Huyu raia Godwin Gondwe amepata wapi ujasiri wa kuvaa sare za JWTZ?

Huyu raia Godwin Gondwe amepata wapi ujasiri wa kuvaa sare za JWTZ?

Kinaitwa "mkasi:
Ni kweli ni mtu mnyenyekevu kwa kiwango chake...Binafsi ninamkubali...kwa unyenyekevu wake....mzee wetu wa kanisa pale mbezi tangibovu...hivi bado upo ...mkuu wa ulinzi na usalama wilaya ya Handen...ninakubali historia yake kaanzia maisha mbali sana...tafuta stori akipiga na salama...kwenye kipindi chake cha channel five enzi hizo...{sijui kile kipindi kilifia wapi..kilikuwa bomba sana}
 
Acheni TUTAWALIWE jamani, tuliyataka wenyewe! Tulichagua udikteta badala ya demokrasia.. na miaka mitano ijayo ndio itakuwa "kulima kwa meno"
 
Halafu anajifanyaga mlokole huyo
Sijawahi ona mlokole akiwa ndani ya kombat za jeshi

Kwa hiyo ndugu Nyumbu kwa hiyo mtu akivaa nguo za jeshi ulokole unaondoka papo hapo?
 
Ndugu Nyumbu wamepata ajenda mpya!
 
Ni kushow love tu ...yaani kama Simba inavyocheza mashabiki tunavas jezi zao kwa upendo nasio kwamba sisi ni wachezaji wa Simba ni vile JW wanajidai hawataki mazoea....
 
Hapo insue ni kwamba, unapoambatana na kikundi chochote cha ngazi ya kuanzia section na kuendelea mbele kwenye operation yoyote mkiwa pamoja, hasa ukiwa raia mwenye professional yenye tija ktk operation iyo ni muhimu kufanana nao, lkn iyo aitoshi tu, kwa kesi ya Godwin ni kwamba yeye ni Mwenyekiti wa ulinzi na usalama ndo maana kavaa izo sare za jeshi senior, kwa maana operation iyo inaongozwa na JW na siyo polisi.
Akuna kosa apo, ni uelewa tu.
 
Hakuna kosa hapo.DC ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya Wilaya na kwa msingi huo yeye ni Amiri jeshi mkuu kwa ngazi ya Wilaya huku Rc akiwa Amiri jeshi kwa ngazi ya mkoa. Tukumbuke kuwa hawa wote wanasimama kwa niaba ya Rais ambaye ni Amiri jeshi mkuu. Majukumuambayo angeweza kuyatimiza Rais wao ndio huyafanya kwa ngazi zao. Hivyo si dhambi na si kosa kisheria kwa RC au DC kuvaa nguo za kijeshi. Na wakati mwingine inapotokea oparesheni yoyote ya kiusalama DC anapaswa kuwa mstari wa mbele, na haendi kama DC anaenda kama Askari wa kwa ngazi ya Wilaya.
 
Inashangaza hata aliyekuwa Amiri Jeshi Ngazi ya Taifa Mstaafu lieutenant colonel Rais Jakaya Mrisho Kikwete sikumbuki akivaa gwanda la TPDF / JWTZ katika utumishi wake kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Huyo JMK hakuwa na ulimbukeni maana alishazivaa sana enzi zake akiwa bado mwanajeshi tofauti na chattleboy
 
Back
Top Bottom