Ikulu: Rais Magufuli awaapisha viongozi walioteuliwa. Mathias Kabunduguru, Godfrey Mweli na Ali Sakila

Ikulu: Rais Magufuli awaapisha viongozi walioteuliwa. Mathias Kabunduguru, Godfrey Mweli na Ali Sakila

Safi Sana waliokuwa wakitaka afe,hafi!! Mzee wa watu endelea kukaza mambo yawe mambo hakuna namna.
Acha kabisa kiongozi. Mijitu tuliiambia tangu juzi kuwa uongo na uzushi ni kitu kibaya sana,haikuelewa.Haya sasa, mipuuzi yote imeumbuka kwa uprofessional wao wa uzushi.

Kuna mijnga sana ya uzushi.
 
Kama ni kweli basi sijawahi kuona watu wapumbavu kama ofisi ya ikulu na kurugenzi ya habari. Mtaacchahe watu wasambaze uvumi na kuwa na wasiwasi kiasi hiki bila kusena lolote. Inawezekaba walianzisha wao hili jambo ili kupima upepo. Yaani kanacNagu ni mzima basi mmefanya uchuro na mtaoatwa ba kuwapata ka kweli sasa. Yaani watu hofu tele nyie mbakunywa chai ikulu bila hofu?
Yaani ikulu iandae conference kujibu uzushi wa kigogo...
 
Lakini amejimaliza mwenyewe, hakuna wa kumuamini tena.
Kujificha pia kumemsaidia kujua ni kwa kiasi gani watumishi wa umma wasivyopenda kunyimwa nyongeza za mishahara na pia wasivyopenda kuhamia Dodoma na malalamiko yao mengi
 
Kigogo yuko wapi alete mrejesho mana yeye ndo alikua kinara huko tweeter kuupotosha umma
 
TAARIFA​

Mhe. Rais Magufuli leo tarehe 20 Oktoba, 2019 atawaapisha Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI na Balozi.

Hafla ya uapisho huo itafanyika Ikulu Jijini DSM kuanzia saa 9:30 alasiri hii. Itarushwa mubashara kupitia Redio, Televisheni na Mitandao.

====

UPDATES: 1600hrs

Rais John Magufuli amewaapisha Mathias Kabunduguru kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania, Godfrey Mweli kuwa Naibu Katibu Mkuu Tamisemi na Ali Sakila kuwa Balozi leo Oktoba 20 Ikulu jijini Dar

Rais Magufuli: Niwapongeze sana viongozi niliowaapisha leo hii, nendeni mkafanye kazi, katimizeni majukumu yenu kwa weledi”

Rais Magufuli: Muende mkawatumikie Watanzania bila kumuonea mtu kwa kadri Mungu wenu atakavyowaongoza. Kabunduguru wewe umefanya kazi sehemu nyingi, Utumishi na TAMISEMI naamini kwenye Mahakama utatusaidia sana

Rais Magufuli: Kaendeleze mazuri yanayofanywa na Mahakama. Mahakama inafanya kazi nzuri na imekuwa kimbilio la Wananchi wengi - Balozi Ally kaendelee na kazi zako. Kwa ufupi mkafanye kazi zenu vizuri kwa kwenda kuwatumikia watu

Rais Magufuli: Brigedia Jenerali wa TAKUKURU anafanya kazi vizuri. Kwenye Vyama vya Ushirika huku wakulima walikuwa wanadhulumiwa - Viongozi 99 wamekamatwa na Tsh. Bilioni 1.2 zilikuwa kwa viongozi wa AMCOS. Brigedia ameniambia lakini hadi sasa zimerejeshwa Milioni 255

Rais Magufuli: Kazi ya uongozi ni kusimamamia Haki, kufuata Sheria bila kumuonea mtu yeyote. Unaweza kusemwa vibaya ila wewe endelea na kazi - Si wote watakupenda ila tufanye kazi. Kwa ujumla nawashukuru wote, Mama Samia na kila mtu katika Utumishi wenu
View attachment 1239299
View attachment 1239300
View attachment 1239302
View attachment 1239303

Asante Mungu
 
Wale wakata mauno wa ufipga siwaoni hapa.
Ufipa wala hawana tatizo nae licha ya kuwatendea mabaya mengi wabaya wake wengi wapo ndani ya CCM na hasa watumishi wa umma wanataka nyongeza za mishahara na wasiotaka kuhamia Dodoma
 
Kuna watu nawaonaga wana akili na upeo kama akina Maria Sarungi, cha ajabu Kigogo2014 kawakamata pia.
 
usiempenda kaja.. Heheheeeee BAVICHA wako uvunguni washajinyea sasa
Screenshot_2019-10-20-17-07-17.jpeg
 
Back
Top Bottom