigumu unachopitia na pili naomba ufahamu kuwa na GPA kubwa tu haitoshi wewe kupata kazi kirahisi cha msingi tafuta connection .wengi tuna historia kama zako za kupata ma GPA makubwa pengine zaidi ya hiyo yako lakin baada ya kutambua maisha ni zaidi ya GPA ndo tukaingia kutafuta connection na pia nikutoe wasiwasi kidogo ipo siku na ww utapata usijali kabsaa

Na mfano mmoja hai kabisa kuna mwana tumesoma nae uwezo wake mdogo na sup zilikuwa kawaida kwake ilaa siku tumehudhuria usaili ni yeye tu alipata ilee kazi nzuri na kutuacha wengi na wengine wenye vyeti vizur.

Pole sana tulia omba mungu ipo siku yako na ww utapata unacho stahili dunian hapa hakuna usawa na pia hakuna aliyekuja kwa bahati mbaya ipo siku narudia ipo siku mungu atatenda upande wako na utasahau haya yote ya kujiona una bahati mbaya

Ahsante ....ipende nchi yako kuwa mzalendo .

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom