Zuriel_cfc
JF-Expert Member
- Nov 2, 2017
- 4,104
- 9,116
Kwa siku kadhaa sasa kuna watu [majuha] kupitia hii mitandao ya kueneza na kujazana ujinga na ujuha walikuwa wameshupaza shingo na kupaza sauti zao kutoa na kueneza uongo, uzushi, na pumba zao kuwa Rais ni mgonjwa, mara amekufa, sijui kapelekwa wapi huko kwenda kutibiwa, na kadhalika.
Wengine wakaja na upumbavu wao kuwa sijui kafanyiwa mambo ya kichawi huko Ruangwa. Wakaja na video inayoonyesha moshi kwenye sehemu aliyokuwa amesimama Rais wakati anahutubia. Wengine wakasema kwenye video hiyo wameona mwanga ambao hawana uhakika ni wa nini! Hata kama ni mwanga wa jua, eti hawakujua ni wa nini.
Just stupid beyond belief.
Nadhani sasa huo upumbavu wao umemalizwa na Rais mwenyewe. Nampongeza kwa yeye kuendelea kubaki njia kuu [taking the high road] na kufanya kazi zake.
Hao majuha wanaomwombea mabaya sasa sijui watakuja na tukio gani jingine!?!! Tusubiri tuone...
Ila nimestaajabu sana. Hivi hata kama mtu hukubaliani naye kisiasa na kiitikadi ndo umwombee mabaya ya kiwango cha kifo??
Kweli kabisa?? Yaani mtu unajitoa fahamu kabisa na kumwombea kiongozi wa nchi kifo??
Kifo hakina mwenyewe. Madhila maishani hayana mwenyewe.
Nyie mlokuwa mmeshupaa kuombea na kufurahia mmenufaikaje sasa?
Magufuli akifa leo hii wewe kama liuso lako lilikuwa na chunusi kama tunda la fenesi, hizo chunusi zitatoweka?
Bure kabisa.
Hii mitandao ya kijamii imetengeneza tabaka la majuha na mapunguwani kwa kiwango kikubwa sana hadi inatisha.
Ooh eti Kigogo kasema...[sasa hivi naona wametoka kwa ‘Da Mange kasema’ na wamehamia kwa Kigogo 🤣].
Wengine wanasema kuwa eti sijui Magufuli ajitafakari, ajifunze, n.k.
Ha! Ajifunze nini? Ajitafakari nini?
Kwendeni zenu huko.
Jitazameni nyie wenyewe kwanza kabla hamjaanza kuwahubiria wengine.
Mliokuwa mnashabikia madhila dhidi yake ndo mna la kujifunza na kujitafakari......
Wenu Ngabu aka Outlaw Immortal [emoji1548][emoji1617]
Waraka kama wa lemutuz huu!
Watu wameumbuka sana jioni ya leo, zile nyimbo wakajiimbie wenyewe na familia zao maana watasubiri sana