Ikiwa wao wanataka handsome na wenye Pesa Kwa nini wewe iwe kosa ukiwa na vigezo?

Ikiwa wao wanataka handsome na wenye Pesa Kwa nini wewe iwe kosa ukiwa na vigezo?

Linapokuja swala la mapenzi na mahusiano,WANAUME TUNAKUWAGA WAJINGA SANA. TUNAJIPENDEKEZA NA KUJISHUSHA SANA NA KUPOTEZA HADHI.


Nafunga mkono hoja. Wanaume tujithamini na kuwa na misimamo sio kwenda kwenda tu kama ling'ombe
Ubadilike sasa. Anza kuishi kwa vitendo si maneno. Robert Heriel Mtibeli hajaanza jana wala juzi kuwashtua wahanga. Usiwe mtu wa kusikiliza na kuishia kukaa tu kimya, anza kuishi.
 
Kwema Wakuu!

Vijana, ikiwa usipokuwa na Pesa wanakudharau, wanakunyali, hawakutaki, na Wakati mwingine wanakutukana. Au ukimuoa siku ukafilisika wanakukimbia. Kwa nini kwako iwe kosa ukijiwekea vigezo?

Mfano, Kwa nini iwe kosa ukisema kamwe hautaoa single mothers? Wakati Muda huohuo wao ili uwe NAO lazima wakuulize unafanya kazi gani sijui hauna pesa na blah! Blah! Blah!
Kwa nini wafikiri wao ni spesho au wanataka uwaone spesho, Kwa nini wanataka uwaone hivyo? Na Wakati wakitaka uwaone wao ni spesho wao wanataka aidha kuku-neutralize au kukushusha thamani!

Hiyo kwetu Watibeli haipo hivyo. Sisi hatufanyi hivyo. Na tunajulikana hivyo. Na kila ambaye atakutana na wanaume jamii yetu atakiri hivyo.
Ukishaanza kuleta vigezo basi elewa vigezo vya Watibeli ni vigumu Mno. Ukitaka niwe WA thamani basi lazima ulingane na thamani unayoitaka kwangu.

Vijana wakiume, ninyi ndio wanaume. Ukikutana na Mwanamke ambaye anajifanya ni mtu wa vigezo na masharti basi nawe katika masharti yake ongeza mara Mbili.

Kamwe usijisalimishe Kwa Mwanamke. Kamwe usijihangaishe kisa Mwanamke. Kamwe usijitumikishe kisa Mwanamke. Kamwe! Kamwe! Kamwe!
Upendo sio kujisalimisha! Kujishusha! Yeye ndiye anatakiwa ajisalimishe, yeye ndiye anatakiwa ajishushe. Hataki apite kushoto. Atafute level yake au misukule yake.

Be a Man. Wewe ni Kichwa. Kicha kipo juu na sio Chini. Kichwa kipo Mbele na sio Nyuma.
Mwanaume ndio unatakiwa uwe na vigezo na masharti. Sio Mwanamke akuwekee masharti yake ya kijingajinga alafu nawe kama bwege unamsikiliza.

Msiwe kama Vijana wapuuzi. Jitu linahangaika kutoa jasho Mchana Kutwa Usiku kucha alafu bado linapelekeshwa na Mwanamke. Kudadadeki! Upuuzi tuu! Mara linanyimwa unyumba kisa sijui ujingaujinga. Hiyo kwetu Watibeli kamwe haitowezekana iwe Kwa Mwanamke kufikiri au kutenda. Hilo haliwezekaniki.

Mimi Taikon Mtibeli, naongea mambo haya bayana bila kificho wala kuficha utambulisho wangu. Ili Vijana wakiume muelewe Kwa urahisi. Msijesema ooh! Anayeongea hatumjui, ooh! Anaongea tuu Kwa vile anatumia Fake ID. Noo!

Vijana jitambueni. Sio kijana mzima unawaza kujipodoa na kujinakshi kisa kuwafurahisha mademu. Huko ni kujishusha thamani, Wanawake ndio wanatakiwa wafanye vitu kwaajili ya kukufurahisha.

ATI Vijana kama majinga, yanaambiana tafuta Pesa alafu ATI hizo Pesa zenyewe lengo Lao ni ili yapate Wanawake. Yaani kama majinga hivi. Mwishowe yakipata Pesa yanashangaa bado Wanawake hawawataki yanabaki kubung'aa na kupiga Mayowe kuwa Wanawake hawajui wanachokihitaji. Upuuzi tuu!

Kamwe Mwanamke asikuwekee vigezo vyake. Akijifanya ni MTU wa vigezo na masharti, mwambie Fresh, si anataka Michezo, cheza naye. Kisha akiingia kwenye kumi na nane fanya yako. Kisha pita kushoto. Mwanaume ndiye unayetoa mwongozo, sheria, vigezo na masharti.

Nimemaliza! Leo kiumeni.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kujipangia unachotaka ni haki yako ya msingi ya kikatiba na kibinadanu.

Wala huhitaji kujieleza sana, ukijieleza sana inakuwa kama hujitambui, unaanza kuomba upya haki yako mwenyewe.
 
Kujipangia unachotaka ni haki yako ya msingi ya kikatiba na kibinadanu.

Wala huhitaji kujieleza sana, ukijieleza sana inakuwa kama hujitambui, unaanza kuomba upya haki yako mwenyewe.
Kiranga huwa naku imagine sana. Ni mtu wa aina gani? Na guess ni dubwasha kuuubwa, halafu kumbe huenda ni mwembamba mfupi mweupe.[emoji23][emoji23][emoji23]

Anyways napenda michango yako
 
Ni kweli Kabisa.
Ishu ni kuwa Wanawake wengi wanavigezo vyao wanavyowapa Vijana wakiume lakini wao wakipewa vigezo vya Vijana wanaona kama wananyanyaswa.
Nakupa Mfano, Single Mothers.
Alafu na wanaume wasio na Pesa.
Wanaume wasio na Pesa tangu na tangu wamekuwa wakisemwa lakini haionekani na wala hawaoni kama wananyanyaswa lakini upande wa pili inakuwa vinginevyo
Hii ni kweli kabisa, haya mambo walioleta wazungu mambo ya equal rights wanatuvurugia sana dada zetu , wanaleta jambo ambalo hta wao in reality hawawez kulipractice..
 
Linapokuja swala la mapenzi na mahusiano,WANAUME TUNAKUWAGA WAJINGA SANA. TUNAJIPENDEKEZA NA KUJISHUSHA SANA NA KUPOTEZA HADHI.


Nafunga mkono hoja. Wanaume tujithamini na kuwa na misimamo sio kwenda kwenda tu kama ling'ombe
Nawashangaaga sana vijana wenzangu, ili mwanamke ajue unampenda eti lazima uwe fala, yan unakuta jitu limekuwa zezeta, linateseka alafu linasema hayo ni mapenz.. Maisha yenyewe mafupi, ni ujinga mtupu...
 
Back
Top Bottom