IGP Sirro: Hatuna barua ya kumkamata Askofu Gwajima, utaratibu ufuatwe

IGP Sirro: Hatuna barua ya kumkamata Askofu Gwajima, utaratibu ufuatwe

Sasa imejulikana ni akina nani wapo nyuma ya askofu gwajima na kwa jeuri hii ya afande sirro huenda hata Rais Samia akawa yupo mifukoni mwa watu
 
Toka lini waziri akawa amiri jeshi? Yaani waziri atoe amri kwa jeshi? Tukiendekeza hilo kuna siku we waziri Mulamula ataamrisha jwtz ivamie Malawi!
Kwa Tanzania Mwenyekiti wa CCM Wilaya anaweza kumpa amri IGP au RPC kama hujui. Imeshatokea mara nyingi.

Kwa taarifa yako mkuu wa majeshi anampigia saluti mkuu wa wilaya, IGP na RPCs woooote wanampigia saluti mkuu wa wilaya hivyo wanaweza kupewa amri yoyote.

Hii ni bongoland.
 
Kwa Tanzania Mwenyekiti wa CCM Wilaya anaweza kumpa amri IGP au RPC kama hujui. Imeshatokea mara nyingi.

Kwa taarifa yako mkuu wa majeshi anampigia saluti mkuu wa wilaya, IGP na RPCs woooote wanampigia saluti mkuu wa wilaya hivyo wanaweza kupewa amri yoyote.

Hii ni bongoland.

IGP hana tatizo anataka huyo mjumbe wa nyumba kumi wa Tanzania aweke kwenye maandishi.
 
Kwani wale wanaokamatwa kwenye mikutano ya Mawaziri Jaffo, Awesu, Majaliwa nk papo kwa papo huwa inakuwa je?

Wale waliokuwa wanasukumwa ndani na yule mwamba wa Tabora nao je?

Karatasi zipi zilikuwa zinasainiwa au jinai ipi ilikuwa ikiangaliwa kabla ya habari?
Wakumbushe mkuu. Tanzania mwenyekiti wa CCM wilaya anakuweka ndani sembuse Waziri?
 
IGP Sirro amesema kuwa jeshi la polisi linaendeshwa kwa maandishi na kuna taratibu hivyo wanasubiri barua kutoka kwa waziri ili waangalie wanatekeleza vipi agizo lake...
Sirro mnapowakamata Viongozi wa Chadema mnakuwa na barua kutoka kwa nani ? wewe utavunja rekodi ya IGP mbovu kuwahi kuwepo tangu nchi hii ipate uhuru
 
Waziri amezoea kutengeneza kiki huko alipo kuwa,huwezi kuamrisha majeshi na TAKUKURU wamkamate Mchungaji. Mwenye mamlaka ya kuamrisha majeshi ni Amiri Jeshi Mkuu.

TAKUKURU awamu iliyopita ilitumika kutengeneza tuhuma za "kutakatisha fedha" kwa wananchi. Sasa Waziri anaingilia uhuru wa mwananchi kuongea maoni yake.

Waziri utajikuta umeingia kwenye 18 na safari yako ya madaraka na kìsiasa itaisha na utajikuta hutoshi kwenye nafasi uliyonayo:
1.Unaye mtuhumu, ametoa mfano wa Afisa wa Serikali aliye" fake" zoezi la chanjo.

2.Unaye mtuhumu anayo mifano ya wewe na msaidizi wako mkipinga chanjo (awamu iliyopita, mkionyesha mifano ya kutovaa barakoa,mkionyesha watu kunywa michanganyiko ya tangawizi iliyotengezwa Tanzania,mkiwaaminisha Watanzania kuwa hakuna korona).

3.Unakumbuka mwaka jana kuna baadhi ya nchi jirani zilikubali kutumia chanjo, lakini Tanzania tulikataa chanjo(Waziri na msaidizi wako mlikuwa katika Wizara hiyo ambayo mwaka huu mnatoa maelekezo tofauti na mlivyowaaminisha Watanzania.)

4.Unakumbuka kauli ya Serikali "Chanjo ni hiari"!!!,Tumia ushawishi na elimu kwa jamii badala ya vitisho.
 
Kuna baadhi ya Watanzania ni wapumbavu sana, yaani amri ya kumkamata Gwajiboy itoke kwa rais?

Acheni kumpa uspecial huyo tapeli ndio maana anaropoka anavyotaka.

Kipindi alivyokuwa anakamatwa na Makonda rais alihusika?
 
Gwajima amengukuwa ni mwanachama wa CHADEMA msingekuwa mmesubiri hata tamko...
Kila siku wanaimba Weledi, weledi, sijawahi ona ni mahali gani weledi wao hautiliwi shaka.
 
Hatujapa taarifa rasmi ya maandishi ya kutakiwa kumkamata Mhe.Gwajima.

Lakini hata tukiipokea tutachunguza iwapo matamshi yake yanaangukia Kwenye Jinai.

Na lakini tunaweza kuwashauri wakatatua jambo hili kwa njia za mazungumzo badala ya Polisi...... IGP Simon Sirro
 
Back
Top Bottom