Huwezi nishawishi Nyerere alikuwa Rais bora

Nyerere alitenda kulingana na usawa wa zama husika.
Kwangu Nyerere ni bora kwasababu kuu tatu;
1)Ni mtu aliyepambana kwa nafasi yake hadi uhuru wa hili taifa unapatikana.
2)Alikua mtu mwenye mawazo na sera chanya za kizalendo japo nyingi ama baadhi zilifeli.
3)Ni rais ambaye alikiri kukosea katika zile sera alizozianzisha baada ya kuona matokeo yake asi baadae.


Mambo mengine ya kibinadamu tu.
 
Sawa basi bora mama SSH. Wabongo mnagubu sana.
 
Nyerere alikuwa na akili mno. Yaani hata ukionganisha akili za marais wote bado sum yao haizidi akili ya JK Nyerere. Nyerere hakuwa Mwehu na sio wa kumlinganisha na wehu.
 
Nenda Kenya kama sio mkikuyu kutoboa inabidi ukaze kweli kweli ikibidi uue mtu . Nilienda Marekani nikakutana na radio ya wakikuyu. Kwenye kutokomeza ukabila Mwalimu nampa marks.
 
Ni kweli kwa 100%. Huyu babu ndio kaua nchi yetu na kaweka nchi ya MISUKULE
 
Nyerere alikuwa kiongozi bora kwa wakati ule zamani, saiz asingetoboa hata nusu mwaka enzi zile watanzania walikuwa hawajui dunia inaishije inshort alitawala watanzania wajinga. Saiz kila mtu ana akili timamu ndo maana mabadiliko yalipoanza alistaf urais
 
Julius Nyerere, rais wa kwanza wa Tanzania, anajulikana sana kwa harakati zake za kupigania uhuru na sera zake za Ujamaa, lakini kuna mambo makubwa aliyoyafanya ambayo hayajulikani sana na watu wa kawaida. Hapa kuna baadhi ya mambo hayo:

1. Kuimarisha Elimu kwa Kuweka Msingi wa Elimu ya Bure:
Wakati sera yake ya elimu inajulikana, watu wengi hawajui kuwa Nyerere alijenga mfumo wa elimu kwa msisitizo wa kuwaelimisha wananchi wote, bila kujali hali yao ya kifedha. Alitumia rasilimali ndogo za taifa jipya kuanzisha programu za kujua kusoma na kuandika. Hili liliwezesha Tanzania kuwa na kiwango kikubwa cha watu walioweza kusoma kwa muda mfupi.

2. Sera ya Kujitegemea na Kilimo cha Kujikimu:
Kupitia Azimio la Arusha, Nyerere alisisitiza kujitegemea kiuchumi kwa njia ya kilimo. Alianzisha programu za vijiji vya Ujamaa ambapo watu walihamasishwa kufanya kazi pamoja ili kuongeza uzalishaji wa kilimo. Ingawa utekelezaji wake ulikumbana na changamoto, nia ya kujenga uchumi wa kujitegemea bado ilikuwa ni wazo kubwa lisilojulikana vizuri na watu wengi.

3. Msukumo wake katika Siasa za Afrika na Ukombozi:
Nyerere alifanya kazi kimya kimya katika kusaidia nchi nyingine za Afrika kupata uhuru. Alitoa msaada mkubwa kwa harakati za ukombozi katika nchi kama Msumbiji, Zimbabwe, na Afrika Kusini, bila kutafuta sifa binafsi. Tanzania ilitumia rasilimali zake kusaidia makundi ya wapigania uhuru kama FRELIMO na ANC, hata wakati nchi ilikuwa na changamoto zake kiuchumi.

4. Kujenga Umoja wa Kitaifa:
Nyerere alifanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa Tanzania inabaki kuwa na amani na mshikamano licha ya kuwa na makabila zaidi ya 120. Alifanya juhudi za makusudi kuhakikisha kuwa taifa halikujigawa kwa misingi ya kikabila, kidini, au kijiografia. Lugha ya Kiswahili ilitumika kama chombo cha kuimarisha umoja huo.

5. Kusaidia kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki:
Wakati mwingi mchango wa Nyerere katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) haupewi uzito unaostahili. Nyerere alikuwa mmoja wa waanzilishi wa Jumuiya hii, akiamini katika nguvu ya umoja wa kikanda kwa maendeleo ya kisiasa na kiuchumi. Hata baada ya kuvunjika kwa Jumuiya hiyo mwaka 1977, alibaki kuwa mtetezi mkubwa wa umoja wa Afrika Mashariki.

6. Nafasi yake kama Mwanafalsafa:
Watu wachache wanajua kuwa Nyerere alikuwa pia mwanafalsafa wa kisiasa. Mbali na kuwa kiongozi wa kisiasa, Nyerere aliandika na kufundisha falsafa ya Ujamaa wa Kiafrika. Alijaribu kuunganisha mawazo ya kijamaa na tamaduni za Kiafrika ili kujenga jamii yenye usawa.

7. Kuongoza kwa Maadili na Kujinyima:
Katika dunia ya siasa iliyojaa rushwa na ubinafsi, Nyerere alisimama kama mfano wa kujinyima binafsi. Aliishi maisha ya kawaida hata akiwa rais, na hakuacha mali nyingi baada ya kung'atuka madarakani. Hii haijulikani sana kwa wengi, lakini ilitoa mfano mzuri wa uongozi wa maadili.

Mchango wa Nyerere unakwenda mbali zaidi ya yale yanayojulikana kwa juu juu, na alijitahidi kujenga misingi imara kwa taifa jipya na kwa bar

a la Afrika kwa ujumla.
 
Naunga mkono hoja kwa 80% hakuwa bora kama anavyohubiriwa sema alijitahidi sana kueneza propaganda kuhusu yeye kuwa ni bora
 
Nyerere ali-supp chuo scotland,halafu ujiniazi haupimwi kwa kujua tebo ya tisa
 
Nyerere ali-supp chuo scotland,halafu ujiniazi haupimwi kwa kujua tebo ya tisa
Mwalimu hakuwahi kusupp Chuo. Wa kusupp na kufoji documents za Vyuo wanajulikana, na mmoja wao alimchukia sana Ben Saanane kwa kumuanika.

Historia inaonyesha alifanya vyema sana mitihani ya kwenda Makerere. Wakati huo Babu yako akiutumia ujana wake kupiga matunguri bush huko.
 
Unabisha nini, ali-supp chuo scotland
 
Alifanya makosa mengi lakini kubwa kuliko kitendo cha kuwatimua wazungu mapema kabisa baada ya uhuru wakati hatukuwa na watu wenye uelewa kuhusu viwanda alichemka sana. Tukabaki na kilimo chetu na mazao yetu hatuna pa kuyapeleka.
Kama watu kama Sinde wakiweka ukweli bila kumumunya maneno wangeongea mengi ila kakazania muungano tu
Wakati tunapewa uhuru kumbuka kukikuwa na hela nyingi sana yaani million za dollars na zilikuwa za serikali wakiwepo wazungu wakamwachia PM Nyerere
Viwanda vilikuwa vipya na vinafanya kazi
Hela zote zilienda wapi?
Baada ya miaka kadhaa tukaingizwa vitani kwa maneno ya kuwa Uwezo tunao
Hela zikaisha zote
Mpaka dawa za mswaki zikawa magendo
Halafu ikaja Uhujumu uchumi kwa sisi ilikuwa mengine
Ila vijana hawajui haya
 
Babu yako alifeli, baba yako kafeli, wewe umekuwa mtu mzima bado upo pale pale huna mbele wala nyuma, hapo mjinga ni nani wewe au babu yako? Kuendelea kumlalamikia mtu aliyetoka madarakani over 30yrs ago ni ufinyu wa fikra na ujinga wa hali ya juu. Mlitaka Nyerere asolve matatizo yenu yote ya mbele ili nyie mfanye nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…