Ikulu: Rais Magufuli awaapisha viongozi walioteuliwa. Mathias Kabunduguru, Godfrey Mweli na Ali Sakila

Ikulu: Rais Magufuli awaapisha viongozi walioteuliwa. Mathias Kabunduguru, Godfrey Mweli na Ali Sakila

Kuna hawa watu, niliona post zako hadi nikashangaa kama kweli upinzani kuna watu wenye akili timamu
- Lema
- Heche
- Zitto
- Mashinji
- Lissu
Ila namuomba mh. Raisi awakanyage kwelikweli, safari hii asione huruma hata kidogo kwa hawa
Post ya Lissu kidogo ipo kiufundi huwezi Moja kwa Moja mlaumu
 
Ndo ajue kabisa hapendwi...
Maana mda wote kwenye kasheshe hilo katika comment 10 karibia 8 zinaomba mabaya kwake

hili jambo si kawaida
 
Kuna hawa watu, niliona post zako hadi nikashangaa kama kweli upinzani kuna watu wenye akili timamu
- Lema
- Heche
- Zitto
- Mashinji
- Lissu
Ila namuomba mh. Raisi awakanyage kwelikweli, safari hii asione huruma hata kidogo kwa hawa
Hivi Vicky Emmanuel Nchimbi ndiyo nani... Ni Mwanamke balaa.
 
Hongera mkuu.

Maana nikiona bandiko lako tu lazima niwe na dictionary pembeni. Leo umetiririka kiswahili maridhawa kabisa na nimenyaka neno MADHILA.

Kudos.

Hahahaaa ulidhani Kiswahili sikimanyi?

Ngoja nisiseme sana maana nikisema nitaishia kuonekana mtaraghani bure.

Nipo safarini kuelekekea Mijikenda...
 
Elimu elimu elimu
Narudia tena, kuitawala hii nchi ni rahisi sana!
Kizazi kinachosadiki kila jambo bila hata kuchukua sekunde chache kupima, kutafakari na kuhoji jambo ni hatari kuliko kansa.

Lakini kubwa zaidi, kiwango cha chuki na roho mbaya kimenistaajabisha sana.
Naweza kusema magonjwa, matatizo na shida nyingi zinazowasumbua watu huenda ni roho mbaya tu! Huwezi kuwa na roho mbaya namna hii ukabaki kawaida, haiwezekani.

Kweli napishana na mheshimiwa kwenye baadhi ya mambo, lakini kumuombea kifo au kufurahia mabaya yakimpata sijafaulu bado nihitimu hayo masomo kuelekea uchawi.
 
Kwa siku kadhaa sasa kuna watu [majuha] kupitia hii mitandao ya kueneza na kujazana ujinga na ujuha walikuwa wameshupaza shingo na kupaza sauti zao kutoa na kueneza uongo, uzushi, na pumba zao kuwa Rais ni mgonjwa, mara amekufa, sijui kapelekwa wapi huko kwenda kutibiwa, na kadhalika.

Wengine wakaja na upumbavu wao kuwa sijui kafanyiwa mambo ya kichawi huko Ruangwa. Wakaja na video inayoonyesha moshi kwenye sehemu aliyokuwa amesimama Rais wakati anahutubia. Wengine wakasema kwenye video hiyo wameona mwanga ambao hawana uhakika ni wa nini! Hata kama ni mwanga wa jua, eti hawakujua ni wa nini.

Just stupid beyond belief.

Nadhani sasa huo upumbavu wao umemalizwa na Rais mwenyewe. Nampongeza kwa yeye kuendelea kubaki njia kuu [taking the high road] na kufanya kazi zake.

Hao majuha wanaomwombea mabaya sasa sijui watakuja na tukio gani jingine!?!! Tusubiri tuone...

Ila nimestaajabu sana. Hivi hata kama mtu hukubaliani naye kisiasa na kiitikadi ndo umwombee mabaya ya kiwango cha kifo??

Kweli kabisa?? Yaani mtu unajitoa fahamu kabisa na kumwombea kiongozi wa nchi kifo??

Kifo hakina mwenyewe. Madhila maishani hayana mwenyewe.

Nyie mlokuwa mmeshupaa kuombea na kufurahia mmenufaikaje sasa?

Magufuli akifa leo hii wewe kama liuso lako lilikuwa na chunusi kama tunda la fenesi, hizo chunusi zitatoweka?

Bure kabisa.

Hii mitandao ya kijamii imetengeneza tabaka la majuha na mapunguwani kwa kiwango kikubwa sana hadi inatisha.

Ooh eti Kigogo kasema...[sasa hivi naona wametoka kwa ‘Da Mange kasema’ na wamehamia kwa Kigogo [emoji1787]].

Wengine wanasema kuwa eti sijui Magufuli ajitafakari, ajifunze, n.k.

Ha! Ajifunze nini? Ajitafakari nini?

Kwendeni zenu huko.

Jitazameni nyie wenyewe kwanza kabla hamjaanza kuwahubiria wengine.

Mliokuwa mnashabikia madhila dhidi yake ndo mna la kujifunza na kujitafakari......

Wenu Ngabu aka Outlaw Immortal [emoji1548][emoji1617]
Kwenye DHIKI ni rahisi mno kueneza CHUKI. Suala ni kutafakari kwanini uzushi utokee na wengine waufurahie?
 
Kwenye DHIKI ni rahisi mno kueneza CHUKI. Suala ni kutafakari kwanini uzushi utokee na wengine waufurahie?

Labda ni roho za kutu tu walizonazo watu.

Wengine hufurahia madhila ya wengine maana furaha hiyo huwapa faraja dhidi ya madhila yao.

Wakiona mtu kapatwa na mabaya, wanazisahau kwa muda shida zao.
 
Muda huwa ni mwalimu mzuri.

Muda utasema. Mficha maradhi kifo kitamuumbua.
 
Wanajamvi habari zenu,kama mnavyojua tokea jana kumekuwepo na mkanganyiko juu ya afya ya Rais wetu John Magufuli na utata wa wapi alipo.Ghafla zikaibuka taarifa kwamba mheshimiwa Rais angehudhuria sherehe za uapishaji.

Kilichonishangaza ni kwamba TBC 1 ambo wamekuwa wakionyesha matukio yote yanayomuhusu Rais Magufuli,leo wakati sherehe zinaendelea wao walikuwa wanaendelea na vipindi vyao vya kawaida kikiwemo kipindi cha ibaada ya misa takatifu kutoka RC.
Wakuu,hii imekaaje?!!
 
Back
Top Bottom