Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
Hata kama huendi wanakublock wakigundua uko kinyume nao. RC PM alizuiliwa.Amekwambia ana mpango wa kwenda kwenye nchi zao?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata kama huendi wanakublock wakigundua uko kinyume nao. RC PM alizuiliwa.Amekwambia ana mpango wa kwenda kwenye nchi zao?
Kama hana mpango wa kwenda hata wakim-block ni kazi bure.Hata kama huendi wanakublock wakigundua uko kinyume nao. RC PM alizuiliwa.
Kweli kabisa,Pole pole hii ni mara ya tatu nakusihi, mlio karibu naye mumkumbushe umuhimu wa kunyamaza kimya, hebu akumbuke yaliyofanywa kwa Membe kama yalikuwa sahihi, na yeye alikuwa miongoni mwa watoa maamuzi. Zama zimepita atulie tuu.
Hi guys. Hope mnado poa.
Kuna page imeandika kuwa bwana Polepole atajitoa chamani wakishirikina na taasisi 2.
Hii ni nyepesi nyepesi.
At Calvary.
====
Taarifa kwa Vyombo vya Habari.
Jumamosi tarehe 11, Disemba 2021 saa 5:00 Asubuhi nitazungumza na Wanahabari pamoja na Mambo mengine nitazungumzia Shule ya Uongozi | The Leadership School. Mahali - Ofisi za Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC).
-Ujamaa ni Imani-
View attachment 2039936View attachment 2039938
=====
UPDATES;
======
View attachment 2040626
"Kama viongozi wasiposali na kumtemea Mungu nchi yetu haiwezi kuendelea, tumtangulize Mungu mbele. Kuanzia diwani, mpaka mawaziri na kule juu tuwe watu wa maombi, kukumbushana ni muhimu, naona kama tunatakiwa tuishi maisha ya Kimungu hivi." - Humphrey Polepole
"Viongozi wanatakiwa wawe waadilifu na wanyenyekevu." - Humphrey Polepole.
"Nilisema kuhusu magonjwa, mfano ebola, kesi moja tu imewahi kupenya na ikafuatiliwa na sasa tuko salama. Yakaja haya magonjwa mengine maarufu hivi karibuni lakini sio kitu. Nikasema muwe makini hawa wahuni wa kimataifa ni wajanja." - Humphrey Polepole.
"Nilizungumza kuhusu songombingo la wamachinga, Mhe. Rais Samia Suluhu alitoa maelekezo mazuri sana lakini wapo waliotekeleza vizuri wengine wamefanya vibaya mno, wameboronga, ukimkosoa DC au RC kuhusu hili wanasema umemkosoa Rais, nani kakwambia?" - Humphrey Polepole.
"Rais Samia Suluhu alitoa maelekezo mazuri sana kuhusu wamachinga, wapangeni vizuri, msiwazonge, msiwapige, msiwanyanyase.... mimi ni mwana-CCM bana, fitina kwangu ni mwiko. Nikasema mlivyotenda kwa machinga baadhi yenu mmekosea na nikatoa mifano." - Humphrey Polepole.
"Kwenye mgongano wa kimasilahi kuna aina tatu, masilahi ya Taifa, kundi au mtu mmoja mmoja, wanaanza na masilani ya mtu mmoja, kisha kundi na baadaye Taifa, nikasema wanaopanga hivi ni wahuni." - Humphrey Polepole.
"Wahuni wanapenda masilahi binafsi kwanza, kazi yetu ni kuwadhibiti bila huruma wala kucheka nao. Yanatokea majitu tena viongozi na kusema mimi ni muhuni nimepenya, unaweza kutafakari namna gani kiongozi huyu yuko serious, huwezi kuwa kiongozi ukachekelea kuwa mhuni." -Polepole.
"Kule bungeni tunakutana mara chache, mfano kuna kipindi cha mwezi Machi hadi Julai, ina maana mimi niongee mara nne tu kwa mwaka kuhusu wahuni, unadhani inatosha, nitatumia fursa zozote za kusema ili kuwasema wahuni," - @hpolepole, Mbunge wa kuteuliwa.
"Kwa sasa nimeshaanza kufuatilia mambo kadhaa, watu wakizingua pahala ninatoka ninasema hapa umezingua nitaruka na wewe, nakulipua, si wanachelewa kuchukua hatua? - Humphrey Polepole.
"Sijasema Serikali haifanyi kazi, Serikali inafanya kazi nzuri sana lakini ni jukumu letu na kukumbushana. Unadhani kwa nini malaria haiishi na tumesoma mpaka madarasa tukayamaliza? Halafu tunasema tu lete net, hivyo viwanda wanatengeneza wapi?, vya msaada. - Humphrey Polepole.
"Nilieleza kuhusu uchambuzi wa matatizo, malaria haiishi Tanzania kwa sababu hatuchambui tatizo, unadhani ufumbuzi ni chandarua kwani ukitoka usiku kwenda haja ndogo mbu si wanaunga na wewe? tunafanya maamuzi ambayo hayajajengwa katika kutatua tatizo, hilo nalo tatizo." -Polepole
"Kuna kiwanda kipo hapa nchini kinatengeneza viuatilifu vya kuua mazalia ya mbu, nyie wanahabari waulizeni wamewahi kunnuua pale? Mtu analala kwenye chandarua mguu upo nje, mbu wanamng'ata, nauliza sisi tumekwenda shule tukasoma, hii ndio suluhisho kweli?" - Humphrey Polepole.
"Nilizungumza kuhusu deni la taifa, kuna watu wengine ni wabunge wakaibuka wanasema ooh deni limekuuwa kubwa, zito linamuelea mama. Nikatoka nikasema ukweli wasipotoshe, ni uongo. Si viongozi wote tupo kwa nini mwenzetu anapotosha na hatutoki kusema? kimya. -Humprhey Polepole.
"Sijui kwa nini viongozi wanaogopa kusema, sijui wanaogopa, kwa sababu deni linalosemwa viongozi wote walikuwepo, niweke sawa watu wasielewe tofauti. Kwa nini wenzetu msitoke mkasema, au mpaka watu wachanganyikiwe, penye ukweli lazima tuseme ukweli? - Humphrey Polepole.
"Juzi Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ndiye amekuwa mtu wa kwanza kutoka na kusema deni la Taifa ni himilivu, na yeye amejiongeza tu baada ya kuona kimya." - Humphrey Polepole.
"Sijazungumzia mtu, mbunge, mamlaka ya nchi wala mjomba wake mtu lakini baadhi ya viongozi wamechukia, kwa nini unaongea? Hivi imefika pahala tunaulizana kwa nini umeongea, Mungu amenipa mdomo unataka nifanye nini? Kuna kula na kuongea. - Humphrey Polepole.
"Nilipofanya Shule ya Uongozi nikapigiwa simu na watu wanaambiwa acha kwanza, nikauliza kwa nini? hakuna majibu. Nimefanya kazi na Mzee Mkapa, Kikwete, Magufuli na Mama Samia, hawa viongozi wangu wote hawajawahi kuniambia 'kaa kimya', nawashangaa wanaotaka ninyamaze." - Polepole.
"Mwalimu Nyerere alisema 'hoja ahipigwi rungu, inajibiwa kwa hoja bora zaidi', mimi ni mwana-CCM ninawaambia hapa kuna tatizo linarekebishika hivi, unasema kaa kimya, hilo ni jibu la hoja nilililoitoa." - Humphrey Polepole.
"Niliitwa kwenye chama kwa tuhuma, nilizijibu zote moja baada ya nyingine, siwezi kusema, chama kitakuja kuzungumza." - Humphrey Polepole.
"Nimeitwa TCRA, wanasema nimetoa maudhui ya kupotosha umma yanayoweza kuchochea Watanzania kugomea na kudhoofisha kampeni ya Kitaifa kujikinga na Corona. Hivi mimi nimeshawahi kuwaambia tudhoofishe kampeni ya kujikinga na corona? hawa wanataka kunichomeka hapa" -Humphrey Polepole
"Sijawahi kusema kwa nini sichanji, sasa tusisukumane nikafafanua kwa nini sikutaka kuchanja. Sasa nitakwenda TCRA kupeleka utetezi wangu nikaseme ukweli maana tunatafutana kwenye korido la corona." - Humphrey Polepole.
"Hii hoja ya wamachinga nasema kweli mmeonea watu, halafu mtu anasema kaa kimya, kumbe jukumu la mbunge ni nini? Sauti ya watu ni ipi? Hii kaa kimya nimehangaika nayo sana, nimefanya tu kiubishi." - Humphrey Polepole.
"TCRA wanasema wamenipa leseni kwa ajili ya maudhui ya kipindi cha Papo kwa Hapo, wanahoji kwa nini ninafanya Shule ya Uongozi... hivi mimi nimekulipa milioni ile halafu unanipangia cha kuzungumza? naweza kuposti familia yangu au mbwa wangu, utaniuliza?" - Humphrey Polepole.
"Kuhusu corona kuna ubishi wa kidunia, kila mtu ana upande wake, na mimi niweke wazi nipo kwenye ubishi huo. Mpaka Yesu atarudi tunaendelea na ubishi," Humphrey Polepole.
"Suala la machinga wanasema nimesema uongo, tena kwenye hilo nitasema na mengine ambayo sikutaka kusema, nina ushahidi, nimepeleka watafiti wilaya zote za Dar es Salaam, mtu amehamishwa na kupelekwa kwenye karo la choo, hivi Mhe. Rais aliwatuma hivyo?" - Humphrey Polepole.
"Kuna watu wanasema Polpole anajitoa CCM anakwenda kuanzisha chama chake, nataka niwaambie niliingia CCm kwa hiari mwaka 2000 nikapiga kura kwa mara ya kwanza, sitatoka CCM kwa hiari. Kama ninatoka CCM washike wanitupe nje, bado tupo sana hapa." - Polepole.
Mbunge wa Kuteuliwa (CCM),Humphrey Polepole amesema amepokea Mashtaka ya TCRA yanayosema kupitia Kipindi chake cha Shule ya Uongozi, amerusha Maudhui yanayopotosha Umma na yanayoweza kuchochea Watanzania kuweza kugomea Kampeni ya Kitaifa ya #COVID19
Akizungumza leo amesema, "Hivi mimi nimewahi kuwaambia ninyi tudhoofishe Kampeni ya Corona? Wapi niliwaambia kwa maana hiyo?"
Amesema kwasababu amepewa nafasi ya kujibu, atapelekea Utetezi wake aliodai unajitosheleza
#JamiiForums #UVIKO3
"...ukweli wa siasa za nyakati hizi"?Wanaokataa kuwa tawi la CCM wanavyohangaishwa?
😂😂😂😂
Natamani ungeujua ukweli wa siasa za nyakati Hizi👣👣👣👣
KARMA !!Laana hiyo itasumbua mpaka vizazi vyako na bado utazidi kuhangaika tu.
He is underdog!Nadhani slow slow anatafuta namna ya kutoka kwa vile hana cha kupoteza na hana future tena kwenye siasa maana alipata vyeo kwa kuteuliwa sio kupambania.
Kweli, ni kama vile amedata, na pia anahisi hayupo salama, depression hiyo !!Binadamu ni kiumbe ghali sana kupata kuumbwa, haiwezekani Mungu atulie amuumbe mwanadamu halafu mwingine ujitokeze umpoteze Tu kiboya....hapo hajiamini, na hivyo CCM hawamjibu wala kumuita anahisi uhai wake upo rehani na yeye atapotezwa....anaitisha hivyo vipress Ili kutafuta ulinzi WA macho ya watu.
Huyu kwa kifupi ni kadata, Ila asipewe dawa Ili aropoke yote walivokuwa wakiyafanya.
Kukaa CCM lazima ukubali #Stockholm-Syndrome.Haka kajamaa ni ka tapeli, ni ka seasonal politician. Wakati wa Mchakato wa Katiba kalikuwa kanisimamia itikadi za kupunguza ukiritimba wa chama kimoja, leo kinasema UJAMAA ni Imani. au hakijui ujamaa na siasa za chama kimoja ni chanda na pete?
Hahahaaaa......The same boiling water that hardens the eggs softens the potatoes.Mzee wa Mavieite , tulimuonya sana kuhusu uharamia wa awamu ya 5 lakini akatupuuza
The sun that melts the ice but hardens the soil.Hahahaaaa......The same boiling water that hardens the eggs softens the potatoes.
Chora 7 wacha manenooooo.You are allright, nilijua uwezo wa kufikiri utakufikisha hapa. Jina lako ni kama akili yako.
Sasa mtu kama wewe na genge lako utakuwa kiongozi sahihi kwa Watanganyika?
Vipi inaweza kuwalinda watoto wetu, vijana wetu, kuwapa elimu sahihi, maadili, uaminifu, uadilifu kujiamini.
Tena sana tu,Kwa hiyo unakiri polepole ni ndumilakuwili kama lowasa au membe?
Chora 7 wacha manenooooo.
Hi guys. Hope mnado poa.
Kuna page imeandika kuwa bwana Polepole atajitoa chamani wakishirikina na taasisi 2.
Hii ni nyepesi nyepesi.
At Calvary.
====
Taarifa kwa Vyombo vya Habari.
Jumamosi tarehe 11, Disemba 2021 saa 5:00 Asubuhi nitazungumza na Wanahabari pamoja na Mambo mengine nitazungumzia Shule ya Uongozi | The Leadership School. Mahali - Ofisi za Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC).
-Ujamaa ni Imani-
View attachment 2039936View attachment 2039938
=====
UPDATES;
======
"Kama viongozi wasiposali na kumtemea Mungu nchi yetu haiwezi kuendelea, tumtangulize Mungu mbele. Kuanzia diwani, mpaka mawaziri na kule juu tuwe watu wa maombi, kukumbushana ni muhimu, naona kama tunatakiwa tuishi maisha ya Kimungu hivi." - Humphrey Polepole
"Viongozi wanatakiwa wawe waadilifu na wanyenyekevu." - Humphrey Polepole.
"Nilisema kuhusu magonjwa, mfano ebola, kesi moja tu imewahi kupenya na ikafuatiliwa na sasa tuko salama. Yakaja haya magonjwa mengine maarufu hivi karibuni lakini sio kitu. Nikasema muwe makini hawa wahuni wa kimataifa ni wajanja." - Humphrey Polepole.
"Nilizungumza kuhusu songombingo la wamachinga, Mhe. Rais Samia Suluhu alitoa maelekezo mazuri sana lakini wapo waliotekeleza vizuri wengine wamefanya vibaya mno, wameboronga, ukimkosoa DC au RC kuhusu hili wanasema umemkosoa Rais, nani kakwambia?" - Humphrey Polepole.
"Rais Samia Suluhu alitoa maelekezo mazuri sana kuhusu wamachinga, wapangeni vizuri, msiwazonge, msiwapige, msiwanyanyase.... mimi ni mwana-CCM bana, fitina kwangu ni mwiko. Nikasema mlivyotenda kwa machinga baadhi yenu mmekosea na nikatoa mifano." - Humphrey Polepole.
"Kwenye mgongano wa kimasilahi kuna aina tatu, masilahi ya Taifa, kundi au mtu mmoja mmoja, wanaanza na masilani ya mtu mmoja, kisha kundi na baadaye Taifa, nikasema wanaopanga hivi ni wahuni." - Humphrey Polepole.
"Wahuni wanapenda masilahi binafsi kwanza, kazi yetu ni kuwadhibiti bila huruma wala kucheka nao. Yanatokea majitu tena viongozi na kusema mimi ni muhuni nimepenya, unaweza kutafakari namna gani kiongozi huyu yuko serious, huwezi kuwa kiongozi ukachekelea kuwa mhuni." -Polepole.
"Kule bungeni tunakutana mara chache, mfano kuna kipindi cha mwezi Machi hadi Julai, ina maana mimi niongee mara nne tu kwa mwaka kuhusu wahuni, unadhani inatosha, nitatumia fursa zozote za kusema ili kuwasema wahuni," - @hpolepole, Mbunge wa kuteuliwa.
"Kwa sasa nimeshaanza kufuatilia mambo kadhaa, watu wakizingua pahala ninatoka ninasema hapa umezingua nitaruka na wewe, nakulipua, si wanachelewa kuchukua hatua? - Humphrey Polepole.
"Sijasema Serikali haifanyi kazi, Serikali inafanya kazi nzuri sana lakini ni jukumu letu na kukumbushana. Unadhani kwa nini malaria haiishi na tumesoma mpaka madarasa tukayamaliza? Halafu tunasema tu lete net, hivyo viwanda wanatengeneza wapi?, vya msaada. - Humphrey Polepole.
"Nilieleza kuhusu uchambuzi wa matatizo, malaria haiishi Tanzania kwa sababu hatuchambui tatizo, unadhani ufumbuzi ni chandarua kwani ukitoka usiku kwenda haja ndogo mbu si wanaunga na wewe? tunafanya maamuzi ambayo hayajajengwa katika kutatua tatizo, hilo nalo tatizo." -Polepole
"Kuna kiwanda kipo hapa nchini kinatengeneza viuatilifu vya kuua mazalia ya mbu, nyie wanahabari waulizeni wamewahi kunnuua pale? Mtu analala kwenye chandarua mguu upo nje, mbu wanamng'ata, nauliza sisi tumekwenda shule tukasoma, hii ndio suluhisho kweli?" - Humphrey Polepole.
"Nilizungumza kuhusu deni la taifa, kuna watu wengine ni wabunge wakaibuka wanasema ooh deni limekuuwa kubwa, zito linamuelea mama. Nikatoka nikasema ukweli wasipotoshe, ni uongo. Si viongozi wote tupo kwa nini mwenzetu anapotosha na hatutoki kusema? kimya. -Humprhey Polepole.
"Sijui kwa nini viongozi wanaogopa kusema, sijui wanaogopa, kwa sababu deni linalosemwa viongozi wote walikuwepo, niweke sawa watu wasielewe tofauti. Kwa nini wenzetu msitoke mkasema, au mpaka watu wachanganyikiwe, penye ukweli lazima tuseme ukweli? - Humphrey Polepole.
"Juzi Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ndiye amekuwa mtu wa kwanza kutoka na kusema deni la Taifa ni himilivu, na yeye amejiongeza tu baada ya kuona kimya." - Humphrey Polepole.
"Sijazungumzia mtu, mbunge, mamlaka ya nchi wala mjomba wake mtu lakini baadhi ya viongozi wamechukia, kwa nini unaongea? Hivi imefika pahala tunaulizana kwa nini umeongea, Mungu amenipa mdomo unataka nifanye nini? Kuna kula na kuongea. - Humphrey Polepole.
Huyu Mpuuzi angekaa kimya tu kama ambavyo maj.uha wenzake wanavyomshauri.
Kwanza ahame aende wapi? Wakati yeye ndie alikuwa dalali kununua wapinzani?Polepole anawawakilisha mazuzu wenzake kama wewe.