Huyu aliyebandika mabango ya Imani Upendo Miujiza ya mkutano wa dini Dar, achukuliwe hatua

Huyu aliyebandika mabango ya Imani Upendo Miujiza ya mkutano wa dini Dar, achukuliwe hatua

Hahah!!!

Sisi CCM tutamsajili huyo jamaa atusaidie kumtangaza mama 2025, maana si kwa uwezo huo wa kuipamba Dar kwa vipeperushi
[emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji23][emoji28][emoji28][emoji23][emoji28][emoji28]
 
Sasa huu ubishi inabidi tukamlete Munishi mzee wa Malebo aje aseme neno. Maana naona upande wa pili hawataki haya mabango.
 
Eti Muhindi. Huyo anaitwa Daniel Kolenda mrithi wa Bonke.

Kuanzi tar 6-10 October atakuwa anapiga mikutano zaidi ya mitano kona zote za Dar kwa wakati mmoja. Yupo na timu yake.
 
Umeona uchafuzi alioufanya..kwenye madaraja na Kuta za watu?
Hamna kibanda changu hakijabandikwa hayo matangazo,sasa hivi

namimi nang'oa banner zao walizotundika nachukua turubai lile

na zile mbao na ile mirunda inisaidie katika ujenzi wa ofisi zingine

yeye si ana pesa sana acha sisi maskini tubebe hayo mabanner yake,ANABOA si kitoto.

wabandika matangazo wake sijui wanazunguka saa ngapi kubandika maana kazi wanayofanya,Mchwa akasome.
 
Tatizo ni akili za hao vijana wanaochukua haya maposta na kwenya kuyarundika sehemu moja!! Hooligans!! Kama kazi ya kusambaza habari ya mkutano WA injili huwezi acha kuchukua haya maposta!! Pia haya hutokea kipindi cha mikutano ya kampeni ya Chama kikubwa twawala
Mbandikaji anapewa poster PC 100,000 anaambiwa zote zibandikwe UBUNGO

Only Ubungo, hivi ili azimalize zote atafanyaje? Shida sio kubandka shida ni mzigo anaopewa

Halafu anaambiwa Yote yaishie mtaa flani na picha apige akishamaliza bandka ndio atalipwa, kifuatacho ndio hiki tulichokiona....
 
Nlikua nmepaki gar nikakuta kabandika kweny kioo Cha nyuma
 
Nilidhani una hoja ya maana kumbe umeona matangazo usiyoyapenda wewe binafsi yako

Maana maeneo hayo hayo matangazo ya wengine hasa waganga wa kienyeji yapo,hujaongea lolote,umeona hili usilolipenda umeamua kuongea

Kwanini usipige marufuku matangazo ya aina yeyote hua yanakua maeneo hayo siku zote?

Matatizo ya double standard yanakupelekesha sana..Kaa kwa kutulia mkuu
Issue sio matangazo asiyoyapenda. Tatizo ni aina ya ubandikaji. Tangazo hilo hilo limejirudia x 800 eneo moja. Zaidi ya kuwa uchafuzi wa mazingira lakini pia ni uharibifu wa raslimali. Alitakiwa kuyabandika moja moja maeneo tofauti tofauti ili ujumbe uwafikie watu wengi.
 
IMG_20210924_132508_243.JPG
 
Afrika unaweza jiamkia ukafanya kitu openly bila kufuata utaratibu na maisha yakasonga kawaida tu. Huu upuuuzi huwezi kuufanya nje.

Tunaona wachina wanamiliki hadi migodi bila vibali na wanadunda mitaani.

Kuna mtu alisema ni rahisi kutoboa kimaisha Afrika kuliko nje sababu Afrika kimsingi bado hatufuati sheria na taratibu.
 
Cha muhimu akimaliza wayatoe maana ni too much! Yani imekuwa kero sasa! Ila ndo hivyo kafaulu kucapture attention zetu, kila mtu sasa anajua kuna mkutano wa injili
Na ni pesa nyingi sana imetumika kwenye kazi hiyo, kwani ni vijana, mateja ndio wamepewa kazi hiyo ya kuyabandika, sehemu za hatari hatari wanabandika usiku!!!unakutana na kijana amebeba furushi na ndoo ya maji anaenda kubandika, na yale yanagundi kabisa, anachukua maji anamwagia sehemu anayotaka kubandika tu, tayari kitu kinanasa!!ki ukweli ni vurugu tupu
 
Back
Top Bottom