Waziri amezoea kutengeneza kiki huko alipo kuwa,huwezi kuamrisha majeshi na TAKUKURU wamkamate Mchungaji. Mwenye mamlaka ya kuamrisha majeshi ni Amiri Jeshi Mkuu.
TAKUKURU awamu iliyopita ilitumika kutengeneza tuhuma za "kutakatisha fedha" kwa wananchi. Sasa Waziri anaingilia uhuru wa mwananchi kuongea maoni yake.
Waziri utajikuta umeingia kwenye 18 na safari yako ya madaraka na kìsiasa itaisha na utajikuta hutoshi kwenye nafasi uliyonayo:
1.Unaye mtuhumu, ametoa mfano wa Afisa wa Serikali aliye" fake" zoezi la chanjo.
2.Unaye mtuhumu anayo mifano ya wewe na msaidizi wako mkipinga chanjo (awamu iliyopita, mkionyesha mifano ya kutovaa barakoa,mkionyesha watu kunywa michanganyiko ya tangawizi iliyotengezwa Tanzania,mkiwaaminisha Watanzania kuwa hakuna korona).
3.Unakumbuka mwaka jana kuna baadhi ya nchi jirani zilikubali kutumia chanjo, lakini Tanzania tulikataa chanjo(Waziri na msaidizi wako mlikuwa katika Wizara hiyo ambayo mwaka huu mnatoa maelekezo tofauti na mlivyowaaminisha Watanzania.)
4.Unakumbuka kauli ya Serikali "Chanjo ni hiari"!!!,Tumia ushawishi na elimu kwa jamii badala ya vitisho.