IGP Sirro: Hatuna barua ya kumkamata Askofu Gwajima, utaratibu ufuatwe

IGP Sirro: Hatuna barua ya kumkamata Askofu Gwajima, utaratibu ufuatwe

IGP Sirro amesema kuwa jeshi la polisi linaendeshwa kwa maandishi na kuna taratibu hivyo wanasubiri barua kutoka kwa waziri ili waangalie wanatekeleza vipi agizo lake.

Pia ameongeza kuwa hayo maelekezo ameyaona kwenye mitandao ya kijamii hivyo anasubiri barua rasmi ili waangalie jinsi ya kuyatekeleza hayo maelekezo ya Waziri wa afya kwani serikali inakwenda kwa maandishi.

Sirro pia amesema wataangalia kama kweli kuna jinai au lah ambayo ina haja ya kufungua mashitaka...

Na ameendelea kusema pia kama hatokuta jinai watashauri jinsi ya kumaliza hilo swala katika njia nzuri.

Source: Clouds FM

Pia soma:
- #COVID19 - Waziri Gwajima aagiza Askofu Gwajima kukamatwa ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya UVIKO-19
Du kweli huyu Sirro ni ZERO kweli kweli! Alipomkamata Mbowe alipata maandishi kutoka wapi? Nchi hii ina mijitu mitutusa sana.
 
Wale waliokuwa wanasukumwa ndani na yule mwamba wa Tabora nao je?
Kumbe hufahamu jinsi muundo wa kiserikali ulivyo, wakuu wa mikoa na DC wao wanauwezo wa kutoa amri ya kumsweka mtu ndani (nafikiri ni 48hrs) kwenye sehemu yao. Wao wanasimama badala ya Rais katika wilaya/mikoa yao.
 
Single touch double manifestation ( sijui kama niko sahihi)
 
Kumbe kamata kamata zinahitaji barua.... Sirro awe na akiba na maneno, yatamrudia siku moja.
 
Kumbe hufahamu jinsi muundo wa kiserikali ulivyo, wakuu wa mikoa na DC wao wanauwezo wa kutoa amri ya kumsweka mtu ndani (nafikiri ni 48hrs) kwenye sehemu yao. Wao wanasimama badala ya Rais katika wilaya/mikoa yao.

Kwanini umechagua mstari mmoja badala ya aya zote 3?

IMG_20210817_232921_638.jpg


Hiiiiii bagosha!
 
Toka lini waziri akawa amiri jeshi? Hilo likiruhusiwa kuna siku waziri atatoa order kwa jwtz ivamie nchi nyingine. Mawaziri wajifunze namna ya kufanya kazi.
Unachokosea ni kwamba hujui Central government ina nguvu kuliko Local government.
Unaelewa kuwa mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa wana mamlaka ya kuamrisha mtu akamatwe? (Local government)
Je unasemaje kwa waziri ambaye yuko katika central government?
 
Kumbe hufahamu jinsi muundo wa kiserikali ulivyo, wakuu wa mikoa na DC wao wanauwezo wa kutoa amri ya kumsweka mtu ndani (nafikiri ni 48hrs) kwenye sehemu yao. Wao wanasimama badala ya Rais katika wilaya/mikoa yao.
1629232760740.png


Huyu Katambi ni DC au RC wa wapi? Mbona katoa amri ya mwananchi kuwekwa ndani?
 
Hizi Busara Sirro amezitoa wapi [emoji16][emoji16][emoji16] oooh! itakuwa ni side effects ya chanjo sio..??[emoji1787]
 
Kwa Tanzania Mwenyekiti wa CCM Wilaya anaweza kumpa amri IGP au RPC kama hujui. Imeshatokea mara nyingi.

Kwa taarifa yako mkuu wa majeshi anampigia saluti mkuu wa wilaya, IGP na RPCs woooote wanampigia saluti mkuu wa wilaya hivyo wanaweza kupewa amri yoyote.

Hii ni bongoland.
Asichokijua ni kwamba wakuu wa wilaya, mikoa, mawaziri ni makamishna, wateuliwa wa rais.
 
Imetoka kutaka kichwa cha Gwajima imekuwa double manifestation tunataka vichwa Gwajima na Sirro. Hii corona sikuwahi fikiri inaweza kuleta mitafaruku ndani ya serikali yetu.
 
Kwamba Mkuu wa wilaya anaweza kuitisha majeshi kufanya kitu fulani?
Salute ni ishara ya heshima, hiyo haina maana kwamba kila anaepigiwa salute anaweza kumuamrisha yule anaepiga salute wakati wowote,na kwanza sio simple hivyo kama unavyodhani unless kuwe na go-ahead kutoka kwa Amri jeshi.

Yaani CDF apewe amri na Mkuu wa wilaya? Kwamfano Albert Msando asimame jukwaani kumpa amri MABEYO alafu itekelezwe?[emoji15]

Moja Kati ya hoja ya kijinga kabisa kwenye huu mjadala.
Unaishi nchi gani?
 
Nijuavyo mimi mbunge kama mbunge ana sheria zake kukamatwa sasa wakimkamata hovyo hovyo anaqeza waumbua kama anaijua sheria kingine hata wakisema wampandishw kizimbani bado atawashinda kwa mfano akiwauliza hayo maneno aliyazungumzua wapi ma awrikali imjibu kanisani je?serikali si imesema haina dini? imekuwaje tena inatambua hilo
Kwani wale wabunge waliosemekana na mkuu wa mkoa kuwa wametoroka bungeni na kuja Dar, kuna sheria ipi ilitumika kuwakamata, hadi mkuu wa mkoa kuwataka warudi bungeni? Taja hiyo sheria hapa!
 
Kwani wale wabunge waliosemekana na mkuu wa mkoa kuwa wametoroka bungeni na kuja Dar, kuna sheria ipi ilitumika kuwakamata, hadi mkuu wa mkoa kuwataka warudi bungeni? Taja hiyo sheria hapa!
Walikua wanazurula Dar, imebidi wakamatwe kwa amri ya mkuu wa mkoa.
 
Kuna uwezekano mkubwa hata Sirro mwenyewe ni Pro Askofu 😁 ila alichanja kwa shinikizo la Mamlaka ya uteuzi tu ila haikuwa HIARI.

Kutumika nako kuna ukomo wake,waachwe watu waongee na wenye wajibu wajitokeze kuweka mambo sawa.

Kikwete aliwaambia,"Hoja hazipigwi rungu,Hoja hujibiwa kwa hoja".
 
  • Thanks
Reactions: mmh
😂😂😂 hapo Gwajiboy kapata pa kupumzkia atamuandama uyo Dorothy mpaka aombe pooh. Akili ya Gwajiboy na manara ni moja wote ni waropokaji na hawachagui neno.
Sio watu wa kubishana nao hao ni kuwapuuza tu .
 
Back
Top Bottom