Humprey Polepole atachanja au hatochanja atakapokwenda kuwa Balozi Malawi?

Humprey Polepole atachanja au hatochanja atakapokwenda kuwa Balozi Malawi?

Jamaa wana style nyingi sana za kukufunga mdomo wakihisi ni threat kwao.

Wanaweza kukuvuta karibu kama alivyofanya kwa kina Lukuvi na Kabudi, au wakakupeleka mbali kama walivyofanya kwa Polepole, uoga unamtesa sana mama yao.

Polepole bora astaafu siasa akawe mwalimu wa shule yake ya siasa, au wampeleke kwenye chuo chao walichoanzisha akawe mkufunzi japo sidhani kwa itikadi zake kama watampokea.
Polepole ni mjamaa kule wanafundisha ujamaa?
 
Kitendo cha Rais wa Tanzania, Samia Suluhu kumteua Humphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi kimewashangaza wengi, kwa kuwa ni kama haikutegemewa hata kidogo...
Slow slow asikubali huo teuzi

Bi. Mikopo ana kinyongo naye, kama Bi. Mikopo asingelikuwa na kinyongo juu yake wala haya yaliyofanyika yasingefanyika

Akienda huko kwa kukubali kuachia nafasi aliyonayo sasa, afahamu kwamba huko ng'ambo watamvumilia kwa mwaka kisha watamtema

Na akienda anaweza kuishi maisha magumu sana yakutopewa ushirikiano na nchi yake, kutopewa fedha za uendeshaji wa ofisi (OC), nakadhalika


Slow slow makinika!
 
Jamaa wana style nyingi sana za kukufunga mdomo wakihisi ni threat kwao...
Polepole hakuwahi kufikiriwa kufungwa mdomo, na hakuwahi kuwa stress kwa serikali, Upendo tu wa mama ndio umempaisha na kufikia hadhi ya balozi ambayo ni kubwa kuliko Ubunge tena wa kuteuliwa, RAISI ameonyesha ana nia thabiti ya kutokuacha alama ya uwakilishi kwa wananchi,
Tumuunge mkono mama
Kotapini
Kuingia kwa nyundo kutoka kwa nyundo
 
Jamaa wana style nyingi sana za kukufunga mdomo wakihisi ni threat kwao...
Kilichomuharibia credibility yake ni kufunga mdomo na kujisahaulisha aliyowahi kuyapigia kelele kabla hajasogezwa jikoni na JPM, ila ukiamua kuzungumzia uwezo wake wa kiakili utamfananisha na wachache sana pale CCM.

UKUFUNZI ni kitu anachokiweza kwa asilimia 95 au zaidi (kipaji), sema itikadi zake tu.
 
Kwenye habari kama hizi huwezi kumkosa STIVE NYERERE.
 
KAZI KAZI KWELI AMA UCHANJE AU UKOSE UTEUZI😂😂😂

Binafsi ningekuwa Polepole ningesimamia ninachokiamini.
Hajawahi kuwa na msimamo, ni tumbo lake tu... sasa kwa kumvua ubunge njaa itaamua....
 
Hadi 2024 safi ya jiwe itakua imeweka viti vya nyuma, ikisubiri wanafunzi wa mbele wamalize kupewa pipi
 
Wajamaa hawachukui Mgao kutoka kwa Wagombea ili awasafishie njia kwa 'Mzee'

Nchi hii katika safu ya Uongozi iliwahi kupata wajamaa wanne tu
1) Julius Nyerere
2) Rashid Kawawa
3) Ibrahim Kaduma
4) Balozi Daudi Mwakawago

Haya ni maneno ya Mkurugenzi Mstaafu wa Usalama wa Taifa Dr Hassy Kitine na aliyasema haya mbele ya Jakaya kikwete, Mwinyi, na Mkapa kwny Msiba wa Hayati Daudi Mwakawago…wengine ni waigizaji tu wa Kuvaa mashati ya kijani na wengine tai zenye rangi ya Bendera lakin hamna kitu


Polepole ni mjamaa kule wanafundisha ujamaa?
 
Kitendo cha Rais wa Tanzania, Samia Suluhu kumteua Humphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi kimewashangaza wengi, kwa kuwa ni kama haikutegemewa hata kidogo.

Mshangao huo ni kwa kuwa ilionekana wazi kama Polepole ameshakuwa ‘mpinzani flani’ kwa ile kampeni yake ya 'kuondoa wahuni' huku akiongoza katika kukosoa mambo kadhaa ya Serikali ya sasa kiasi kwamba TCRA ikakifungia kipindi chache cha Darasa la Uongozi alichokuwa akirusha YouTube.

Lakini mimi natazama hii kitu katika macho ya utofauti:

1. Polepole siyo muumini wa chanjo, ukifuatilia sheria za Malawi ili uweze kuingia ndani ya nchi hiyo kama ni mgeni unatakiwa uwe umechanjwa ndani ya saa 72 kabla ya kuingia nchini humo.

Unatakiwa kuwasilisha vielelezo vya majibu yako ya njia ya electronic, pia ukifika nao watatakiwa kukuchanja, lakini kama hutakuwa muumini wa kuchanja, unatakiwa kukaa karantini kwa muda wa siku 10 kabla ya kuruhusiwa kuingia na kuendelea na shughuli zao.

Swali, Polepole atakubali kuchanja na kubadili ule msimamo wake kwa kuwa tu amekuwa balozi? Au mimi sijui kuwa ukishakuwa balizi hadi kwenye ishu za afya unapewa kipaumbele cha kutokaguliwa kama umechanja au la?

2. Kwa kuwa alikuwa ameshaanza katabia ka kuwa mpinzani ndani ya mfumo, ni kama wamemuweka mbali ili wamfunge mdomo, kwani kwa levo ya ubalozi huwezi kumsikia akianza mambo yake yale ya WAHUNI au kuipinga Serikali ambayo imemteua.

3. Wanamseti, aende akawe balozi ili apotee kwenye siasa za Tanzania, kisha akiwa huko jamii ya Watanzania itapoteza kumbukumbu dhidi yake na baada ya muda anapigwa chini, kazi kwisha!

Wamemtega ili aondoke kwenye mfumo wa kijani
 
Back
Top Bottom