Huyo mwamba alishawahi kuwa mnunua karanga Kahama leo ni Ltn Col wa RDF

Hakuna wakati Tanzania inatoa namba za NIDA kwa Warundi wengi kama wakati huu na sababu ni ile ile Makamu wa Rais anatokea Kigoma.
Duu kwamba damu ni nzito kuliko Maji? Niliwahi kuona taarifa BBC jinsi warundi walifurahia Mpango kuwa VP na pia alifanya ziara walimpa heshima kubwa..

Sasa Kila nikiitafuta iliondilewa hivyo nimeshindwa kuandaa Uzi bila ushahidi ila nilisikia Kwa maskio yangu.
 
Natumaini hata wa kwetu wapo huko kwao, tena wako na mission kubwa kuliko hizi za kwao hapa kwetu.

Hata mataifa makubwa hayajaweza kuzuia moja kwa moja majasusi kuingia katika ardhi yao, Marekani kuna majasusi wa china urusi na kwingineko, kadhalika na huko china na kwingineko kuna majasusi wa kimarekani.

Kwa hio sio ajabu sana kukuta majasusi wa kirwanda na kwingineko wapo kwetu, ila ajabu itakuwa kama wakwetu hawapo kwao au kwetu tutakuwa rahisi taarifa kuvuja kwao .
 
Maana yake ni kuwa Tanzania hasa Tanganyika haina kitu maalum cha kujivunia katika dunia ya leo. There is simply no national pride.

Watu hujivunia nchi yenye alama kubwa za maendeleo; nchi inayotambulika kwa sifa maalum duniani. Ndio maana hata ndugu zetu wa zenji hujitambulisha zaidi kwa uraia wa Zanzibar kuliko wa Tanzania.
 
Wakati huo Rwanda haina cha kujivunia ukiachana na mauaji ya kimbali. Rwanda ina kipi cha kujivunia kuzidi Tanzania ambacho ndio unadai wanatumia?
 
Doohh!!! Kwamba Tz haifahamiki kuliko Rwanda!.
Maajab haya
Harakati za propaganda za Kagame kuinasibu Rwanda kimataifa si za mchezo. Huku kwetu siasa za ndani za madaraka na upigaji wa kidola (kleptocracy) ndizo kila kitu.

Tumewaachia Kenya na Zanzibar kuvuma kimataifa kupitia rasilimali zetu. Hatuna mkakati makini wa kitaifa wa kujiinua kimataifa. Kila anayeingia madarakani anakuja na yake kwa maslahi binafsi ya familia yake na genge lake basi.
 
Tz is very known compared to them all ila ni kwel TZ tuna viongozi wapumbavu haswaaaa
 
TUMELALA KIASI HICHO???!!!...
Tanzania yetu 🇹🇿....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…