😄😄 anakuhesabia unavyotumia unit zake za umeme as if gharama ya Unit ya umeme kwa dar Ni tofauti na ya mkoani ambako wakija hua wanashinda wanaangalia tv kwny majumba ya watu kabla jioni hajatoka kuzunguka mji ili aje awahadithie jinsi gani ambavyo ameona maeneo mazuri ya ku-invest hapo mkoani kwenu ambako nyie wa mkoani hamtumii fursa.
Utamsikia tu:
1.Lile eneo ukipiga lodge yako ya maana, hakikisha Ina maji ya Moto(heater) ukaweka na jiko lako la kitimoto unatoboa fasta.
2.Mara aseme nimejaribu kucheki English medium zilizopo huku naona bado bado Sana hii ni fursa Sana.
3.Baadae anawaambia Ni namna gani anataka anunue maeneo makubwa ya kilimo aje afanye kilimo Cha kisasa huku akisema si unajua tena nguvu zinapungua ni muhimu niwekeze huku mkoani.😄😄 Mtasubiri huo uwekezaji.
4.Nimekumbuka hua wanauliza tena hivi kutoka sehemu flani mpk sehemu flani Ni Kilometers ngapi?Mkishamwambia unauliza fasta barabara ikoje akishaambiwa anasema hio Ni fursa ukiweka Coaster yako Ni uhakika kupiga pesa.
Watu wa Daslam wanajionaga wao ndio 'smartest person in the room',nyie wa mkoani Ni mafala flani hivi.
Kumbe wao Ni wazee wa Day dreaming na maneno mengi yenye lafudhi ya kidaslam 😄😄