Huyu kijana Amedhalilika sana

Huyu kijana Amedhalilika sana

Kaokota dodo afu wewe wasema nini?

Maisha ndio haya haya.
Mkuu lakini ukiwaangalia kwa jicho la tatu huyo Mama na mume wake sizani kama ata wanazo hizo mali walizo zitaja.
 
Haha! Kwanini mimi? 😅

Halafu hii ndoa itadumu miaka na miaka mi nawaambia 😅 Mchezo ni mmoja tu, jamaa kujifanya hamnazo , Vijana wa siku hizi tunawajua….. Ukiwa na ka kazi wanakung’ang’ania sembuse umepewa mimali 😂
Mh... labda. Ila mwanaume itabidi awe kama house boy. Hakuna kuhoji, hakuna kuona wivu.
 
Mkuu kwanza familia ya mwanamke wamemdharau sana, wameshindwa nn kuorodhesha hivyo vitu kwa jina la mkwe wao badala ya Binti yao?
Hivo vitu tupeane kimya kimya sio kutangaziana hadharani,mwanaume unaonekana huna lolote,vitu vyote umepewa
Jamaa atapelekeshwa sana na kutokua na sauti
 
Mbona wamtaje binti yao tu kwenye hayo? Kwani anaenda kuishi mwenyewe huko?
Wameshamuandaa kisaikolojia kijana kuwa hizo zawadi ni za mwanamke sio za wanandoa! Hivyo ajue kuwa anakwenda kupigwa na kitu kizito
 
Huwezi kuumpa zawadi yoyote mke wangu bila concern yangu kama Mume, je kama ni hawara wa Deborah ndiyo katoa hizo zawadi kupitia mama mkwe utajuawaje!!?? Mwanaume usikubali haraka haraka kila kitu kutoka ukwenu hata kama kapewa mkeo,chunguza kwanza
Huyo siyo mkeo ni mchumba, na hapo wako kwenye send-off.
Narudia tena, hizo zawadi kapewa mwanamke na familia yake, kapongezwa kwa kupata bwana.
Siku ya harusi ndipo watapewa zawadi za pamoja.

Swali la kizushi, je, wakwe wangempa mavyombo ya plastiki, mngekuwa na hasira kama hizi za viwanja?
 
Back
Top Bottom