Huwa kila siku natafakari umuhimu wa Baba katika maisha ya kila Familia

Thamani haipimwi hivyo mzee. Thamani ya mama iko hapa :

Anasema Allah mtukufu :

14. Na tumemuusia mtu kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili. (Tumemuusia): Nishukuru Mimi na wazazi wako. Ni kwangu Mimi ndiyo marudio. (Luqman : 14)

Haya mengine ni katika wema tu,wema ambao hata asiye baba yako wala asiye mama yako anaweza kukufanyia. Na hii ndiyo mizani ya sawa.
 
wa mama wengi huwachochea watoto kuhusu baba na kusema vibaya na kujenga chuki mtoto kumchukia baba mamawengi wabaya
Umejiuliza sababu ni kwanini wanachochea huo ubaya
 
Hapo umeingia kwenye suala lingine.....kwa haya ya mama kubeba mimba, kuzaa na kunyonyesha hakuna kiumbe mwingine amepewa uwezo huo zaidi ya jinsia ya Ke/ Mama..... watoto wengi hawana mapenzi na baba zao si kwamba kwa kuwa akina baba hawajabeba mimba na kunyonyesha bali silka za akina baba za kutowajibika ipasavyo kwa watoto wao na hiki ndicho kinachozungumzwa kama sikosei
 
Sorry
Wewe Ni mwanaume au mwanamke?
 
Kwa nini mkuu huja-acknowledge mwandishi wa hili bandiko lako? Hivi plagiarism humu inaruhusiwa? Hii habari alishaisimulia Julius Mtatiro, sacha hizo mwamba! Ni ujinga kufanya copy and paste habari ya maisha ya mwenzako na kuigeuza kuwa ya kwako!
 
Sasa hapo ndipo thamani ilipo mzee,ndiyo maana nikasema hivi hayo uliyo yataja hata mama wa kambo anaweza kuyafanya mzee au mtu kando mwingine,kama mdau mmoja huko juu alipo msifia mama yake mlezi.

Ndiyo maana nikasema hivi,suala la wajibu anaweza kulisimamia hata asiye kuwa mama wala baba. Leo hii mama yako angeamua kukumaliza hata kabla ya kukuzaa angeweza tu.

Ndiyo sisi katika dini yetu,kutokana na thamani ya mama tukaambiwa tumpe mara tatu zaidi ya baba. Sema ulimwengu wa kufanana kwa haki zama hizi wanamdogosha mama na kumfanya akawa sawa na baba,wakidhani wanampa thamani.

Nakomea hapa.
 
Shukran mkuu nimejifunza kitu
 
Ninachoona hapa yoyote kati ya wazee wawili awe mama au baba akiishi na wtt wake vizuri ipaswavyo akatekeleza majukumu yake na wajibu wake basi watoto watarudisha thamani tu labda for rare cases.

Chengine wa Baba wengi waliokuwa wamekimbia majukumu yao wakati familia inamuhitaji ndio wanao kuja kidharaulika kwa watoto wao. (wtt wachache wanaojielewa na wasio na visasi ndio huwacha tu mambo yapite yaende)

Binafsi sijalelewa na baba mzazi (walitengana na mama)

Baada ya hapo nmekuja kumuona baba yangu nikiwa mtu mzima kabisa) So sina uchungu nae kihivyooo. Though simdharau hata kdg naongea nae kwa simu mara kwa mara. (nimeshapuuza yaliyopita japo yamenithiri sana kisaikolojia. Tunaishi na trauma. Sasa kama mtu una moyo mgumu basi ndio unabaki na chuki moyoni mwako daima)
 
Angekuwa ndiyo mama katelekeza mwanaye kamuacha na baba yake ungeshauri hivi
 
Wakati nakua baba yangu ni mtu wa kusafiri sana hivyo sipati nae muda mwingi nikawa kila tatizo namwambia Mama anasaidia nikawa naonaga baba hana msaada kabisa lakini nilivyozidi kukua nikaanza kuelewa kwann tunamuita baba anapambana mno huyu mzee kutuweka mahali pazuri Mungu awabariki wazazi wote wapambanaji kwa ajili ya watoto zao
 
Nimekuja kujua thamani ya baba baada ya mimi kuwa baba, aisee mzee wangu nampenda sana na alifanya kila kitu ili wanae tupate chakula na nguo..

mzee ramo kwa sasa amezeeka hana nguvu tena za kutafuta...
 
Sisi wanaume..
Sisi vijana ambao ni baba tunachukuliwa POA sana....ila tutaendelea kutimiza WAJIBU WETU Kama tulivyofanyiwa tulipokuwa wadogo na wategemezi....

Malipo yetu ni kufanikiwa KUISIMAMISHA familia BORA.....

Mwenyezi Mungu atupe afya njema,nguvu na uhai mrefu mababa wote ,aaaamin aaaamin aaaamin 🙏
 
Niliiona kwenye group hi story nikaipuuzia ila very painful and relevant
 
Kaka you nailed......🏋️🏋️
 
Mkuu wewe ni Mtatiro au umekopi hii Stori yake manake nimewahi kusoma hili andiko kutoka Kwa Mtatiro. Kama wewe si yeye ulipaswa kumtambua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…